Inawezekana tunaishi katika siku za mwisho kabisa za uhai wetu, ila masikini hatuna habari. Kama corona ikifumuka Africa kama ilivyofumuka China, Italy nk, kufikia tarehe kama ya leo mwakani unaweza kukuta hakuna mtu yuko hai bara zima hili.Je, umeanza kufikiria jinsi ya kujikinga na virusi vya korona? Basi anza sasa;
- kisha fikiria unavyopokea na kutunza fedha;
- kisha fikiria Daladala za mbagala;
- kisha fikiria mwendokasi;
- kisha fikiria mabasi ya mikoani;
- kisha fikiria msikitini siku za ijumaa
- kisha fikiria kanisani siku za jumamosi na jumapili;
- kisha fikiria kwenye masoko yetu;
- kisha fikiria kwenye vibanda umiza
- kisha fikiria kwenye mashule yetu ya serikali;
- kisha fikiria tamaduni zetu watanzania
- kisha fikiria umakini wa wasimamizi wetu;
Mdomo wangu unajizuia lakini Nausikia Moyo wangu ukiniambia R.I.P
- fikiria umakini wa marekani lakini umeshindwa kuzuia korona;
- fikiria teknolojia ya China lakin imeshindwa kuzuia Korona;
- Fikiria nguvu ya Italy lakin nao wameshindwa kuzuia Korona.
KILA MTU KWA IMANI YAKE AMUOMBE MUNGU KWA JINSI ANAVYOAMINI ILI NCHI YETU HII ISIGUSWE NA GONJWA HILI.
Amina.
daah! kweli wewe usher-smith!
Wacha tufe tu mkuu maisha yenyewe hayaeleweki... .Inawezekana tunaishi katika siku za mwisho kabisa za uhai wetu, ila masikini hatuna habari. Kama corona ikifumuka Africa kama ilivyofumuka China, Italy nk, kufikia tarehe kama ya leo mwakani unaweza kukuta hakuna mtu yuko hai bara zima hili.
Kuna wimbo nausikiliza hapa nawaza jinsi roho itakavyotengana na mwili wangu..Mimi mwenzenu I honestly believe huu ugonjwa utakuja tu na huku kwetu its just a matter of time...
Wacha tufe tu mkuu maisha yenyewe hayaeleweki... .
Kuna wimbo nausikiliza hapa nawaza jinsi roho itakavyotengana na mwili wangu..
I wish uwe ni usingizi mzito tu na kwenda kuoza moja kwa moja, isiwe kuna maisha mengine baada ya kifo.. Japo kuna wapendwa wangu waliotangulia huko, natamani niwaone tena maana nimewamisi sana.LOL hilo ni fumbo tumefumbiwa wanadamu...
MlokaNilikuwa nahofu kipindi kile cha ebola, nipo zangu kigoma, naambiwa iko hapo upande wa pili kongo kwa ndugu zetu!
Ebwana mungu siyo mudi ebola ikatuliza mzuka nikiwa poa kabisa.
Leo hii korona inawapa watu joto la jiwe, nikijiangalia sehemu nilipo, kuipata ni shetani menyewe aamue. Niko mbuga ya Selous.