Arfi ashangaa wanaojadili urais CHADEMA

Arfi ashangaa wanaojadili urais CHADEMA

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2][/h]JUMAMOSI, JANUARI 26, 2013 09:41 NA KHAMIS MKOTYA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Said Arfi, amewashangaa baadhi ya viongozi wenzake ndani ya chama hicho wanaojadili suala la urais.

Arfi, ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, alisema huu siyo muda mwafaka wa kubishania hoja ya mgombea urais kwa sasa, kwa kuwa muda wa jambo hilo haujafika.

Amesema kwamba, kitendo cha kuendelea kufanya hivyo ni kutafuta migogoro isiyo ya lazima ndani ya chama hicho, badala ya kuanza kujipanga na kujijenga zaidi kwa wananchi.

Arfi alitoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza na MTANZANIA, alipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd, zilizopo Sinza, Kijiweni, jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, katika maelezo yake, mbunge huyo alisema Katiba ya CHADEMA ipo wazi kuhusu haki za wanachama wanaotaka kugombea nafasi yoyote.

“Katiba yetu ipo wazi, sisi kila mwanachama anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa, ndiyo kusema kuwa kila mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yoyote kwa sababu ni haki yake kama mwanachama.

“Sipo hapa kuzungumzia nani anayefaa, ninachosema ni kwamba, nafasi ya mgombea urais siyo hoja kwa sasa kwa sababu muda wake bado haujafika.

“Muda ukishafika, chama kina utaratibu wake wa namna ya kuwapata wagombea wa nafasi zote hadi hiyo ya urais, sioni haja kwa nini tushughulishwe na jambo hilo sasa,” alisema Arfi.

Wakati huo huo, Arfi alirejea kauli ambayo imekuwa ikitolewa na viongozi wenzake wa juu, kwamba Chadema itashinda urais wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Alisema kwamba, hali ya kisiasa ndani ya chama chake bado ni shwari na kwamba migogoro iliyopo inayohusisha Baraza la Vijana (BAVICHA), haiwezi kukiyumbisha chama.

“Chadema ni chama makini, tunajua wapi tulipotoka, wapi tunapoenda, baadhi ya watu wanaitabiria kifo Chadema, mimi nasema wanajisumbua, hao wanapoteza muda wao kutabiri vitu wasivyovijua.

“Chadema inazidi kuimarika kila kukicha, tutachukua dola katika uchaguzi wa mwaka 2015, watu hawa wanaoiombea mabaya Chadema hawataamini kitakachotokea,” alisema.

Alipoulizwa chama chake kitawezaje kuchukua dola wakati kimepata mafanikio kidogo kisiasa, ikiwamo kutopata wabunge na madiwani wengi, alisema:

“Wewe unajua Chadema tulikuwa na wabunge watano mwaka 2000, leo tunazungumzia wabunge 50 ndani ya Bunge.

“Lakini suala la idadi ya viti peke yake siyo kigezo, kuchukua dola ni suala la utayari wa Watanzania, tukijipanga vizuri na kwa kutumia utayari huu walionao wananchi, naamini hakuna wa kuzuia tusichukue dola,” alisema.

Hawa ndio watu wanaojitegemea kiakili wanajua wanatoka wapi walipo na wanapoelekea well done Hon @Arfi sio watu wakiwa kwenye media hutaka kujipandishia mi CV yakishamba tu big up Arfi .
 
Aache kujishaua, Huo ushauri angewapa kina Zitto,Mbowe na Mtei. Yeye kamaliza vikao akiwa nao hakuwapa huo ushauri lakini anakimbilia kwenye Media. Mjadala wa Urais Chadema umeshafungwa na Mwenyekiti keshamtangaza mgombea yeye ana ubavu gan wa Kupinga? Arudishe chenji alizopewa na Pinda asijifanye Mkavu! Eti watachukua nchi 2015 hizo ARV za kurefusha maisha ya Kisiasa akawanyweshe Wafipa wake wa katavi!
 
Ubarikiwa ARFI. Watu wenye mtazamo kama wewe. Muda huu CDM ifanye kazi ya ziada ya kuingia vijijini. Angalau kila kata kuwe na Ofisi. Then unakuwa na ccess na wapiga kura walio wengi maana kura almost zote ziko vijijini. HONGERA ARFI
 
Well said Mzee Arfi, ama hakika wewe ni hazina kwa chama
 
"hali ya kisiasa ndani ya chama chake bado ni shwari na kwamba migogoro iliyopo inayohusisha Baraza la Vijana (BAVICHA), haiwezi kukiyumbisha chama.

"Chadema ni chama makini,
tunajua wapi tulipotoka, wapi tunapoenda, baadhi ya watu wanaitabiria kifo Chadema, mimi nasema wanajisumbua, hao wanapoteza muda wao kutabiri vitu wasivyovijua."

Nimependa hiki kipengere ambacho ni Muhimu sana kwa chama chochote cha siasa. CCM walivyoambiwa hawana dira wala mwelekeo walitaharuki vibaya mno lakini uweli ndiyo huu tunaouona: RIP H. Kolimba, tunakukumbuka.
 
Aache kujishaua, Huo ushauri angewapa kina Zitto,Mbowe na Mtei. Yeye kamaliza vikao akiwa nao hakuwapa huo ushauri lakini anakimbilia kwenye Media. Mjadala wa Urais Chadema umeshafungwa na Mwenyekiti keshamtangaza mgombea yeye ana ubavu gan wa Kupinga? Arudishe chenji alizopewa na Pinda asijifanye Mkavu! Eti watachukua nchi 2015 hizo ARV za kurefusha maisha ya Kisiasa akawanyweshe Wafipa wake wa katavi!

masalia bado tunaendelea kuwachuja na kuwafukuza
 
Aache kujishaua, Huo ushauri angewapa kina Zitto,Mbowe na Mtei. Yeye kamaliza vikao akiwa nao hakuwapa huo ushauri lakini anakimbilia kwenye Media. Mjadala wa Urais Chadema umeshafungwa na Mwenyekiti keshamtangaza mgombea yeye ana ubavu gan wa Kupinga? Arudishe chenji alizopewa na Pinda asijifanye Mkavu! Eti watachukua nchi 2015 hizo ARV za kurefusha maisha ya Kisiasa akawanyweshe Wafipa wake wa katavi!

hapo kwenye nyekundu wafipa tumekukosea nini we panya buku mpaka ushindwe kujenga hoja bila kutaja kabila.....mijitu mingine bhana .....yani bila kutaja kabila au dini ya watu maisha hayaendi......jinga zima
 
Back
Top Bottom