Habari zenu wana jukwaa hili pendwa!
Ndugu zangu nina hamu ya kujua au kupata msaada toka kwenu kuhusu haya nimekuwa sina ufahamu nayo juu ya huduma fulanifulani zinazokuja na simu zetu hizi za kisasa (smartphones).
Kuna apps unapofungua tu akaunti ama ya google(android) au microsoft(wp) basi zinakuomba updates.
Nimejaribu kuangalia kuna baadhi tangu nimemnunua simu sizijui matumizi yake au zinafanyakazi kimfumo pasipo mimi kujua.
Msaada wangu kwenu ni kwamba kwa hizi ambazo sintazitumia nisipo zi-update nini madhara au faida ya simu yangu?
Applications ambazo mimi situmii kwenye simu yangu lakini mara kwa mara zinaomba updates;-
1. AllShare Cast Dongle S/W updates
2. Amazon Kindle
3. GROUP PLAY
4. Hangouts
5. HP Print Service Plugin
6. IMD Movies & TV
7. NFL mobile
8. Samsung Link
9. Samsung Print Service Plugin
10. Samsung Watch on (on TV)
11.Share Music for Group Play
12. TripAdvisor
13. Blurb Checkout
14. Samsung Push Service
Kwa uchache ni hizo naomba kuwasilisha!