Apoteza maisha wakati akiogelea

Apoteza maisha wakati akiogelea

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607

Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Mwaka wa Tatu aitwaye Samwel James Chacha (25) amekufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Tukio hilo lilitokea Machi 7, mwaka huu na jitihada za kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo
zilifanyika. Mwili wa marehemu ulipatikana Machi 11 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya imeeleza chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kusubiri uchunguzi wa kitabibu.
 
Uzembe sio? Nadhani hata kupigwa na radi ni uzembe wa kutembea kwenye mvua bila tahadhari au sio?
Kuogelea mtoni ni hatari.Mto huwa na sehemu zile ambazo maji huwa yanazunguka Kama kiduara duara ulifika hapo unasimamishwa halafu unavutwa chini maji unaenda swekwa kwenye shimo ndani kabisa chini ambako huwezi ogelea hata ufanyaje. Utafia huko ndani maiti itaelea baadaye. Kuogelea mto watu huogelea sehemu chache Sana za mto.
 
Mimi ninaona lugha iliyotumika ipo sawa tu kama imethibitika marehemu alifanya uzembe.Tubadilikeni watanzania,penye ukweli tuuseme, itatusaidia kuepuka mengi.Ndiyo hivihivi hata mtu akiuawa kwa sababu ya ujambazi ,bado tunajidai kumpamba tu mazishini.Mi naona mniseme tu ili mliobaki mpate fundisho.
 
Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Mwaka wa Tatu aitwaye Samwel James Chacha (25) amekufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Tukio hilo lilitokea Machi 7, mwaka huu na jitihada za kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo
zilifanyika. Mwili wa marehemu ulipatikana Machi 11 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya imeeleza chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe – Makandana kusubiri uchunguzi wa kitabibu.

Mbona ule mto ni hatari sana, yasemekana una mikondo mingi mno underground (kijungu) na isitoshe ni mto wenye kasi sana
 
Kuogelea mtoni ni hatari.Mto huwa na sehemu zile ambazo maji huwa yanazunguka Kama kiduara duara ulifika hapo unasimamishwa halafu unavutwa chini maji unaenda swekwa kwenye shimo ndani kabisa chini ambako huwezi ogelea hata ufanyaje. Utafia huko ndani maiti itaelea baadaye. Kuogelea mto watu huogelea sehemu chache Sana za mto.

Umenikumbusha kijungu ina mithili ya handaki limesogea mpaka chini ya ardhi waliyojenga makazi wenyeji
 
Back
Top Bottom