Antony Diallo anena kuhusu yanayoendelea nchini

Kwa lugha ya jumla jumla ulioyotumia humu huku ikikujumuisha na wewe napata shida kukuelewa una mlenga nani. Watanzania ni watu makini na ndio maana tunaye JPM pale juu. Tulitaka mtu wa aina hii na kamwe sio dhambi kuwa na mitizamo tofauti.

Madhara ya Bashite au Makonda kwa utendaji na usimamizi wa kauli za Raisi ni makubwa. Bashiitee au Makonda anamtesa Raisi, ana mui-embarass. Haaminiki na hana sifa za kuwa Kiongozi katika ofisi za umma.

Jambo moja tunaloweza kujifunza kutoka kwa Makonda aka Bashite ni ujasiri na uthubutu. He is exceptional and brilliant. Ni kichwa cha aina yake.

Hivyo, Makonda ambaye pia ni mtanzania anaongezea sifa watanzania kuwa ni watu majasiri. Makonda ni mwakilishi mzuri katika hili. Haogopi kufanya kile anachokiamini bila hata kupima madhara yake. Yeye ni results oriented, which actually is good attitude.

Acha kutukana watanzania, mheshimiwa mstaafu. Utavuliwa uheshimiwa hapa jamvini.
Rudiii darasani kaka
 
Wewe Diallo hutakiwi kusema umejifunza hiki na kile, kwa kauli nzito kama hizo, bila kutoa sababu zilizokupeleka katika conclusion hiyo ili ziweze kuangaliwa na watu waone kama umejifunza kitu cha kweli au umeingia choo cha kike.

Kuanzia hapo tu unaonekana hujaweza kuwa makini.

Huko kwingine assumptions nyingi, facts hakuna.

Tupe facts, ukishindwa unajivua heshima na kuwa mbwatukaji kama wengine wengi tu tunaowajua.

Fact ni kwamba Makonda hajakanusha tuhuma dhidi yake.

Fact ni kwamba Makonda hajaonyesha vyeti vyake.

Hizi ni facts. Hujaweza kuzipangua.

Kama unataka twende kwa speculation, ukiziita "Hypothesis", na mimi naweza kusema wewe unajiona umetupwa nje ya uongozi, umesikia Msukuma mwenzako (Magufuli) anapendelea Wasukuma, na umeone umteteee kwa kujitoa akili na kuleta hekaya za Alfu Lela Ulela wakati kamatuhuma dhidi ya Makonda zingekuwa za uongo, kuzikanusha ilikuwa kazi rahisi tu.

Unatafuta kiki Magufuli akukumbuke katika ufalme wake na uwe relevant katika midomo ya Tanzania.

Hiyo nayo ni "Hypothesis" kama yako kama unataka kuleta habari zako hizo.

Ukiandika kwa mbwembwe nukuu ya Albert Einstein kwamba "Akili iliyotumika kutengeneza tatizo haiwezi kutumikakutatua tatizo hilo" unatafsiriwa kama unasema akili ya chama tawala iliyotutengenezea tatizo la madawa ya kulevya haiwezi kutatua tatizo lamadawa ya kulevya".

Wewe ndiye mtu unayewasagia Watanzania kwa maneno ya jumla jumla?

Wewe mwenyewe una akili?

Ungekuwa na akili ungeweza kutumia nukuu hiyo hali ukijua context ya CCM kuwa ndicho chama kilichotufikisha hapa na ndicho chama kinachojinadi kutatua matatizo yetu yaliyoletwa na uongozi mbovu wa chama hiki?

They say a little knowledge is dangerous indeed, yours is a case of little knowledge and high confidence, even deadlier.
 
"Kuanzia Sakata la kutaja Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya mpaka kinachodaiwa "Uvamizi wa kituo cha Clouds Media Gruoup"! RC Paul Makonda amekuwa gumzo kuu hapa Nchini kwa sasa ,kuanzia kwenye vyombo vya habari,mitaani na kwingineko!

Nikiwa hapa Kijijini kwangu Mwanduhitinje nimekuwa nikilifuatilia suala hili kwa taratibu sana bila mihemuko ili nijifunze kitu kipya na kwa kweli nimejifunza sana!

Kabla sijasema mafunzo niliyopata kutokana na "Sakata" hili niwaeleze kuwa nimesikiliza Clips zote za "Askofu" Gwajima kuhusu RC Paul Makonda,Nimesoma magezeti yote yaliyo na yanayoandika habari kuhusu RC Paul Makonda,Nimefuatilia post zote za Mange Kimambi kuhusu RC Paul Makonda,nimefuatilia comments za Watu mbalimbali kuanzia RC Paul Makonda akichipukia UVCCM akitokea TAHLISO kama Rais wake na hata alipom-blast Lowassa kuwa hana sifa za kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, na sasa naeleza mafunzo niliyopata na hasa baada ya kusoma Gazeti la JAMUHURI kwa kile walichokiita Uchunguzi uliofanywa na WAANDISHI WETU!

FUNZO LA KWANZA: Tanzania ni miongoni mwa Nchi Duniani zenye uhaba wa Waandishi wa habari na Wasomi (Ninaposema wasomi simaanishi wale wenye "A" zote na Makofia mengi lakini wameishia kufuga kuku na Nguruwe kule CHANGANYIKENI).

FUNZO LA PILI: Watanzania wengi ni watu wasio na agenda yoyote ya maana ya ku-accomplish katika maisha yao bali ni watu waliokata tamaa na wanaotumia MATUKIO kama "pain killers" ya kuwapunguzia maumivu kutokana na KUSHINDWA kwao.Ndio maana Watanzania wengi hushabikia sana habari zinazomdhalilisha mtu au kumshusha chini mtu aliyeko juu kama RC Paul Makonda.

FUNZO LA TATU: Watanzania hatuna wanasiasa wenye maono,wanasiasa wetu wengi ni waganga njaa tu ambao wamefanya siasa kama kichaka tu kujifichia na kutafuta riziki kwa ajili ya maisha yao na siyo maendeleo ya wapiga kura na Taifa kwa ujumla!

FUNZO LA NNE: Tanzania hakuna UPINZANI,na itachukua miongo mingi sana Nchi hii kuweza kuongozwa na Chama cha Upinzani.Hawana Ajenda na ni watu wa MIHEMUKO! Ajenda zao ni kama hizi WEMA SEPETU KUPOKELEWA CHADEMA,TUNDU LISSU KUWA RAIS WA TLS, RC PAUL MAKONDA KAVAMIA KITUO CHA CLOUDS MEDIA GROUP.

FUNZO LA TANO: Wapinzani wa Tanzania HAWAJITAMBUI na WALA HAWAJUI WANAMTUMIKIA NANI! Hawana Rafiki wa kudumu wala Adui wa Kudumu! LOWASSA FISADI,LEO LOWASSA JEMBE! NAPE VUVUZELA leo NAPE JEMBE kwa kuwa "amekurupuka" kutoa tamko la kulaani Kabla ya Taarifa ya uchunguzi wa kamati yake aliyounda kumfikia mezani!

Baada ya kusoma hayo MAFUNZO niliyopata kuhusu "SAKATA" la RC PAUL MAKONDA embu njoo sasa nikupitishe kwenye hizi "hypothesis" zangu kabla hamja-conclude jambo lolote.

Observation moja muhimu kwanza ni hii hapa: Watanzania wengi, Wanasiasa,Wasomi na Wananchi wa kawaida wanafananishwa na mnyama mmoja mwenye umbo kubwa sana sawa na Uwanja wa mpira wa miguu lakini ni mnyama mwenye kichwa kidogo mithili ya bakuli ndogo ya kulia supu! Uwezo wa mnyama huyu kufikiri ni mdogo sana na kuhisi chochote ni mpaka umguse kichwani.( Their brains are very small to entertain two big events at once ! they must drop one event to entertain the other !) ! Ndio maana Nchi hii ni ya MATUKIO hili likija litafunika hili na hakuna impact yoyote na hata hili la RC Paul Makonda litapita muda si mrefu kama unabisha subiri Bunge lianze April! RC Paul Makonda wewe vumilia tu bado KITAMBO KIDOGO WATASAHAU TU!

HYPOTHESIS YA KWANZA:

Nimesoma kwa utulivu sana Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI kuhusu Paul Makonda,Mtu aliyesemwa na akina "Askofu" Gwajima kuwa Paul Christian Makonda anatumia vyeti vyake Ndugu Paul Pierre Christian amekanusha vizuri sana na pia hana dada aitwaye Christina aliyetajwa na akina "Askofu" Gwajima. Hakuna dhambi yoyote jina lako kufanana na la mwingine, Juma Ali wako wangapi Zanzibar? Mohamedi Ali wako wangapi Duniani?!

Sheria inaruhusu kubadili jina na RC Paul Christian Makonda na kama ni kweli alikula kiapo mahakamani kubadili jina basi alijua jina alilokuwa akitaka kutumia la PAUL CHRISTIAN MAKONDA si lake la awali! Kwa nini basi aliende mahakamani?

HYPOTHESIS YA PILI:

Je PAUL CHRISTIAN MAKONDA hawezi kuwa ni mtu makini mwenye "SPECIAL MISSION" kutoka "KITENGO" fulani anayo-accomplish ?!

