ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Habari marafiki zangu
Siku ya leo nimeona niwaambie kitu ambacho ni muhimu sana kwenu au kwetu sote, jambo ambalo muda mrefu lilikuwa linanitatiza ndani ya moyo wangu nak usema ni lini nitalisema hapa.
Watu wengi hudhani kuwa kesho ipo tu na wala hawajisumbui kwa siku ya kesho kwani huona inakuja tu, wengine hawana mwelekeo katika mstakabali wa maisha yao wao ni bora liende wakiamka na kulala ni hivyohivyo tu, hawana mawazo mpya ya nini wafanye kwa siku hiyo walionayo. Marafiki zangu jambo lolote haliji hivihivi tu mpaka uwe umejituma, umejithatiti, umejiona kuwa waweza kulitenda hilo wazo lako, na waswalhili wanasema mambo mazuri hayaji hivihivi tu yaani wewe ukinge mikono kupokea bila hata kujishughulisha au kuchakalika upate.
Hebu jaribu kufanya kile ambacho umekiwaza kukifanya, Kama unataka kuwa na maisha mazuri yenye furaha ndani yake kwanini leo usithubutu kufanyakile ambacho unaweza fanya au tenda kwanini ushindwe kuthubutu kutenda ulichokusudia katika maisha yako, unasubiri nini? unangoja nini? unadhani kuwa muda unakusubiri wewe? kwanini usiamue kufanya maamuzi yenye busara na kufanya pale wakati muda ungalipo? Au unadhani muda unakusubiri hasa kwa wewe kijana rafiki yangu?
Usidhani muda unakusubiri wewe, kama hautathubutu kufanya yale uliyojiwekea basi ujue uko hatarini kuporomoka na kuwa na stress nyingi pindi utakapokuwa mzee. Anza sasa uchalewa rafiki tuna nusu mwaka ya 2013 fanya maamuzi yenye busara sasa. huku ukimtanguliza Mungu kwa kila jambo ufanyalo, kwani yeye hujishughulisha na maisha yetu.
Hebu thubutu achana na dhana ya kushindwa, AMUA KUTHUBUTU KUTENDA JAMBO JIPYA jisemee moyoni ya kwamba UNAYAWEZA MAMBO YOTE KWA YEYE AKUTIAE NGUVU
soma warumi 3:14. Nawatakia kila la kheri na mafanikio tele pale utakapoamua na kuthubutu