Arumeru ni chadema vs ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru ni chadema vs ccm

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by TUNTEMEKE, Mar 1, 2012.

 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ulewakati wakuwajua ni akinanani watasimamisha bendera za vyama vyao katika uchaguzi mdogo bila shaka umesha malizika,Katika kuangalia ubora na ustahimilivu wa kisiasa tunatupia macho yetu kwenye vyama vikuu viwili CCM na CHADEMA

  1.JOSHUA NASARI(CHADEMA)
  Ni bwana mdogo ambaye akifanikiwa kuingia bungeni atakuwa ni mbunge mdogo kulikowote katika bunge letu la Tanzania,,,amepita katika kura za maoni kwa kishindo kikubwa sana na kimsingi ilitakiwa iwe hivyo kutokana na aina ya mtu mwenyewe kuwa aligombea mwaka 2010 na mzee sumari aliyetangulia mbele za haki. Joshua amepita kura za maoni kwa msaada mkubwa wa kamanda wa arusha Mh.G.lema ambaye alitumia muda wake mwingi kufundlize pesa kwaajili ya kuhakikisha Joshua anapita wakati wa kura za maoni pamoja na kipindi cha uchaguzi...Kimsingi hili halipingiki kwa sababuhadi kufikia jana Joshua alikuwa tayari ameshakusanya takribani Million 11 na magari kadhaa kwa ajili ya kuhakikisha kampeni zake zinafana sana na zinakuwa na mashiko mbele za wapiga kura wa arumeru.

  Hofu yangu juu ya Nasari ambayo naomba alifanyie kazi ili mwisho wa siku atuletaa ushindi ni hili. Katika uchaguzi wa mwaka 2010(uchaguzi mkuu) NASARI aligombea kwa tiketi ya chadema na mzee sumari aligombea kwa tiketi ya ccm,Kama wewe ni mfuatiliaji wa siasa za arumeru,katika uchaguzi ule JOSHUA NASARI ndiye mgombea pekee aliyepata nafasi ya kufanya kampeni za nguvu na za uhakika kuliko mgombea yeyote yule,Wakati huo mgombea wa ccm alikuwa kwenye matibabu ya afya yake hivyo hakupata nafasi ya kufanya kampeni.Hadi dakika ya mwisho tunakwenda kwenye kura ni JOSHUA pekee alikuwa anaonekana(kisiasa tunasema katika uchaguzi ule NASARI alisimama na KIVULI kwenye uchaguzi ule kwa sababu mzee sumari hakuwepo). Wote tunajua matokeo yalikuwaje.

  Kwa hiyo ni wazi kuwa JOSHUA anahitaji kufanya kampeni zanguvu na za uhakika kuhakikisha anapata wapigaji kura wengi kwa kipindi hiki cha kampeni...Bila shaka CHADEMA wataliona hili na watampa sapoti ya kutosha japo sijui kama watu waliopewa jukumu hili wanaweza kulitendea haki

  2.SIOI SUMARI
  Huyu ni mgombea toka familia ya mzee sumari(mtoto wa mzee sumari) ni mgeni kabisa katika siasa za Tanzania na hana uzoefu na purukushani zozote zile za hapa tz,muda mwingi wa maishha yake amekuwa nje akisoma na shughuli mbalimbali....Nilipata kufanya mazungumzo naye siku moja....ni wazi hata kuongea kiswahili sanifu na kilichonyooka kwake ni tatizo.

  Sumari anabebwa na jina la baba yake mzee sumari katika uchaguzi huu,na katika ushindi wa kishindo wa kura za maoni aliopata haikuwa kazi yake pekee bali ni msaada wa ndani kabisa toka kwa viongozi wa ccm wakiongozwa na mezee mkongwe na mwenye sifa ya kushika wizara nyingi hapa tz kipindi alipokuwa waziri(E Lowassa).Mh.El ametumia nafasi yake kuhakikisha jimbo linabakia katika familia ile na huyu kijana anapita katika kura za maoni.

  Hofu yangu juu ya SUMARI ni kucheza ama kulizoea jukwa la siasa za tz,namna ya kujieleza namna ya kushawishi wapiga kura itakuwa kikwazo sana katika kampeni zake. Lakini ni nani asiye fahamu ccm na propaganda zake....Nguvu zote za ccm kwa sasa zinaelekezwa ARUMERU..nadhani tumeshajionea wenyewe hadi dakika hii si Chiligati,Mukama,Nape,Lowasa,n .k wapo arumeru kwenye jombo.si muda mrefu tutasikia mzee mkapa na KIKWETE mwenyewe ataelekea huko.
  Imani ya ccm ni kwmaba hata mende anauwawa kwa nguvu kubwa....na wanataka sana kulichukua jimbo lile ilikudhihirisha uma kuwa wao bado wanakubalika katika jamii.....na kama watashinda watakuwa wameshinda majimbo matatu tofauti katikachaguzi ndogo na hii itawapa mtaji wa kisiasa siku za usoni japo bado sikio la kufa halisikii dawa.

