Arumeru: Kijana amuua mama yake mzazi kwa shoka na kunywa damu yake

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kijana anayedhaniwa kuwa na matatizo ya Akili, Daniel Emanuel(32) mkazi wa Sakila Chini wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha, amemuua kikatili mama yake mzazi kwa kumkata vipande kwa shoka na kutenganisha kiwiliwili kisha kunywa damu yake.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Jana majira ya SAA 9 Alasiri nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Sakila chini wilaya ya Arumeru,mkoani hapa.

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Jonathan Shanna alimtaja marehemu kuwa ni Eliamulika Emanuel mwenye umri wa miaka 79 mkazi wa Sakila chini wilayani humo ambaye alikuwa akiishi jirani na mtuhumiwa ambaye ni mama yake.

Kamanda Shana amefafanua kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alichukua shoka na kumkata shingo mama yake na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kisha kumkata miguu yote na kuitenganisha na kiwiliwili.

Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alichukua kikombe cha maji na kukinga damu iliyokuwa ikichuruzika kwenye majeraha na kunywa jambo lililowastaajabisha wakazi wengi wa eneo hilo.

Hata hivyo polisi waliofika eneo la tukio hawakukuta damu yoyote ya marehemu baada ya mtuhumiwa kufanikiwa kuinywa kwa lengo la kupoteza ushahidi.

Kamanda alidai kuwa mtuhumiwa alijaribu kukimbia baada ya kuwaona polisi, hata hivyo askari hao walifanikiwa kumkamata na kwamba baada ya kufikishwa kituo cha polisi amegoma kuongea chochote.

Kamanda ameongeza kuwa mtuhumiwa atafikishwa katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini iwapo anamatatizo ya akili na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Kamanda Shanna ametoa wito kwa jamii kuacha kuishi kwa mazoea na mtu anayedhaniwa kuwa na matatizo ya akili badala yake iwapeleke katika hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu.

Ends....

IMG_20200516_095808.jpeg
IMG_20200516_095413.jpeg
IMG_20200516_095026.jpeg
IMG_20200516_094947.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo umri wa huyo mama na mwana nadhani kuna shida hapo! 79-32=47, ina maana mama alimzaa huyo mwanae akiwa na 47 yrs!

Mama r.i.p, wafiwa poleni!
 
Ugumu wa maisha ndo kipimo cha akili.

Vijana wengi tunapenda shortcut ambazo kikanuni za utafutaji hazipo,umaskini usitufanye tuonekane hatuna akili bali Umaskini ndo njia pekee ya kukufany uthink extra miles namna sahihi ya kupata kipat,kuliko kufany ujinga km huo unaoonyesha harufu ya ushirikina.

Make hay when the sun is still shinning.

Tupgie kazi tumake money.
 
Back
Top Bottom