Anus miserabilis: Kipindi cha njaa, maafa, mateso na mwambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anus miserabilis: Kipindi cha njaa, maafa, mateso na mwambo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Jul 20, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Katika lugha ya kilatini kuna msemo wenye maana ya mwaka(kipindi) wa njaa, mwambo, maafa na mateso. Neno hilo ni ANUS MISERABILIS. Kwa hapa Tanzania msemo huu unaakisi kipindi cha mwaka 2010-2015. Kwa maoni yangu kipindi hiki kitakuwa kigumu vibaya kwa watu wengi sana ukiondoa wateule wachache.

  Kwa nini nimesema hivyo, ninaelezea!!!
  Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa katika utawala wowote ambao unapatikana kwa njia za uchaguzi, kuna vipindi vitatu vya msingi. Kipindi cha kwanza cha utawala huo hutumika katika kuweka malengo ya utekelezaji(setting goals), kipindi cha pili hutumika katika kutekeleza malengo hayo kwa ufanisi(implementing the goals) na kipindi cha tatu huwa ni kwa ajili ya kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine(Preparing the future). Kwa kesi ya huko nyumbani Tanzania nilitegemea iwe hivi: Mara baada ya JK kushinda uchaguzi miezi 6 ya kwanza(Nov-April) ingekuwa ni kuweka malengo ya utekelezaji. July-Dec 2014 kingetumika kama kipindi cha utekelezaji wa malengo kwa ukamilifu na Jan-(may-Oct) 2015 kiwe ni kwa ajili ya kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu na kuingia ktk uchaguzi mkuu. Waswahili wanasema, nyumba ni msingi. Ukijenga msingi vibaya nyumba itatetereka na haita dumu.

  Tuangalie CCM na mustakabari wa nchi yetu
  Katika kipindi hiki cha mwisho cha utawala wa JK hkika nchi yetu itakwenda kwa kusuasua. Kada zote za wananchi zitaumia. Wawe wasomi, wakulima, watumishi wa umma wa ngazi za chini na kati na hata wafanyabiashara wadogo na wa kati lazima waumie. Ninasema hivi kwa kuwa CCM ambacho aidha tunataka ama hatutaki ndio chama tawala na ndicho chenye mustakabali wa nchi yetu kwa sasa.Badala ya kupanga agenda za maendeleo katika kipindi hiki cha kwanza, wao ndio kwanza wanajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa CCM mwaka 2012. Viongozi wote wa CCM mawazo yao ni kupanga safu kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2012 ambao utatoa taswira ya nani kugombea urais kupitia CCM mwaka 2015. Baada ya uchaguzi mkuu wa CCM mwaka 2012, macho ya wanaCCM yatakuwa jinsi ya kujipanga kuipeperusha bendera ya kijani katika uchaguzi mkuu wa 2015. Kwasura hiyo niambie, maendeleo yatatoka wapi!!! Nani atamuwazia mwananchi wa kawaida huko vijijini na mijini!!! Tuangalie mfano huu: Mikutano inayoendeshwa na Nape na wenzake"mkutano wa Mbeya hivi majuzi" lengo lake lilikuwa ni nini! Je, si madaraka ya 2015? Kujiuzulu kwa Rostam Aziz, si kwa kuwa kuna msuguano wa nani awe rais ajae?
  Mwenye kufahamu anieleze! Lini tutaanza kutekeleza mipango yetu ya maendeleo? Na tutatekeleza mipango ipi, maana mpaka sasa hakuna tulichopanga.

  Angalia swala hili! Wakati nchi ipo gizani, Rais wa nchi yupo ziarani Afrika kusini eti pamoja na mambo mengine amekenda kuvutia wawekezaji. Huu ni usanii, unamuita vipi mwekezaji wakati huna nishati, unamvutia kwa maneno yapi!

  HII NI ANUS MISERABILIS

  I STAND TO BE CORRECTED
   
 2. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Mnataka kutuvurugia chama chama chetu nyie. Udom, barabara za lami zote huzioni? N a mchakato wa katiba mpya je?

  UPOFUUUUUU
   
Loading...