Aoa mwanafunzi, amkeketa usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aoa mwanafunzi, amkeketa usiku

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kilimasera, Dec 28, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Kijiji cha Borenga katika Kata ya Kisaka wilayani Serengeti, Nyaraya Chacha (65), amemkeketa kwa siri usiku Esta Ouru (13) aliyemuoa hivi karibuni kwa madai kuwa asingeweza kushiriki naye tendo la ndoa bila ya kumkeketa, licha ya jamii kuipinga kwa nguvu mila hiyo.

  Ouru aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Itirio wilayani Tarime, alishindwa kuendelea na masomo mwaka 2004 akiwa darasa la nne kutokana na familia yake kukosa uwezo wa kifedha.

  Alikeketwa usiku wa Novemba 11, mwaka huu katika Kijiji cha Borenga nyumbani kwa mumewe Chacha, meta 200 kutoka katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Borenga.

  Akizungumza na gazeti hili jana nyumbani kwake katika Kitongoji cha Byasuma, Esta alisema
  aliolewa na Nyaraya aliyemtorosha na kisha kutoa mahari ya ng’ombe wanne, na usiku huo aliokeketwa, alikamatwa na mumewe kwa kushirikiana na mkewe mwingine, Bhoke Chacha (40) pamoja na ngariba wa kike.

  “Siku hiyo mume wangu akiwa ameongozana na mkewe huyo, aliniita katika nyumba yake na kunikamata kwa nguvu, kunifunga kamba na kunikeketa kwa nguvu kwa kutumia nyembe, na baada ya kunikeketa, alinifungia ndani kwa wiki mbili.

  Baada ya kupata nafuu aliniamuru nikachunge ng’ombe,” alisema Esta.

  Alisema baada ya kutoka kulisha mifugo, siku ya pili yake alitoroka kwenda kwa baba yake mzazi, Ouru Bara (49) aliyemjulisha alikuwa amekeketwa, jambo lililosababisha mzazi huyo ambaye ni Mluo, kwenda kumuuliza mkwewe kulikoni amkekete mwanawe na kabila la Waluo, halina desturi hiyo kwa wanawake.

  “Nilitoroka saa sita mchana kwa siri kwenda kumwambia baba juu ya kukeketwa kwangu, lakini siku hiyo hiyo alinirudisha kwangu akisema kuwa alichokuwa anakitaka amekwishakifahamu na kuwa hana shida na mimi tena,” alisema binti huyo na kueleza nia ya kurudi kwa mumewe ilikuwa ni kuchukua nguo zake, lakini zote zilichomwa moto na kuambulia kupewa sketi moja na blauzi moja tu.

  Esta alisema mumewe huyo alikuja nyumbani kwao kudai mahari na ndipo baba yake mzazi alipeleka shauri hilo katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Byasuma, Maro Bochoke (41) ambaye alithibitisha mtuhumiwa huyo kukabidhiwa ng’ombe watatu wa mahari na kubaki ng’ombe mmoja.

  Mzee Bara alisema amesikitishwa na kitendo cha kinyama kilichofanywa na mtuhumiwa huyo
  aliyedai alimtorosha bintiye kwa nguvu bila ya ridhaa yake kama mzazi na kwamba baada ya kukosa uwezo wa kifedha na vitisho alivyokuwa akipewa na mtuhumiwa huyo alishindwa kupeleka shauri hilo Polisi.

  “Baada ya yeye kumkeketa, kwa nini aliamua kumrudisha nyumbani maana alisema kuwa jinsi alivyokuwa kabla hajakeketwa asingeweza kufurahia tendo la ndoa.

  Ni kwa nini tena aliamua kumrudisha nyumbani kwangu, wakati ni kama alimbaka maana alimtorosha mwanangu kwa kumrubuni na umri wake ni mdogo sana,” alisema na kuongeza:

  “Cha ajabu baada ya kuchukua mahari, alinijibu kuwa mwanangu bado ni mdogo hana kovu na kuwa ataolewa, sasa kama alikuwa anafahamu kuwa mwanangu bado ni mdogo, kwa nini aliamua kumkeketa tena kwa siri bila ya kutushirikisha sisi wazazi wake,” alisema Bara ambaye aliachana na mkewe mwaka 2004 na binti yake huyo kwa sasa ni kama ndiye mama anayewapikia wadogo zake wawili na kaka yao mkubwa.

  Esta aliiomba serikali imsaidie apate msaada wa kisheria kutokana na kukeketwa na mume huyo na kumharibia usichana wake, huku akidai hakuwa tayari kuingia katika ndoa kwa sababu ya umri mdogo.

  Naye Chacha alikana kumkeketa binti huyo ingawa alikiri alikuwa ni mkewe na kuwa aliamua kumrudisha kwa wazazi wake baada ya kubaini kuwa ana matatizo ya akili, hoja iliyopingwa na mzazi wa binti huyo.

  “Nakwambia huyu binti alikuwa anakuja kwangu hapa mara kwa mara kununua chakula, na
  nikamuuliza kuwa nimuoe akanikubalia na nikaamua kumchukua na nikapeleka mahari kwao ng’ombe wanne na nikaishi naye kwa muda mfupi, lakini sijawahi kumkeketa, na ningewezaje kumkeketa wakati niko umbali mchache kutoka katika Kituo cha Polisi,” alidai Mzee Chacha.

  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Byasuma, Maro Bochoke, alikiri mzee huyo kurudishiwa mahari na kueleza kusikitishwa kwake na kitendo cha kinyama alichofanyiwa binti huyo; na kwamba alimshauri baba yake kuchukua hatua za kisheria, lakini akadai hana uwezo ikiwemo nauli ya kwenda mahakamani kwa kuwa mahakama iko mbali kutoka katika kijiji hicho na hawezi kufungua kesi.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  65 kwa 13
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  hiyo noma sana.

  Lkn pia kushindwa kusma shule ya msingi eti kwa madai ya kukosa ada nao ni upuuzi. Hivi ada ya shule ya msingi bei gani?
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  hiyo sio sababu ya kuacha shule hata kidogo. Shule yenyewe shule ya awali/ya msingi?
   
 5. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2013
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ajabu ni pale kanapokuambia ingiza yote dear wakati wewe tayari umeishajikunja mpaka mwisho..! Hapo mimi ndo huna nachoka kabisa
   
 6. C

  COPPER JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2013
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 1,670
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Muoaji, muolewaji na mkwe, wote wamechangia katika kilichotokea.
   
 7. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,782
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Baadhi ya watani zangu Wakurya wanaishi enzi za kijima na kishamba sana!
   
Loading...