"Qualities "anazoonyesha RC PAUL MAKONDA zinazoweza ku-support hii hypothesis ni hii ya kupoteza "initial identity yake",pili angalia comments za Mzee Khamesse na familia yake ni watu ambao wamekuwa "disappointed" na tabia za RC PAUL MAKONDA, Nawanukuu kwa mujibu wa JAMHURI, " alikuja hapa kama mara mbili saa saba usiku na saa tano usiku,hakuingia ndani! Hapokei simu na namba anazowapa ni feki muda wote hazipatikani!

Kwa utamuduni wa kiafrika kwa watu waliokulea na tena kwa MUSUKUMA kama PAUL MAKONDA na pia kwa umaarufu na hesima aliyonayo Mzee Suleiman Khamesse lazima kuna KITU HAPA si Bure!!!!!

HYPOTHESIS YA TATU:

Katika vita hii ya Madawa ya kulevya tunajua RC PAUL MAKONDA amefanya jambo ambalo hata Marehemu Amina Chifupa alitaka kujaribu lakini hakulifikia. Kilichompata Amina Chifupa sote tunajua. Hivyo hawa WAUZA UNGA NA WATEGEMEZI WAO HAWAWEZI KUMFURAHIA RC PAUL MAKONDA LAZIMA WAJARIBU KUMWANGAMIZA TU! Na hapa Mheshimiwa Rais DR. JMP kama unaujua ukweli kuhusu kijana huyu basi please MLINDE KWA GHARAMA YOYOTE!
Ndio maana unapoona NAPE NNAUYE anatukuzwa kuwa ni jembe japo ukweli ni kuwa "AMEKURUPUKA" sana na kutozingatia ile dhana ya "collective responsibilty". WENGI WANAPIGANA VITA YA WAUZA UNGA DHIDI YA RC PAUL MAKONDA BILA WAO KUJUA au KWA KUJUA na Nape Nnauye AKIWEMO!

HYPOTHESIS YA NNE:

Kuhusu RC PAUL MAKONDA kuvamia kituo cha CLOUDS pamoja na kupewa Magari na Watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya kulevya yaani kampuni za TANGA PETROLEUM LIMITED NA NAS HAULAGE LIMITED. Hapa nikiri wazi kuwa najenga hoja yangu kufuatia maarifa niyopata kutokana na kusoma vitabu vifuatavyo: Kitabu cha The Book of Five Rings cha Mjapani Miyamoto Musashi, Kitabu cha 48 Rules of Power na Kitabu cha Lucifer Principles cha Howard Bloom.

Ukiangalia kwa hao marafiki zake kwa pamoja RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA amejaribu sana kujenga nao urafiki wa karibu mno! Je hii HAIWEZI kuwa ni strategy ya "kum-nail" adui ?! Je CLOUDS media Group hawatajwitajwi katika hii biashara HARAMU ya Madawa ya Kulevya?! Chunguza na fuatilia kifo cha Msanii Albert Mangwea kama MKONO wa CLOUDS MEDIA GROUP hautajwitajwi.

RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA anaweza kuwa ni mtu "HATARI" kuliko anavyochukuliwa ,kubezwa na kudhalilishwa na WATU WENYE UPEO MDOGO kama yule Mnyama niliyemwelezea hapo juu!

Yawezekana RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA akawa sawa na mtu anayetupia kuku wake mahindi pale tu anapotaka kumkamata ili amchinje! ZITTO KABWE anasema ameambiwa kuwa kile kikosi alichotumia RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA "kuvamia" CLOUDS kilikuwa maalum ambacho idhini yake hutolewa na Rais au Boss TISS. Je,tunajuaje kama RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA alitumia style ile ya YUDA ISKARIOTE aliyotumia kumtambulisha YESU Christo kwa wale maadui waliofika bustanini kumkamata? Labda RC PAUL MAKONDA "alinusa" kuwa CLOUDS MEDIA GROUP depot yao ya "UNGA" wameihamishia Studio na hivyo akaona aende na kikosi maalum incase ameukuta huo "UNGA" upo awakombe na incase ameukosa awapotezee tu kuwa yeye ni mtu wao na anafuatilia "Kipindi chake".

Kwanini isiwezekane hivyo kama ni huyu PAUL CHRISTIAN MAKONDA ambaye alituhumiwa kumfunga Ridhiwani Kikwete kamba za viatu na bado akaja kumuorodhesha katika orodha ya watu 97 anaowatuhumu kufanya Biashara ya dawa za kulevya!