  NGOMA NGUMU IPO hapa kwenye kampeni managers na operation kamandas wa hivi vyama....Je chadema mtu mliyempeleka huko atafanikisha ushindi?,Je ccm mtaweza kushindanana nguvu ya umma?hapa EL pale G.lema...hapa Nape nauye....kule Jonh Mrema....ukienda mbali zaidi unamwona Kikwete na mkapa wakifunga kampeni huku Dr.slaa na Kamanda wa anga wanafunga kampeni.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Very good msg. Ni wakati muafaka sasa CDM kudraw attention
   
 3. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  TUNTEMEKE,
  Huu ujumbe kweli umeuchambua kwa makini mwenye kusuka asuke na mwenye kunyoa anyoe...uchambuzi upomakini
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Bila shaka CDM wanaliona hili la tuntemeke lipo sahihi,inatakiwa kuwa makini
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wewe ni nani hapa nchini,ni mchambuzi wa mambo ya siasa?Katika hili naona umefikiria mbali sana...go goo....goooo
   
 6. Kakati

  Kakati Senior Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapana huu sio uchambuzi. Maelezo yote yana lengo la kumtaja Lowasa. Yaani hawa watu hawachoki kumtaja huyu mtu. Jamani Lowasa ni mTanzania kama wengine. Shida ni moja, sio mtu msafi mbele ya jamii yetu. Msipoteze muda wenu hasafishiki. Si apumzike ale hayo mahela aliyokwishapata?

  Pili mwelekeo mada yenyewe imeegeme/ kupendelea CCM. Huwa nafurahi kama ukiamua kupongeza kitu basi kiwe kinafaa. Hakika uchambuzi huu sio makini ki hivyo!
   
 7. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kati ya siku ambazo nimefurahia message zako, ni leo. Kwa sababu umetoa caution kwa CHADEMA ambayo CHADEMA wanatakiwa wajue hilo na kwa kweli uchambuzi wako umekuwa unbiased unlike other posts. Hongera saana. CCM pia umewapa caution. Kulingana na message yako, you wanted fair play na umakini kwa kila chama.
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nimeupata NAHAVACHE,Ila napenda kuuliza swali hili,je ningekuwa na sema uozo wa ccm hapa ungesemaje? au ni kwasababu nimeisema chadema ndio nimekuwa biased?
   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  umetufumbua macho mkuu kama jamaa hata lugha inamsumbua basi ccm watatumia nguvu nyingi kupita maelezo nahisi ccm yote kuhamia AR.Huko inaweza kuwa mara mbili au zaidi ya igunga
   
 10. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hapo ni kazi ya kufa mtu. katika ccm kwenye kutatokea makundi mawili. moja ni lile linalotaka kumwonesha baba mkwe wa Sioi kuwa pesa haiwezi kununua kila mtu na kila mtu na hivyo huenda watakuwa waumini wa siri wa magwanda na kuwapa mbinu na mikakati ya kufisadi kura ili kuonesha ubabe wao na kundi la pili ni la baba mkwe ambalo kwao ushinfi ni lazims kuliko kitu chochote na mtu yeyote. Kwa vyovyote vile magwandwa wana kundi kubwa la waumini wao kutokea upande w pili wa magamba. 75% ya ushindi iko kwa Nassary kwa vyo vyote vile.
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu Royals ulosema ni kweli wasi wasi wangu ni rushwa na njaa za machalii, labda TAKUKURU wapige kambi vijini kuzuia watu wasiuze hizo card za mpiga kura!!!! Unaweza kuona watu wengi kwenye mikutano ya kampeini kumbe watu waisha uza vyeti vya kupiga kura kwa kuwekeza kama ilivyo kuwa Igunga walio wekeza kwa kupewa mahindi!!!!! Rushwa inayotolewa na CCM ni janga la kitaifa!!!!!

   
 12. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ni mwendo wa rushwa kwa kwenda mbele(CCM),,,,hawatakuwa na njia yoyote ile ya kunusuru SUMARI asigalagazwe kwenye uchaguzi huu...
   
 13. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Kiongozi labda hukumuelewa NAHAVACHE...tunaosoma between lines jamaa amesema umekuwa unbiased na sio biased. Kwa hiyo chunguza kwa makini alichokiandika.
   
