Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,497
Habari wakuu,
Nina mtoto wa ndugu yangu namsomesha Chuo Cha Utumishi wa Umma Dar (TPSC) kimezoeleka kwa jina la Magogoni..
Ni mara ya pili matokeo ya mtoto wa ndugu yangu yamebadilishwa..
Nimeona nilete huku maana wahusika hawataki kufanyia kazi.
Pia sio huyu mtoto wa ndugu yangu tu anasema hili ni tatizo kwa wanafunzi wengi na wahusika wa chuo wamekaa kimya.
Matokeo yakitoka yanakuwa yamewekwa katika mtandao wao wa aris TPSC.
Sasa cha kushangaza mtoto alileta matokeo yake ya kwanza kapata B 4 na C 1 akafurahi na mimi nikafurahi kafaulu.
Baada ya waliofeli kurudia mtihani na matokeo kuwekwa. Amekuta na yeye yamebadilishwa ana B3 na C2.
Kwenda kufuatilia anaambiwa ni kazi kurudisha yawe kama zamani.
Kama kuweka matokeo mtandaoni kumewashinda rudisheni ubaoni...
Sasa wakuu...kweli ni haki kubadili matokeo ya mwanafunzi?
Huu ni uonevu...na pia inavunja moyo wa mwanafunzi kusoma.
Naweka matokeo ya awali na yaliyobadilishwa..