Arumeru: Mume amuua mke kwa shoka baada ya kunywa chai Sherehe za Krismasi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mwanamke aliyetambuliwa kwa Majina ya Marry Richard Mushi mkazi wa kijiji cha Kilinga Wilayani Arumeru ameuawa kinyama kwa kukatwa na shoka na mtu anayedaiwa kuwa ni mumewe, Moses Pallangyo baada ya kupikiwa chai kwenye sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo limetokea mapema leo Desemba 25/2019 majira ya mchana katika eneo hilo.

Inadaiwa kuwa mwanaume huyo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili alitekeleza mauaji hayo punde Mara baada ya kunywa chai aliyokuwa ameandaliwa na mkewe na haikufahamika iwapo jamaa hiyo alichukizwa kuona mkewe akimpatia chai badala ya chakula maalumu wakati wa sikukuu ya Krismasi.

Tukio hili limetokea ikiwa ni wiki tatu tangu marehemu aanze kuishi na mtuhumiwa huyo kama mke na mume.

Baba wa mtuhumiwa Mzee Latiaeli Samson Pallangyo amesema hapakuwa na ugomvi wowote na walitegemea kusherehekea siku ya xmass vizuri mara baada ya Marehemu kuwapika chai na kisha kuendelea na shughuli za kawaida mpaka mauti ilipomfika kwa kupigwa na shoka chumbani kwake.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye alifika katika eneo la tukio muda mchache baada ya tukio, mbali na kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha kilinga, amesema tayari vyombo ya usalama vimeanza msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa ambaye alitoweka punde mara baada ya kutekeleza unyama huo.

Muro amewataka wananchi kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake na kuwataka wananchi wenye kujua taarifa za alipokimbilia mtuhumiwa wasaidiane na vyombo vya usalama.

Ends.......

IMG-20191225-WA0019.jpeg
 
Kwanza kikawaida hapo palitakiwa pawe ni eneo la tukio la kijinai (Crime Scene) kwa ivo ilitakiwa lifanyiwe kazi (Processed) bila ya kuwepo kwa watu wasio na utaalamu wa mambo ya kihalifu.

Kesho ukiuliza kama picha za eneo la tukio zilichukuliwa, sidhani kama watakuwa nazo. Halafu wewe unakuja na mambo ya "Autopsy".
 
Mwanamke aliyetambuliwa kwa Majina ya Marry Richard Mushi mkazi wa kijiji cha Kilinga Wilayani Arumeru ameuawa kinyama kwa kukatwa na shoka na mtu anayedaiwa kuwa ni mumewe,Mosses Pallangyo baada ya kunywa chai aliyokuwa ameandaliwa na marehemu katika kushererehekea sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo limetokea mapema Leo desemba 25/2019 majira ya mchana katika eneo hilo.

Inadaiwa kuwa wanaume huyo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili alitekeleza mauaji hayo punde Mara baada ya kunywa chai aliyokuwa ameandaliwa na mkewe na baadae kuanza kutayarisha chakula kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi.

Tukio hili limetokea ikiwa ni wiki tatu tangu marehemu aanze kuishi na mtuhumiwa huyo kama mke na mume .

Baba wa mtuhumiwa Mzee Latiaeli Samson Pallangyo amesema hapakuwa na ugomvi wowote na walitegemea kusherehekea siku ya xmass vizuri mara baada ya Marehemu kuwapika chai na kisha kuendelea na shughuli za kawaida mpaka mauti ilipomfika kwa kupigwa na shoka chumbani kwake.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye alifika katika eneo la tukio muda mchache baada ya tukio, mbali na kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha kilinga, amesema tayari vyombo ya usalama vimeanza msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa ambaye alitoweka punde mara baada ya kutekeleza unyama huo.

Muro amewataka wananchi kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake na kuwataka wananchi wenye kujua taarifa za alipokimbilia mtuhumiwa wasaidiane na vyombo vya usalama.

Ends.......

IMG-20191225-WA0020.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah Apumzike kwa amani, Huyo jamaa ana akili timamu kweli? Au ndo mambo ya ndoa huenda jamaa aligundua kitu?

Lakin kwanini afanye hivi? Eeh Mungu turehemu binadamu wamekuwa wakatili sana sikuhizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom