Application ya kufundisha Kiswahili

Bongo Trust

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
252
241
Habari wana jamvi!

Nina wazo ninalotaka kujadili pamoja nanyi kama litakuwa na maana basi litendewe kazi, laah! kama sivyo basi tuachane nalo.

Kama nilivyo tambulisha maada katika kichwa cha Uzi huu, nimepata wazo la sisi wana JF pamoja na watu wa Forums nyingine ambao tumesomea taaluma ya ualimu, kuwa tushirikiane kwa umoja wetu tutengeneze APPLICATION YA SIMU maalumu kwa ajili ya kufundishia lugha ya kiswahili mtandaoni.

Nilikuwa napitia ripoti moja wiki iliyopita nikaona kuna sehemu imewandikwa kuwa kuna ongezeko kubwa sana la watu wanao hitaji kujifunza lugha hii ya Kiswahili katika nchi mbali mbali, ila ikaonekana kuwa kuna uhaba wa waalimu wa kufundisha lugha hio haswa katika nchi yetu ya Tz, (sijui walitumia vigezo vipi kusema jambo hilo), ila kwa binafsi yangu sijaliafiki hilo suala maana najua kuna walimu wengi tu wenye uwezo wa kufundisha kiswahili kwa ufasaha ila wapo mtaani tu na hawana ajira.

Turudi kwenye lengo letu

Nilipata wazo hili kwamba tutengeneze APPLICATION hii kisha kwa wingi wetu tuitangaze mtandaoni kila kona, mfano hata tukiwa watu mia kila mmoja akaitangaza kwenye magroup kumi katika mitandao ya kijamii mbali mbali basi itakuwa imefika umbali mkubwa mno.

Katika application hii tutaweka mfumo kama ule wa referral link ili kila mmoja atajavyo jitahidi ku promote application huko na huko kwa wale wataofikiwa na tangazo lake na wakatamani kujiunga katika darasa hili kama wanafunzi basi wanafunzi hao watakuwa wa muhisika aliye kutana nao, hivyo juhudi yako ya ku promote app ndio juhudi yako ya kupata wanafunzi.

Nadhani, hii mtu angeweza kuifanya pale anapokuwa na muda wa kutulia hatakama ana kazi nyingine basi pale akitulia anafanya hii kazi ilimradi anawapa wanafunzi wake taarifa kuwa tutakua na kipindi mda fulani.

Nadhani nchi nyingi zinatumia lugha ya kiingereza, hivyo ni vizuri huyu Mwalimu atakaye taka kufanya hii kazi awe na ABC'S kuhusu lugha ya kiingereza, na kwa wale wenzetu walio jaaliwa kujua lugha nyinginezo za nchi nyingine tofauti na kiingereza basi wanaweza kuwa na advantage ya kupata wanafunzi wa nchi hizo cha msingi ni kuweka maelezo husika kwenye profile na tangazo lako.

Ni wazo tu jamani mnaweza kunikosoa au kuliboresha kwa kadiri kila mmoja atakavyo ona ni sahihi.

Ahsante kwa kusoma
 
Back
Top Bottom