Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Aliyekuwa Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa endapo atapata ridhaa ya chama, atakuwa tayari kuwania nafasi hiyo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu leo hii katika ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Mavunde amesema amejitokeza kugombea jimbo hilo kwa nia ya kuendeleza maendeleo na kuwatumikia wananchi wa Mtumba kwa moyo wa uwajibikaji na uadilifu.
“Leo nimechukua fomu kuomba kuteuliwa na chama changu kugombea Jimbo la Mtumba. Hili ni ombi langu kwa chama, na kama nitapata ridhaa ya kuteuliwa, basi nitakuwa tayari kulitumikia jimbo hili kwa moyo wote,” alisema Mavunde mbele ya wanahabari
Mavunde, ambaye kwa miaka kadhaa aliwahi kuhudumu kama Mbunge wa Dodoma Mjini na kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, amesema ana uzoefu wa kutosha katika masuala ya maendeleo ya wananchi na amejifunza mengi kuhusu changamoto za wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini.
Kwa mujibu wa ratiba ya CCM, mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu unaendelea kwa nafasi zote za uongozi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Wanachama mbalimbali wameendelea kujitokeza kuwania nafasi hizo kwa mujibu wa taratibu na kanuni za chama hicho.
Chanzo: Michuzi Tv