Apple iPhone X goes on sale today.

Mfano hyo face unlock naona samsung Wapo vizuri zaidi kwenye iris scanner hata kwenye giza totoro unaweza itumia
 
Mfano hyo face unlock naona samsung Wapo vizuri zaidi kwenye iris scanner hata kwenye giza totoro unaweza itumia
iris sio face unlock, inatumia jicho tu. halafu zinatumia infrared hivyo giza sio tatizo,
 
Ndo maana naona ipo more advanced kuliko face au wewe unaonaje mkuu?
zote zina faida na hasara zake mkuu, inategemea na preference yako. ila kwa ulinzi tu nafkiri bado password ni more secure hasa hizi za ku combine herufi kubwa, ndogo, charachter na namba.
 
Mauzo ya iPhone 8/8+ ni kidogo kwa sababu wengi walikuwa wanasubiria iPhone X
 
Hiyo ni rare cases kutokea na wawe identical kweli wamefanana otherwise haikubari na siyo tatizo sana twin wangu akifungua simu yangu as long as mtu mwingine hawezi.
By the way hata wao walitoa probability ya watu waliofanana kufungua 1 in a milion

na identical twin inafungukaa....kuna dada youtube alikua anafanya majaribio
 
Mkuu huu mjadala ulipaswa kunijibu tu ni simu ipi ya Microsoft iliyokuwa na face id? that's all au ni lumia 1020 au lumia Fulani au nokia Fulani,mambo ya xbox 360 na tablet hayapo kwenye mjadala wetu.
Umechepuka mkuu.
Sihitaji nani wa kwanza kuja na face id ila nahitaji kufahamu simu gani ya Microsoft yenye face id huo mwaka 2015 that's all mkuu.
Nahitaji kufahamu simu toka Microsoft iliyokuja na face id na Microsoft kuitambulisha ina face id sio kunisimulia hadithi.
Kama haikuako sema hamna kama ipo nambie ni model gani?
Natumaini utanijibu haikuwako nasubiria jibu.
 
Wabongo bana.....Simu pia ni kompyuta kama ilivyo kwa calculator !!!!
Simu sio computer mkuu,Simu kazi yake ni tofauti na computer japo simu za sasa zinakuja na feauture za computer.
Huwezi sema ile simu ya mezani ni computer lakini mabadiliko ya teknolojia yanafanya simu kuwekewa feauture za computer ila still simu ni simu na pc ni pc.
Basi sema na simu ni calendar,simu ni calculator,simu ni camera.
Huwezi sema simu ni camera wakati camera zipo,sema tu imewekewa camera lakini sio camera.
Nadhani tumeelewana acha kukariri maneno ya kusikia simu ilivumbuliwa kwa muda wake na computer kwa muda wake.
Simu kazi yake ni moja tu kusafirisha na kupokea mawimbi ya sauti hivyo vingine vyoote ni vya ziada ni mbwe mbwe tu.
 
Microsoft waache biashara ya simu na tablet wataleta mpaka simu inapiga deki lakini believe me hawatofika popote waendelee tu kutengeneza OS.
Mwenzao Samsung kakubali tayari soko la laptop limemshinda maana ulaya hakuna tena laptops za Samsung.
cause soko ni bovu watu ni vaio na apple.
Ila nashangaa wamekazana tu.
Wala sidhani hata hio tablet kama italeta impact yeyote kwa maana naona wamekomaa sana hata ile lumia 950 yenye windows hello kwani ilifika wapi?
Waendelee kututengenezea windows os.


Microsoft wajipange sana.
 
waache Tablet? unajua sasa hivi surface ni billion dollar business? mapato yake yanakuwa kila mwaka.

kaangalie soko la tablet kila mwaka mauzo ya android tablets na ipad yanashuka, tablet pekee ambazo mauzo yanaongezeka ni za windows.

kama wewe ni CEO unge discontinue kitu kinachoingiza matrilioni ya hela?

update
halafu mkuu sijui unafikiria nini, sijajua hayo magraph ya simu ulioeka na mauzo ya surface yanaingiliana vipi

halafu serious kabisa umemtaja vaio mauzo ya laptop? kampuni ambayo imeshauzwa na sony sasa hivi haina hata issue.

Na apple vile vile sio muuzaji mkubwa wa laptop hio ni title ya lenovo, wao ndo wauzaji wa kubwa wakifuatiwa kwa karibu na HP.

na lumia 950 usiilinganishe na kifaa chochote cha surface, hivi vifaa vya surface vinarun full windows na sio os za simu na pia vina innovation kubwa sana na vikitolewa vina define market, mfano angalia hizi products

-surface tablet vs ipad, mpaka apple akawa forced kutoa ipad pro yenye keyboard na kalamu (kuiga surface) sababu surface innovation wise zilizifanya ipad kama toy.

