Anza mradi wa kuku kwa TZS 300,000 tu

Mchanganuo mzuri ila umesahau kwamba kuku wa kienyeji wakishataga mayai 10 au 12 hutaka kuhatamia (kulalia) hapo hawatagi hata ukiwanyang'anya mayai wanachukua muda kuanza kutaga tena hivyo si rahisi kupata hayo mayai ya kila siku
 
Ndugu Kuku wa kienyeji hutaga mayai mpaka 30 Ushahidi Ninao maana ninafuga, kuku usimuachie mayai mengi ayaone kila akitaga ww Ondoa muekee moja Au mawili tu maana ukimuachia mayai mengi ndipo huacha kutaga na kuamua kuatamia.
 
Daa nimependa sana huu Uzi kiukweli pesa tunazo wenyewe kuliko kusubiria hizi ajira ambazo hazieleweki..
 
Asante sana kiongozi mpenda maendeleo ya wote. Mkuu unajua tatizo kubwa ni miundombinu ya kuwafugia hao kuku. Ni rahisi sana kufikiria huo mtaji utatosha, lakini kiuhalisia 300k haitoshi.Unapofikiria kuanzisha mradi wa namna hii lazima kufikiria pia banda la kuhifadhi hao kuku ambapo ghalama la banda hilo ni zaidi ya mtaji wa kununua hao kuku na mlo wao. Je kiongozi una maoni gani kuhusu hili?
 
Ndugu Kuku wa kienyeji hutaga mayai mpaka 30 Ushahidi Ninao maana ninafuga, kuku usimuachie mayai mengi ayaone kila akitaga ww Ondoa muekee moja Au mawili tu maana ukimuachia mayai mengi ndipo huacha kutaga na kuamua kuatamia.
Pengine hao ni kuku chotara lakini kienyeji pure hawana uwezo huo pitia machapisho mbalimbali utaona wote tunatoa haya mayai lakini hawazidi 12
 
Nakushukuru kwa mchanganuo. Kwa vile nina banda, fedha na mfanyakazi ninataka kujaribu mrdi huu.
 
Mashaka yangu ni hapo kwenye uwezo wa kuku wa kienyeji kutaga mayai kwa asilimia 80 kwa siku. Kwa uzoefu wangu labda uwalishe chakula cha layers ndio waweza fikia hapo.
 
mimi pia nadhani hapa nahitaji maelezo
 
Ghafla najiona mfugaji point saNa mkubwa

Lkn kuna ndugu ya alijaribu kufuga haimae ziliishia kufaa tu wakat matibabu kila Kitu zilipata !!!!
 
Pengine hao ni kuku chotara lakini kienyeji pure hawana uwezo huo pitia machapisho mbalimbali utaona wote tunatoa haya mayai lakini hawazidi 12
Usiamini kila kilichoandikwa mkuu mm nina kuku wa kienyeji pure na wanataga mpaka mayai 30 Nimekupa Njia ya kufanya.
 
Ufugaji wa whatsapp.....hakuna biashara yenye hasara kwenye calculator..

Mchanganuo ni mzuri, ila matokeo ni chini 40% ya kile kilichotegemewa..

Kwa usimamizi wa aslimia ngapi? wapo watakaokushangaza kwa matokeo ya 90%-98%
 
Nimependa
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…