figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Fundi mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani.
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo. Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao.
Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani.