Arsena vs Liverpool Panachimbika Emirates.

Arsena vs Liverpool Panachimbika Emirates.

XinKumi

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
1,276
Reaction score
1,146
Akiwa kacheza mechi tisa za ligi na kufunga magoli nane msimu huu huku mwenzie akiwa kacheza mechi tatu za ligi na kufunga magoli sita,hii inaifanya safu ya ushambuliaji ya liverpool kuwa tishio zaidi kwa msimu huu kwa pamoja wanaunda combination ijulikanayo kama SAS.Hapa nawazungumzia Daniel Sturridge anayeongoza kwa magoli msimu huu na Luis Suarez.
Akitokea Real Madrid huku akiwa katika form ya hali ya juu,inamfanya kiungo huyu aliyehamia Arsenal kuwa ni moja kati ya viungo bora kwa sasa katika ligi kuu nchini England,Mesut Ozil amekuwa chachu ya mafanikio ya Arsenal kwa sasa.
Liverpool katika mechi zake tano ilizocheza nyumbani imepoteza mchezo mmoja tu ambao ulikuwa kati yake na Southampton huku ikiwa imeshinda mechi mbili na kutoa suluhu mechi mbili katika mechi zake nne za ugenini.
Arsenal yenyewe inaonekana kufanya vizuri zaidi ugenini kwani katika mechi tano imeshinda nne na kutoa suluhu moja dhidi ya westbromwhich albion.
Liverpool wanatarajia kumrudisha dimbani kiungo wao wa kutumainiwa Philipe Coutinho huku wakimkosa beki wao mahiri Jose Enrique.
Arsenal wanaongoza ligi hiyo wakiwa na point 22 wakifuatiwa na Chelsea pamoja na Liverpool zenye idadi sawa ya point 20 ila zikitofautiana idadi ya magoli.
Tukutane Emirates Stadium kesho,wale wenzangu wa Liverpool muda wetu ndio huu na wale Arsenal,hongereni kwa mwanzo mzuri.
 
Arsenal wanaaibishwa kesho
 
watu hawapendi kuiona ARSENAL yetu ikishinda lakin leo emirates patachimbika na tutashinda inshallah
 
SAS combination kazi yao ni kufunga(na lazima wafunge) suala la nani ataondoka na point zote 3 ni mchezo tu utakao amua
 
Hakika wasiozipenda ARSENAL na YANGA mwaka huu mioyo yenu MONGONYOMONGONYO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom