Apigwa risasi akijaribu kuwatoroka polisi

Apigwa risasi akijaribu kuwatoroka polisi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,426
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mguuni na polisi wakati akijaribu kuwatoroka.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ni kati ya watano waliokamatwa kwa tuhuma za kuvamia maduka makubwa na kupora mali jijini Dar es Salaam.

Sirro alisema tukio hilo lilitokea Septemba 14 eneo la Ununio wakati mtuhumiwa akiwapeleka polisi kuwaonyesha ilipokuwa imefichwa silaha kwenye majaruba ya chumvi.

Alisema mtuhumiwa alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.

Awali, alisema watuhumiwa hao, akiwamo mwanamke, walikamatwa katika eneo la Goba na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na matukio hayo.
 
Risasi ya mguu inauwa?tens mtuhumiwa akiwa chin ya ulinzi na uangaliz was jeshi LA polis?well done polis wetu
 
Aisee huyo jambazi ana mbio sana, alitaka kushindana mbio na risasi
 
Hivi inawezekanaje mnaenda na mtuhumiwa jambazi kwenye eneo hatarishi akiwa hana pingu mkononi au miguuni na kila mwezi tukio la namna hiyo limekua linajitokeza na matokeo yanafanana.

Je ni kweli wote wanakua wanajaribu kutoroka?
 
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mguuni na polisi wakati akijaribu kuwatoroka.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ni kati ya watano waliokamatwa kwa tuhuma za kuvamia maduka makubwa na kupora mali jijini Dar es Salaam.

Sirro alisema tukio hilo lilitokea Septemba 14 eneo la Ununio wakati mtuhumiwa akiwapeleka polisi kuwaonyesha ilipokuwa imefichwa silaha kwenye majaruba ya chumvi.

Alisema mtuhumiwa alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.

Awali, alisema watuhumiwa hao, akiwamo mwanamke, walikamatwa katika eneo la Goba na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na matukio hayo.

Ya Bageni na msitu wa Pande yasijejirudia
 
Hivi inawezekanaje mnaenda na mtuhumiwa jambazi kwenye eneo hatarishi akiwa hana pingu mkononi au miguuni na kila mwezi tukio la namna hiyo limekua linajitokeza na matokeo yanafanana.

Je ni kweli wote wanakua wanajaribu kutoroka?

Kuna maswali mengi zaidi ya majibu. Ya Bageni na msitu wa Pande wa hukumu ya jana Zombe
 
nina mashaka sana na polisi. wamekua kama genge la wauwaji tu, mtuhumiwa mmoja mwenye pingu anawatoroka vipi? bahati mbaya marehemu hana kauli, ukisha kufa watakusemea chochote wanachotaka, utaitwa jina lolote wanalo amua, jambazi, gaidi n.k... na hakuna hata mtu mmoja atakae hoji taarifa ya polisi. ukifa na haki zako zote zimekufa...
 
Kila anayeitwa jambazi na kuuwawa akiwa katika mikono ya Polisi na tukaunda Tume ya jaji Kipenka tunaweza kusikia mengi ya ajabu sana.
Ingefaa pia mtu anapofia mikononi mwa polisi uchunguzi wa tuhuma zake kuwa ni jambazi uendelee kwa kutumia chombo kingine nje ya polisi kudhibitisha kuwa ni jambazi. Kuna uwezekano wa hata visasi vikawa vinatumika kupotezana kwa jina hilo la ujambazi. Haki ya kuishi inatoka kwa Mungu tusiingilie na kuleta balaa kwa taifa
 
Hivi inawezekanaje mnaenda na mtuhumiwa jambazi kwenye eneo hatarishi akiwa hana pingu mkononi au miguuni na kila mwezi tukio la namna hiyo limekua linajitokeza na matokeo yanafanana.

Je ni kweli wote wanakua wanajaribu kutoroka?
ndio over.
 
Muda unakuja kila mtu atahukumiwa kwa mujibu alivyotekeleza wajibu wake kikazi...inaweza tokea ndugu wa watuhumiwa waka jiorganize na kufungua kesi ambayo mwisho wa siku itafunua mambo yote chini ya kapeti.. kimsingi naunga mkono juhudi zote zinazofanywa na polisi katika kudhibiti ujambazi ingawa suala la kuuawa kwa watuhumiwa wa ujambazi mimi siliungi mkono kamwe.
 
Huu Mchezo wa kufa kwa kudaiwa kutoroka naona umekomaa sasa.
Maana kwenye kuonyesha silaha lazima mtu atakuwa na Pingu,na hawezi kuwa na kasi ya kukimbia,maana kuna kuwa na Askari maalum wenye uwezo wa kukimbia wakati wa ku asses watu wa kwenda nae.
Hali hii inazua maswali mengi saana,juu yamtandao wa Majambazi kuonekana kuwa nguvu sana
 
Bado Watz. tuna safari ndefu sana ya kuondokana na ujinga uliopitiliza na huenda ikachukua hata Millenium.
Kwani mawazo yawchangiaji wengi mnaoonyesha mawazo ya mwendo kasi na General Conclusion hata pasipo kufikiria uhalisia wa Tukio au jambo.
Kwa mfano TU mwenye akili TIMAMU NA TIMILFU KAMA SIYO UTAHIRA AU ULEMAVU WA AKILI unaaminije jambo usililijua na inawezekanaje JAMBAZI kutoroka chini ya ulinzi wa Polisi ilikhali amefungwa Pingu???????
Ninyi Watz. wenye mawazo ya mwendo kasi na kutoa hukumu harakaharak pasipo kufuata sheria,kanuni na taratibu zake mnapaswa kuchangaya na AKILI zenu na siyo za kuambiwa TU.
Binafsi siungi MKONO suala la ujambazi na siungi MKONO suala la KUUA tena mikononi mwa polisi na siyo hata kwenye mapambano ya majibizano.
Watz. tunapswa kuhoji masuala mengine kulingana na ni wazi shahiri kuwa mnajua POLISI WETU walivyo.....mfano suala la Mbagala na Kule Pwani bado kwangu ni kiini macho hadi leo.
Hebu tuache kuhukumina na hasa hukumu ya kifo pasipo kufuata sheria,kanuni na taratibu zake vinginevyo hakuna haja ya kuwa na mahakama na tusidanganyane hapa labda tu kwa wale wenzetu wenye ulemavu wa akili ndiyo wanao weza kudanganyika na siyo werevu.
 
Mkuu iko hivi hata ukiwa umefungwa pingu wakati umewachukua askari na kuwapeleka maeneo ambayo ni maficho ya silaha ikatokea unakimbia kiukweli hakuna atakaekukimbiza kwan kuna mambo ya kujiuliza 1:ni kwa nin ukimbie mazingira ambayo ndiyo inaaminika ni maficho ya silaha tafsiri yake ninin, huenda ikawa mazingira yale unayafaham vizur kuwa wenzio ndiko watakuwepo hivyo ukishaanza kukimbia inamaana wao watakuwa standby kuangalia nani anamkimbiza na nirahisi wao kiwashambulia ninyi na hata kuwaua kizembe zaidi kijeshi hairuhusiwi maana mnaweza kupoteza maisha kwa kumkimbiza mhalifu mmoja je mnataka yatokee ili mje mseme polisi ni wazembe kupitiliza kwa kumfukuza mhalifu kisha wakauwawa???hapana inabidi mjiulize walikamatwa wangapi kanin yeye tu???hawa wahalifu wana mbinu nyingi sana hususan wanapofika mazingira ambayo wanaamin wenzao watakuwepo. achen wenye professional yao wafanye yao.
 
Risac ya mguu inaua kweli or ilikuwa ya sumu
Haya ndio yale yale
 
Back
Top Bottom