Armed gangs Msasani/ vikundi vya wahalifu wanaotumia silaha maeneo ya Msasani

Gadaph Mousolin

New Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
2
Reaction score
0
Kumekuwa na taarifa ambayo imekuwa ikisambaa katika mitandao mbali mbali ya kijamii ikiwamo wavuti ya UNDSS.

Katika taarifa hiyo imeripotiwa kuwa maeneo ya Masasani kwa maana ya ukanda mzima wa Peninsula Coco beach, Sea cliff, Saint Peters, Double Tree, Toure drive na maeneo mengine ya Msasani kuwa kuna vikundi vya wahalifu wanaotumia Mapanga, Fimbo na silaha nyingine ambao huwapora wakazi na wapita njia wa maeneo hayo wanaotembea kwa miguu na hata wanapokuwa kwenye magari binafsi; Huwavamia na kuwapora vitu mbali mbali na kukimbilia kwenye vichaka na maeneo ya mapango yaliyo karibu na maeneo hayo huku taarifa hiyo ikibainisha kuwa matukuo hayo hufanyika zaidi nyakati za usiku kuanzia saa 21:00hrs na 22:00hrs.

Taarifa rasmi toka katika vyanzo vya kuaminika ni kwamba hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hiyo na hizo ni taarifa za kizushi zinazoenezwa na bwana mmoja anayeishi maeneo ya baina ya Golden Tulip na Sea Cliff ambaye haijajulikana anadhamira gani mapaka sasa, lakini pia hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa Polisi Kinondoni kuhusiana na matukuo kama hayo.

Doria zimekuwa zikifanyika usiku na mchana ikiwamo doria za miguu na magari kuzunguka maeneo yote hayo na Mkoa mzima wa Kinondoni kwa ujumla.

Hata hivyo UN wanatakiwa kuchunguza kwanza taarifa wazoletewa ili kuweza kutoa taarifa za kweli na za uhakika siyo kila taarifa inayoripotiwa kwao wanaisambaza kama ilivyo huko ni kukiuka taratibu na kanuni za utoaji taarifa hizi zisizo na ukweli zinazotisha watu pasipo sababu ya msingi.
 
Mkuu unapinga nini uhalifu Dar ni wa hatari sana hakuna eneo lililo salama..hao police unaosema wanzunguka huko tuu au ipoje kuna siku mtu kapigwa risasi katika dala dala na vibaka wakaondoka na hela na boxer yao,majuzi tuu umetokea uwizi wa kutumia siraha Chanika huko bank,acha matukio ya Sinza,bamaga wiki iliyopita mtu kapigwa risasi mbele ya watoto wadogo haya ni baadhi ya Matukio ya siku kadhaa tuu,mwizi akiweza kuiba Bamaga atashindwa maeneo uliyataja..sijakuelewa Mkuu mimi nilidhani unakuja na suruhisho ya matukio ya kiharifu wewe unasema tena hakuna Matukio ya kiharifu ?
 
Kumekuwa na taarifa ambayo imekuwa ikisambaa katika mitandao mbali mbali ya kijamii ikiwamo wavuti ya UNDSS.

Katika taarifa hiyo imeripotiwa kuwa maeneo ya Masasani kwa maana ya ukanda mzima wa Peninsula Coco beach, Sea cliff, Saint Peters, Double Tree, Toure drive na maeneo mengine ya Msasani kuwa kuna vikundi vya wahalifu wanaotumia Mapanga, Fimbo na silaha nyingine ambao huwapora wakazi na wapita njia wa maeneo hayo wanaotembea kwa miguu na hata wanapokuwa kwenye magari binafsi; Huwavamia na kuwapora vitu mbali mbali na kukimbilia kwenye vichaka na maeneo ya mapango yaliyo karibu na maeneo hayo huku taarifa hiyo ikibainisha kuwa matukuo hayo hufanyika zaidi nyakati za usiku kuanzia saa 21:00hrs na 22:00hrs.