 14. m

  movichboy JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 212
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Mkuu kwanza nashukuru sana kwa uchambuzi wako kwa kuwa umekuwa ni very constructive kwa CDM lakini upo umetoa angalizo la msingi sana hasa kwa nguvu kubwa ambayo huwa wanatumia wenzetu wakati wa hizi chaguzi ndogo. Ki msingi sioni tabu sana anapekwenda fulani na fulani kutoka kwenye chama chao kwani naona wote mvuto wao kwa wananchi hautofatiani sana ila kinachokera ni nguvu kubwa ya rasilimali vitu inayokuwa inatumika kwani naona ni kama kuwaambia wananchi sisi tuna hiki na hiki mtuchague na msiwachague wale kwa kuwa hawana hiki na hiki. Kwa bahati mbaya sana naona vyama vyetu vingine hasa CDM tumeanza kujikuta aidha kwa kujua au pasipo kujua kuingia kichwa kichwa na kuanza kutumia mbinu zile zile wanazotumia wenzetu matokeo yake tunakuwa tunashindwa, siamini kama huwa tunashindwa kihalali ila kama ndivyo basi ni vizuri tukaangalia kwanza weakness za wenzetu na kutengeneza mbinu zinazoweza kutusaidia kupata ushindi, ni kweli tunahitaji MAGARI, PESA N.K lakini ni lazima tukumbuke aina ya wapiga kura wetu na kutafuta njia madhubuti za kuwashawishi ili tusionekane kuwa sasa kuwa nasi tuna kama walicho nacho CCM basi tupewe kura HAPANA tukumbuke CDM ni chama cha wananchi wa kawaida kabisa hivyo tuwaombe KURA kwa kuwaonesha DIRA yetu sisi ni UKOMBOZI wao wote.
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyo kijana wa Sumari nadhani ndiyo chaguo la Arumeru.
   
 16. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  HABARI TOKA ARUMERU MASHARIKI

  Dk SLAA AWASHA MOTO ARUMERU MASHARIKI

  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amewataka viongozi wa chama hicho katika Jimbo la Arumeru Mashariki, kukamata magari ya viongozi wa CCM watakaopita katika maeneo yao, kwa lengo la kununua shahada za kupigia kura na kutoa rushwa.
  ...
  Akizungumza na viongozi wa chama hicho wa kata zote 17 za jimbo hilo katika mkutano uliohudhuriwa pia na viongozi wa chama hicho mkoani Arusha, mtendaji huyo alisema kila raia ana haki ya kulinda amani na usalama wa eneo lake.

  "Kukamata wahalifu si kazi ya polisi pekee yao, nawaagiza kuwa kuanzia sasa muwe makini na CCM maana tayari magari yao yameanza kuonekana vijijini wakiwarubuni wananchi, mkiwaona wakamateni,"alisema Dk Slaa.

  Katibu huyo, alisema baada ya kukamata magari na wanachama wa CCM watakaotoa rushwa, hatua zichukuliwe kuwafikisha katika vituo vya polisi na kama wakisumbua wawasiliane na viongozi wa kitaifa wa Chadema waliopiga kambi katika jimbo hilo.

  "Kamateni hao wanaokiuka sheria msidanganyike kuwa kazi hiyo ni ya polisi, wakiwasumbua tupigieni simu na hili msiwe na hofu yoyote makamanda wangu," alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa aliwataka wananchi wa Arumeru Mashariki, kutambua kuwa kura moja inathamini kubwa kuliko baiskeli au gari na kwamba lazima wazilinde kura kwa gharama yoyote.

  Akizungumzia mkakati wa ushindi wa chama hicho, katika jimbo hilo, Dk Slaa aliwataka viongozi 10 wa Chadema katika kila kijiji kujiunga na kuchukua fomu za kuwajua wapiga kura na kuhakikisha kuwa wanakipigia kura chama hicho.

  "Mtapewa fomu leo na kila kiongozi ataorodhesha watu wake tayari kwa mkakati wa kampeni na hili sio kosa kwani tunataka kuhakikisha kuwa tunajua mapema kuwa ushindi wetu ni wa kura ngapi,"alisema Dk Slaa.

  Alisema utaratibu huo pia utawezesha kuanza kwa kampeni za nyumba kwa nyumba kwa kila kiongozi na kwamba katika eneo ambalo kura zitakuwa chache kiongozi anayehusika atatoa maelezo.

  Hata hivyo, alisema kazi ya kuhakikisha Chadema inashinda katika jimbo hilo ni ya wakazi wa jimbo hilo na si ya Mbowe wala yeye.

  Aliwapongeza viongozi walioshiriki katika mkutano huo kwa kumteua Joshua Nasari kuwa mgombea wa chama hicho
   
 17. T

  Twaa Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwa kweli CCM wanatumia nguvu kubwa sana ili kuhakikisha ushindi lakini ukweli utabaki palepale kwamba kifo cha CCM chaja! Watachukua jimbo lakini watatekeleza ahadi zao?!
  Kwa mda uliobaki sio mda wa CHADEMA Kuchukua jimbo la Arumeru hata kidogo kwani hawataweza kutimiza ahadi kwa wakati then ni wakati mwafaka kwa CHADEMA kujipanga mwaka 2015!
  Tutazame mambo yanavyoenda kule Igunga, CCM ilishinda lakini alieshinda hajatimiza ahadi mpaka sasa na mbunge mwenyewe hakubaliki hata kidogo hata akiitisha mkutano na wananchi wa jimbo lake!
  Kazi kwenu wana CHADEMA wa Arumeru!.
   
Loading...