Arumeru Mashariki: Mwenyekiti wa CCM ahamia CHADEMA

CCM sasa maji ya shingo huko Arumeru MAshariki; madiwani wake hujiuzulu, wenyeviti wachapa malapa na wanachama walalahoi ndio usipime walivyochanganyikiwa kwa vituko vya Mzee Mkapa huko wiki majuzi.
 
Angalizo: wanachama wanaohamia cdm kipindi hiki cha kampeni arumeru wawe SCANNED before ili kuepusha kupokea VIRUS
 
"Mwenyekiti wa CCM wa serikali ya kitongoji" Hakuna nafasi hiyo kwenye CCM niijuayo mimi! Huyo kakupigeni mchanga wa macho, na kama hata nyinyi hamfahamu mfumo(structure) ya CCM basi mna walakin pia!

Anaweza kuwa hajakieleza vizuri hicho cheo, lakini si lazima ujue "structure" ya chama chochote ili kujua kuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji ni part ya local government, na nafasi hiyo hugombewa kupitia chama cha siasa. Kwa mantiki hiyo huyo mwenyekiti wa serikali ya kitongoji alichaguliwa kupitia tiketi ya ccm. Changa la macho umejipiga mwenyewe.
 
Hongera kwa kuachana na wauwaji,
baba wa taifa ...basi tu mkapa!!
 
Minja ni Mmeru na wala siyo mchaga..meru inamwingiliano mkubwa sana na uchagani..
 
Mwenyekiti wa CCM wa Serikali ya Kitongoji cha Madukani,eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni, Godzed Minja, juzi amerudisha kadi ya CCM na kujiunga na CHADEMA, wakati makada wa chama hicho wakimnadi Mgombea waoNassari wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CHADEMA, Mwenyekiti huyo Minja, alisema kuwa amefanya uamuzi huo kutokana na kuona CCM haina sera zaidi ya kusambaza matusi na kashfa badala ya kujibu hoja za msingi.

"Mimi naahidi nitakuwa mwana Chadema safi na mwaminifu na sitarudi nyuma katika mapambano haya, CCM imepoteza mwelekeo,'' alisema Minja.

Alisema kuwa atatumia muda wake mwingi kuhakikisha CCM katika Kata ya Mbuguni inapotea kabisa kwa sababu hawana sera za kuwaeleza wananchi juu ya ugumu wamaisha waliyosababisha na kuchangia viongozi wa chama hicho kupata wakati mgumukwa Wananchi.

Naye Mchungaji Israel Natse, akizungumza wakati akimnadi Mgombea wao, Nassarialisema kuwa eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni CCM imekwisha kwa sababu wanachama wengi wamehama chama hicho na kujiungana Chadema, kutokana na sera zao za matusi mbele ya watoto wadogo.

Alisema kuwa wanachama zaidi ya 300 wanasubiri Katibu wa chama hicho Taifa Dk.Slaa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ili wakabidhi kadi hizo na kukabidhiwa kadiza Chadema mbele yao.

Mwananchi.

Minja ni jina la kichaga inapendeza kama kafuata sera CDM badala ya uchaga. Dunia ina mambo mengi yanayoonekana na yasioonekana kwa akili ya kawaida
 
matusi yalisababisha aliye kuwa mbunge wangu kuanguka vibaya mno kwenye uchaguzi wa 2010
 
Back
Top Bottom