Taarifa rasmi toka katika vyanzo vya kuaminika ni kwamba hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hiyo na hizo ni taarifa za kizushi zinazoenezwa na bwana mmoja anayeishi maeneo ya baina ya Golden Tulip na Sea Cliff ambaye haijajulikana anadhamira gani mapaka sasa, lakini pia hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa Polisi Kinondoni kuhusiana na matukuo kama hayo.

Doria zimekuwa zikifanyika usiku na mchana ikiwamo doria za miguu na magari kuzunguka maeneo yote hayo na Mkoa mzima wa Kinondoni kwa ujumla.

Hata hivyo UN wanatakiwa kuchunguza kwanza taarifa wazoletewa ili kuweza kutoa taarifa za kweli na za uhakika siyo kila taarifa inayoripotiwa kwao wanaisambaza kama ilivyo huko ni kukiuka taratibu na kanuni za utoaji taarifa hizi zisizo na ukweli zinazotisha watu pasipo sababu ya msingi.

We naona unamaslahi nao hao wezi. Jaribu utembee na gari wakati hujafunga milango halafu taratibu ndio utajua hali halisi huko. Pale kwenye bump ya Officers mess watu wanalia kila mara. Nenda kapunge upepo jioni uone kitakachokutokea utavuliwa hadi suruali. Sio kutishana hivyo ndio hali halisi
 
Uhalifu mbona upo tu kila sehemu ya dar es salaam mleta uzi, labda mleta uzi huu hayuko tz
 
Mleta Uzi hebu pita pale salender bridge mida ya saa tatu usiku au zaidi na ujifanye gari yako imeharibika upaki pembeni uone kitakachokutokea, na kutoka hapo kwenye daraja mpaka kituo cha polisi ni kama mita ishirini
 
Kumekuwa na taarifa ambayo imekuwa ikisambaa katika mitandao mbali mbali ya kijamii ikiwamo wavuti ya UNDSS.

Katika taarifa hiyo imeripotiwa kuwa maeneo ya Masasani kwa maana ya ukanda mzima wa Peninsula Coco beach, Sea cliff, Saint Peters, Double Tree, Toure drive na maeneo mengine ya Msasani kuwa kuna vikundi vya wahalifu wanaotumia Mapanga, Fimbo na silaha nyingine ambao huwapora wakazi na wapita njia wa maeneo hayo wanaotembea kwa miguu na hata wanapokuwa kwenye magari binafsi; Huwavamia na kuwapora vitu mbali mbali na kukimbilia kwenye vichaka na maeneo ya mapango yaliyo karibu na maeneo hayo huku taarifa hiyo ikibainisha kuwa matukuo hayo hufanyika zaidi nyakati za usiku kuanzia saa 21:00hrs na 22:00hrs.

Taarifa rasmi toka katika vyanzo vya kuaminika ni kwamba hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hiyo na hizo ni taarifa za kizushi zinazoenezwa na bwana mmoja anayeishi maeneo ya baina ya Golden Tulip na Sea Cliff ambaye haijajulikana anadhamira gani mapaka sasa, lakini pia hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa Polisi Kinondoni kuhusiana na matukuo kama hayo.

Doria zimekuwa zikifanyika usiku na mchana ikiwamo doria za miguu na magari kuzunguka maeneo yote hayo na Mkoa mzima wa Kinondoni kwa ujumla.

Hata hivyo UN wanatakiwa kuchunguza kwanza taarifa wazoletewa ili kuweza kutoa taarifa za kweli na za uhakika siyo kila taarifa inayoripotiwa kwao wanaisambaza kama ilivyo huko ni kukiuka taratibu na kanuni za utoaji taarifa hizi zisizo na ukweli zinazotisha watu pasipo sababu ya msingi.

wewe ni nani...msemaji wa idara gani?
 
ni ukwel kabisa.
huwezi toka sea cliff usiku ukasema unatembea kwa miguu, utaporwa kila kitu.
 
Hayo Maeneo uliyoyataja ni Hatari sana kwa Usalama wa Raia.
 
Back
Top Bottom