ARUMERU: Mtihani kwa CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ARUMERU: Mtihani kwa CCM?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Kiungani, Feb 24, 2012.

 1. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa mara nyingine tena CCM imejikuta katika uchaguzi ambao unakifanya chama kiwe na kionyeshe msimamo wa sera zake, hasa mapambano dhidi ya ufisadi na kuvuana magamba.

  Kipimo cha kwanza kilikuwa Igunga, ambapo mgombea wao Dr. Kafumu aliibuka kidedea. Kugombea na kushinda kwa Kafumu kule Igunga inaweza kutafsiriwa kama ni ushindi dhidi ya Ufisadi haswa ikitiliwa maanani kuwa Rostam Aziz, mtuhumiwa wa ufisadi CCM, ilibidi aachie hicho kiti. Hata hivyo huu mtihani wa Igunga haukuwa mgumu sana kwani ilikuwa ni rahisi kwa CCM kuonyesha kuwa katoka fisadi Rostam anaingia Kafumu, ambaye ni kitu kingine tofauti (japo kuna watakaodai kuwa naye ni fisadi pia).

  Kwa Arumeru, pamoja na kuwa kiti kimekuwa wazi kwa mapenzi ya Mungu kufuatia kifo cha Mzee Jeremiah Sumari, lakini uzibaji wa pengo hilo ni mtihani mkubwa kwa CCM.

  Mshindi wa kura za maoni ndani ya CCM ni Sioi Sumari, mtoto wa kiume wa Mzee Jeremiah Sumari. Kama ada, NEC ya CCM itakaa na kupitisha jina la mgombea wa CCM kama ilivyo taratibu za chama, na bila kutengua matokeo ya kura za maoni, basi mgombea wa CCM atakuwa ni Sumari.

  Kwa angalizo la haraka haraka, hapa inaonekana kama siyo tatizo hata kidogo. Mzee Sumari kafariki, mtoto wake kashinda kura za maoni na kupitishwa na NEC kama mgombea halali. Hakuna shida, siyo? La hasha.

  Tukiangalia kwa undani, kuna ugumu kuliko picha ya awali. Kijana Sioi Sumari, ni mkwe kwa kumuoa binti mkubwa wa Edward Lowassa. Kijana Sumari amekuwa karibu zaidi sana na wakwe zake akina Lowassa kiasi kwamba anafahamika na hata yeye kujitambulisha kama mmojawapo ya watu wachache sana ambao wana sikio la Lowassa, wakati wowote. Familia ya Lowassa imefungamana sana na familia ya Sumari, na huwezi kupenyesha hata upana wa nywele katika mfungamano huo.

  Ni wazi na kwa mantiki ya kawaida kuwa Sumari alipata ushauri na pengine baraka pia za mke wake, binti Lowassa, na si ajabu pia hata wakwe zake ili aweze kugombea kiti hiki cha Arumeru. Kushinda au kushindwa itategemea pia na support anayopata kutoka kwa chama na ndugu, wakiwapo pia wakwe zake, Lowassa.

  Sidhani kama CCM itafumbia macho ukweli huo, na kama ni hivyo je, CCM itasimama bega kwa bega na Sumari, Lowassa huko Arumeru? Je, ikifanya hivyo CCM itakuwa inatuma ujumbe gani kwa Lowassa na wana-CCM kuhusu suala la kuvuana gamba?

  CCM inaonyesha kuelekeza nguvu zake Arumeru kwani Mwigulu Nchemba tayari katumwa kupeleka ‘majeshi na takrima’ Arusha. Kwa hiyo uwezekano kuwa CCM itajitenga na Arumeru ni mdogo, ila CCM NEC bado inaweza kumuengua Sumari asiwe mgombea wa CCM. Hali hiyo ikitokea (binafsi sidhani kama itakuwa hivyo, na kauli za Tendwa ni uthibitisho kuwa Sumari anabebwa), je Lowassa atasimama kidete kutetea Arumeru kama alivyomsaidia Mzee Sumari mwaka 2010?

  Arumeru ni kipimo kizuri kwa CCM kuhusu aidha kuachana na gamba, fisadi Lowassa na tawi lake Sumari au kuukumbatia u-CCM na magamba na ufisadi wake sasa na hata milele.
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ndo maana Nnape amefunga domo lake,vita ya panzi shibe ya kunguru
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Suala la kujivua gamba lilishaisha! EL anakubalika sana kwa umma
   
 4. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ushauri wako kwa CCM unatoa tahadhali ambayo si vizuri kuipuuza. Hata hivyo si sahihi kumhukumu Sioi kwa sababu ni mkwe wa Lowasa. Hata angekuwa mtoto wa Lowasa, hawezi kukutaliwa kwa makosa au tabia ya baba yake. Hiyo ni kinyume kabisa cha haki za msingi kumhukumu mtu kwa tabia au makosa ya wazazi wake. Kwa upande mwingine, iwapo Sioi amepata kura za maoni kwa rushwa,CCM lazima ilinde sera ya kupinga rushwa. Bila kama fedha alizotumia zimetoka kwa Lowassa au kwa shetani yeyote. Issue hapa ni rushwa siyo sioi Kama mtu, au Lowassa au ukoo wa Lowassa.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mleta mada unaijuwa dhana ya kujivuwa gamba au unakisia tu? Lowassa yuko chama kipi? Mnapenda kweli fitina nyinyi. Lakini kumbekeni kuwa nyinyi wote ni vitoto na vijukuu vya CCM, CCM ndio pekee inayoweza kukamata fimbo ikawatandika na kisha nyinyi ndio mtaomba msamaha, mmekaa kama watoto watukutu, dawa yenu fimbo tu.

  Ikiwa Laibon ni CCM hivi magwanda mnategemea kushinda Arumeru? Mawee.

  Hili litakuwa pigo lililonyooka, pigo takatifu, kama hamumjui Lowassa, basi mtamjuwa huko Arumeru.

  Siku ya kutangazwa matokeo, au hata kabla, InshaAllah ntaingia hapa niwaulize, "vipi, kwemaa?".

  Hivi bado mtakuwa na hamu na chama? mmepigwa Igunga, mkagaragzwa vibaya sana Uzini na sasa mnatandikwa kwa fimbo ya kimasai huko Arumeru.

  Nimeona nyuzi mmeanza kusingizia rushwa! duh, kazi kweli kweli. Mmeshaanza kunung'gunika.
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  M haiwezi kushinda uchaguzi mdogo hata ukifanyika msoga.

  Rushwa na mabavu na uvunjifu wa amani ndio tegemeo lao.chadema tunaamini katika haki na vilevile tunajua huwezi kulima leo na kuvuna leo.
  Watanzania wameielewa chadema na wameamua kuiunga mkono pamoja na hila zote za ccm.
  Ccm si wamoja tena ila wanaonekana wamoja kwa sababu kila mmoja anajua wizi wa mwenzake.

  Siku ipo na inakaribia.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  haubadiki tu? tumeshakwambia lowasa hakubaliki na umma wa watanzania, anatumia nguvu kubwa sana ya fedha, huko si kukubalika!!!!
   
 8. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
   
 9. Hakeem makamba

  Hakeem makamba Senior Member

  #9
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Binafsi sioni tatizo kwa SIOI kupitishwa na chama chake, hata kama angekuwa kao binti wa Mizengo.Hili ni suala lao, hoja hapa ni jinsi ya kumshinda Sioi chama chake, hata mimi ningependa kuwa mkwe wa Lowasa.Alaaaa
   
Loading...