-surface studio vs Mac,
hizi mac zilikuwa tu ni All in one PC ila microsoft akadefine soko kabisa na surface studio, kuanzia display, ile hinge, surface dial, unavyoweza kuieka position tofauti, kalamu, kuchora na mambo kibao.

na kama Hio surface phone itatoka tegemea tena surface kudefine soko, na wengine waanze ku copy kama kawaida yao.
 
hakuna, so point yako ni nini?

kesho mtu akichukua kifuu cha nazi akaeka ios mule ndani atakuwa hajacopy technology ya mtu sio?
 
mkuu simu ni computer lakini sio PC, kuna utofauti wa pc na computer.

kilugha PC ni personal computer, hata kifaa cha android ni pc, ila kimazoea na kijina pc ni kifaa cha windows na unapotaka kutofautisha computer inayorun windows na osx moja utaiita pc na nyengine utaiita Mac

kama calculator ni computer kwanini simu isiwe computer?

computer ni kifaa tu kinachoreceive data then kinakuwa na programs zinazo process na kukupa information au output. ukiingiza 1+1 ikakupa 2 tayari ni computer hio.
 
hakuna, so point yako ni nini?

kesho mtu akichukua kifuu cha nazi akaeka ios mule ndani atakuwa hajacopy technology ya mtu sio?
Aisee nimetumia microsoft surface pro3 ni hatari tupu mkuu.
Iko faster smooth ina pen unaweza kuchora unaweza igeuza kama laptop hapo hapo tablet.
Ya jamaa yangu anaitumia kwenye kutengeneza graphics aliinunua zanzibar kama 3.8 milion
 
Aisee nimetumia microsoft surface pro3 ni hatari tupu mkuu.
Iko faster smooth ina pen unaweza kuchora unaweza igeuza kama laptop hapo hapo tablet.
Ya jamaa yangu anaitumia kwenye kutengeneza graphics aliinunua zanzibar kama 3.8 milion
Tatizo la surface ni bei tu mkuu, ila ni best Tablet kwenye soko. na jamaa ambaye yupo behind hivi vifaa panos panay huwa habahatishi kila kitu anachodesign kinahit. hata wozniak wakati anaiona surface alisema steve job amekuwa reincarnated
http://iphone.appleinsider.com/arti...teve_jobs_came_back_reincarnated_at_microsoft
 
Huyo panay formerly alikuwa wapi chief.
Naona kwenye surface pro na kwenye surface station wamezingatia design kitu ambazo steve jobs alikuwaga anamponda microsoft hasa gates alidai hana essence ya style and design
 
Iris scanner ni ujinga mbele ya face ID , kumbuka face id ndani yake kuna iris scanner yan lazima mtu awe amefumbua macho ... Tusitake kumumunya maneno ukweli ni kwamba iris scanner bado sana kuanzia uwepesi mpaka features ilizonazo, kazi ambazo unaweza kuzifanya ni kwamba face Id imewaacha mbali sana ...

Ku unlcok kwa iris scanner inakulazimu simu yako ikae vizuri yan face to face na ione macho direct, inakubidi uinyanyue na kuionyesha macho au macho yako yakae direct kwenye cm kitu ambacho ni fault na ni usumbufu na hapo hapo isiwe mbali , haina depth scanning kwa hiyo kui trick ni rahisi ndo maana haitumiki ku authorise payments kwa kifupi ni kwamba haiaminiki , ipo kwa ajiri ya unlock tu na showcase basi ndo maana wameiwekea fingerprint maana wanajua itamboa mtumiaji kwa maana ya masharti yake.

Face Id inafanya kazi angle yoyote, ili mradi tu ione uso wako na uwe hujasinzia , iko more secure ndo maana inatumika ku authorise payment , ina scan uso mzima so hata uwe umekunja uso na simu imekaa pembeni kidogo bado itajua ni wewe tu, kumbuka iphone zina raise to wake , so ukinyanua simu yako tayari inaona ni wewe inatoa lock , simple fast ans convinient , ina depth scanning inaifanya iweze kutambua kati ya midoli na watu, camera zake zinatumika kwenye function mbali mbali kama snapchat , animoji n.k !

Tukisema apple hawafanyi vitu ilimradi tu muwe mnatuelewa , wao wanaweka kitu kinachofanya kazi siyo show.

Tuwape samsung miaka miwili ijayo ndo wataweza kutengeneza kitu kama face ID. Kumbuka project ya Face Id imeanza years back
 
mkuu sababu samsung ame implement vibaya technology haimaanishi ni mbaya, iris ina advantage yake over face id,

mfano hao evil twin au hio 1 of million ambayo Apple wameisema kwenye iris haipo, sababu macho ya binadamu hayafanani even jicho lako la kulia na kushoto hayafanani.

na pia face id haina iris kama iris scanner, face id ni tech nyengine na iris ni nyengine. ingekuwa face id ina iris kama iris scanner ingetofautisha evil twin.

isome windows hello utaona hizo biometric zote.
 

Mkuu naona unazunguka , najua umezi review hizi mbili sasa nipe msimamo wako FACE ID vs Iris Scanner. Kiujumla which is better ?
 
nimepitia ifixit walipoifungua iphone x, na kama kawaida yao wale jamaa hawaachi kitu, true depth camera ya face id imetengenezwa na primesense kampuni ya israeli ambayo Apple aliinunua 2013.

kwa wasiofahamu Microsoft alishirikiana na hawa jamaa kutengeneza kinect ya kwanza kabisa. baadae Microsoft akaendelea kutengeneza zinazofuatia mwenyewe.

so nipo sahihi true depth ya Apple ni Kinect like technology ambayo imekuwa inspired na microsoft ukipenda wamecopy, hivyo usiwape sana credit ya Apple kudevelop hio tech.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…