Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,500
- 86,042
Ni mchana tulivu wa Jumapili hii, nimekumbuka mbali sana nikaamua tushee hii habari, kila nikiangalia vijana wa siku hizi wanaofanya miadi kwa simu naona kama vile wanamisi utamu fulani hivi, haina raha kuulizana kila saa umefika wapi "Dear" mbona hufiki? Mbona unakawia sana? aaah hii haina raha kabisa. Ona uzoefu wangu kipindi hicho....
Tumekutana Jumamosi hiii na inabidi tukutane jumapili ijayo, kwahio tunapata muda. Tutakutana kwene kona ileee chini ya ule mti jiarni na kale kamto pale bondeni saa nane na nusu, kwa hio baada ya hapo mnaachana kila mtu anaeda zake. Unasubiri wiki nzima then jumapili inafika, kuna jua kali kama la leo....unatafuta sababu ya kutoka home...unaipata. Taratiiibu unaanza kujongea sehemu ya tukio, ni saa nane na ROBO nakaribia eneo la tukio, hakuna kitu!! Najivuta mbele kidogo jua ni kali mara kwa mbaaali kidogo namuona binti anakuja ameshika kijifimbo anapiga piga majani!!! Ni saa nane kama dakika 31 hivi, tunasalimiana na kujuliana hali then tunaenda kukaa eneo letu la tukio. Ni saa kumi na moja na kidogo tunaamua kuagana na kurudi makwetu hadi jumamosi tena saa tisa maana "Baba Mkwe" to be atakuepo home bado.
Ni jumamosi imefika kwa shida sana ile ahadi imekua ikinitesa sana maana kila sekunde inakua kama lisaa, najivuta tena leo tunaenda kukutana chini ya jiwe fulani jirani kidogo na mto kuna mti wa Eucalyptus (sp), leo nachelewa kidogo kama dakika chache hivi ila namkuta mtoto ameshafika anacheza cheza na vijiti na matete, pana ka upepo kazuri kweeli. Huwezi amini tunakaa hapo hadi saa kumi na moja na nusu!!!!! Tunaagana kwa furaha na kurejea makwetu kila mtu karidhika sana, tunapotembea kila dakika tunageuka nyuma na kuagana tena, hadi tunakatisha kona na hapo hakuna anemuona mwenzie tena!!!!!
Tumeenda shule sasa, tuko mbali mbali ila tunawasiliana kwa barua hasa "Airform" sijui kama bado zipo, zilikua very cost-effective. Barua zimepambwa hadi raha, unaisoma, unaiweka chini ya mto, mmmhh unasoma shule ya Boys tupu, mwenzio yuko kwene Co-school. Ahhhhhh ni raha sana.
Tumerudi tena home, appointment zetu zinaendelea vizuri, nimeombwa nifike home maana baba hatakuepo! Najipiga moyo konde nimeambiwa nifike saa nane maana baada ya muda huo baba atakua ameshakula lunch na kupumzika kidogo na kuondoka kuelekea mjini. Nimefika tayari, nimejificha kwene vichaka, namsubiria Dingi atoke ili nitume mtu au nijipitishe pale nje anione!!! Inaenda kama ilivyopangwa, ni ahadi kamilifu sana hadi raha, anavyinisindikiza kuna kua na hali ya mvua, inabidi tujifiche chini ya msitu kwene miti ili mvua ipite, kumbe nimevaa koti la Jinzi la "kuchovya" (kwa wale wanaokumbuka-kuchovya). Ndani nimevaa Tisheti nyeupe, duh najikuta ile rangi yote imehamia kwene tisheti, mmmhh bado ni upendo tu.
Jamani nina mengi yanayodhihirisha kuwa appointment za enzi zile zilikua tamu sana, yaani unapomuona mpenzio hadi raha, mmmh nimemkumbushia leo ikiwa ni miaka kibao imepita tumeishia kucheka tu. Wewe je uzoefu wako ukoje? Kikubwa ni kwamba baada ya miaka yote hio ya appointment za tabu tulikuja kuoona, appointment za simu hazina ladha jamani!!!! Jumapili njema