Mwanamfalme wa Saudia akataa kuonana na Netanyahu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,994
17,895
Mohammed bin Salman wa Saudia akataa kukutana na Netanyahu

Duru za kidiplomasia za kigeni zinasema kuwa hakuna maendeleo yoyote katika kuanzishwa uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia kati ya utawala haramu wa Israel na Saudi Arabia, kwani Mrithi wa Ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman (MBS) amekataa ombi la waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu la kukutana naye.

Inasemakana Netanyahu na bin Salman walizungumza kwa simu mara mbili katika wiki za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Press TV, chanzo hicho, kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kilisema, mtawala huyo wa Israel mwenye umri wa miaka 73 na Bin Salman, ambaye kimsingi anatajwa kuwa kiongozi asiye rasmi wa Saudi Arabia, walifanya mazungumzo kabla na baada ya mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliofanyika Ijumaa iliyopita katika mji wa bandari wa Bahari Nyekundu wa Jeddah.

Inadokezwa kuwa wawili hao pia hawakujadili uwezekano wa safari za ndege za moja kwa moja kutoka maeneo yanayokaliwa na Israel hadi Saudi Arabia kwa ajili ya Hija hadi mji mtakatifu wa Makkah mwaka huu.

Kulingana na tovuti ya habari ya N12, wakuu wa Saudia wameukabidhi utawala wa Kizayuni wa Israel orodha ya masharti ya makubaliano ambayo yanahusu kadhia ya Palestina. Ripoti hiyo imesema masharti hayo ni pamoja na kuruhusu vyombo vya usalama vya Palestina kuimarishwa ili wanajeshi wa Israel wasiwe na satwa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.


MBS pia iliomba udhibiti wa usalama wa Wapalestina kwenye eneo la Msikiti wa al-Aqsa na Kanisa la Holy Sepulcher katika Mji Mkongwe wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Wiki iliyopita, waziri wa mambo ya nje wa utawala bandia wa Israel Eli Cohen katika mahojiano nagazeti la Kizayuni The Jerusalem Post alidai kuwa kuanzisha uhusiano wa kawaida baina ya utawala wa Tel Aviv na Saudi Arabia "sio suala la kama, bali ni lini."

Alisema Mratibu wa Ikulu ya White House kwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Brett McGurk na Mratibu Maalum wa Rais wa Marekani kuhusu Miundombinu ya Kimataifa na Usalama wa Nishati Amos Hochstein wamezungumza na Mohammed bin Salman kuhusu kukaa na Israeli wakati wa ziara yao huko Jeddah mapema mwezi huu.
Adui mzayuni nduli mkuu waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu

4bvc65e78608f61pf47_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom