Argentina: Maandamano yatanda kupinga ziara ya mwanamfalme wa Saudi Arabia

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Maandamano yafanyika Buenos Aires, Argentina kupinga mkutano wa G20 na Bin Salman
Raia wa Argentina wamefanya maandamano mjini Buenos Aires, mji mkuu wa nchi hiyo wakipinga kufanyika mkutano wa kundi la G20 utakaohudhuriwa na Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia.
Maelafu ya raia wa Argentina wamemiminika katika barabara za mji huo wakilalamikia kufanyika mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo Bin Salman, ambaye anakabiliwa na tuhuma mbalimbali za jinai. Waandamanaji waliokuwa na mabango yenye jumbe mbalimbali sambamba na kulaani pendekezo lililopelekea kuanzishwa kwa kundi la G20, wamezikosoa baadhi ya nchi wanachama katika kustafidi na vyanzo asilia vya nchi yao. Kadhalika waandamanaji wameonyesha upinzani wao kwa safari ya Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia nchini humo, huku wakipiga kambi mbele ya ubalozi wa nchi hiyo kutokana jinai zake yakiwemo mauaji dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.
Mkutano wa G20 unatarajiwa kuanza Ijumaa ya kesho tarehe 30 Novemba mjini Buenos Aires, Argentina, katika hali ambayo kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni, likiwemo tukio la mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari mkosoaji wa utawala wa Aal-Saud na pia ushiriki wa Bin Salman katika mkutano huo, ilitatarajiwa kwamba mkutano huo ungetumiwa kuishinikiza Riyadh na kuihoji kuhusiana na suala hilo. Jumla ya polisi elfu 22 wamewekwa tayari kwa ajili ya kudhamini usalama wa kikao hicho. Wakati huo huo duru za habari kutoka Argentina zimearifu kwamba, bin Salman ameelekea katika ubalozi wa nchi yake mjini Buenos Aires, badala ya kupumzika hotelini kama ilivyokuwa imepangwa. Kwa mujibu wa duru za karibu na mwanamfalme huyo wa Saudia, Mohammad Bin Salman ameelea ubalozini badala ya kwenda katika hoteli ya kifahari ya Four Seasons kutokana na kuhofia usalama wake baada ya kuripotiwa kwamba wananchi wa nchi hiyo walikuwa wamepanga kuizingira hoteli hiyo kwa maandamano. Hii ni katika hali ambayo polisi ya Argentina imezidisha ulinzi katika maeneo yaliyo kando na ubalozi wa Saudia kwa kufunga njia zinazoelekea ubalozi huo baada ya mwanamfalme huyo kuwasili eneo hilo.
 
Usichezee pesa
Watapiga kelele, tembo akipita wanakanyagwa tu
Dunia hii usife walahi
 
MM NI MUISLAM ILA SAUDIA NI GAIDI NAMBA 1 DUNIANI HAIJAALISHI WANA SEHEM TUKUFU, JAPO UKWELI UNAUMA LAKINI NDIO IVYO TENA
 
Back
Top Bottom