Amemtaja Ridhiwani Kikwete na Yusufu Manji kuhusika na biashara ya Madawa ya kulevya kitu ambacho MWIGULNCHEMBA hawezi kufanya hata kama angekuwa na ushahidi mkononi!
Tungekuwa na Waandishi makini wangechunguza RC Paul Makonda anapokuwa nje ya Nchi anaongea na akina nani MISSIONS zake ni zipi lakini kwa hawa wetu ambao wakiamka wanakimbia kuangalia leo Mange Kimambi ame -post nini au Jumapili hii "Askofu" Gwajima atamchanaje Paul Makonda!

Hivi ukiwa hujapewa Vyeti uangalie na ukaambiwa uwasikilize wakijenga hoja SAED KUBENEA, BONIPHACE JACOB (MAYOR WA UBUNGO) na RC PAUL MAKONDA nani utasema ana ZIRO! obviousily ni KUBENEA na BONIPHACE JACOB! Je,ZIRO ya Paul Makonda haiwezi kuwa ni ya kutengeneza kwa "SPECIAL MISSION".?!

Albert Einstein alipata kusema kuwa akili iliyotumika kutengeneza tatizo haiwezi kutumika kutatua tatizo hilo.NDUGU WATANZANIA TUTAMBUE KUWA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA NI NGUMU KULIKO TUNAVYOFIKIRIA na kama unabisha kamuulize JAKAYA MRISHO KIKWETE au WILLIAM LUKUVI.

Unayepiga kelele bila kuruhusu kichwa chako kufanya kazi piga tu kelele LAKINI TAMBUA KUWA yawezekana unapiga kelele bila kujua kuwa wewe ni sawa tu na MBUZIaliyeko kwenye banda la mpika supu!"
Antony Diallo kama wewe ndiye umetoa makala hiyo..unazidi kuniaminisha kuwa nilifanya la maana kukupuuza.

Tunajua kundi lako ndani ya chama chako, unahitaji uitetee serikali uzidi kulinda ugali wako.

Bahati mbaya ni kuwa wakati wewe bado uko ktk giza totoro linalotokana na uwezo mdogo wa kuchambua mambo, wengi wetu tulishatoka huko na tumefunguka sasa.

Nimeona unaongelea Hypothesis..ukweli huujui!

Kazi ninayokupa ni moja...kafuatilie Bashite alifuata nn Clouds usiku ule pale, akupe majibu uje useme hapa.

Pili, muulize elimu yake na vyeti vyake vilipo.

Bila hayo mawili utakuwa unapoteza muda kama wenzio wengi.

Halafu hivi yale madeni ya TRA ulimaliza?
 
Ni mpuuzi tu anayeweza kumtetea bashite.

Huyu anataka tax relief hana lolote. Alipe mishahara wafanyakazi wake aache ujinga
Huyu mzee kashaiuza Sahara media group baada ya sizonje kumdai kodi.
 
DIALO AMEWATUKANA watanzania anaowategemea waangalie Star TV yake ili apate kula yake. Yeye ndiye HAJITAMBUI yuko ICU kifikra. Biashara zake zinawategemea hao hao anao watukana "Hana akili"

Mkiwmbiwa ukweli mnasema mmetukanwa
 
".....................

FUNZO LA KWANZA: Tanzania ni miongoni mwa Nchi Duniani zenye uhaba wa Waandishi wa habari na Wasomi (Ninaposema wasomi simaanishi wale wenye "A" zote na Makofia mengi lakini wameishia kufuga kuku na Nguruwe kule CHANGANYIKENI).

FUNZO LA PILI: Watanzania wengi ni watu wasio na agenda yoyote ya maana ya ku-accomplish katika maisha yao bali ni watu waliokata tamaa na wanaotumia MATUKIO kama "pain killers" ya kuwapunguzia maumivu kutokana na KUSHINDWA kwao.Ndio maana Watanzania wengi hushabikia sana habari zinazomdhalilisha mtu au kumshusha chini mtu aliyeko juu kama RC Paul Makonda.

FUNZO LA NNE: Tanzania hakuna UPINZANI,na itachukua miongo mingi sana Nchi hii kuweza kuongozwa na Chama cha Upinzani.Hawana Ajenda na ni watu wa MIHEMUKO! ...........

FUNZO LA TANO: Wapinzani wa Tanzania HAWAJITAMBUI na WALA HAWAJUI WANAMTUMIKIA NANI!

HYPOTHESIS YA PILI:

Je PAUL CHRISTIAN MAKONDA hawezi kuwa ni mtu makini mwenye "SPECIAL MISSION" kutoka "KITENGO" fulani anayo-accomplish ?!

"Qualities "anazoonyesha RC PAUL MAKONDA zinazoweza ku-support hii hypothesis ni hii ya kupoteza "initial identity yake",pili angalia comments za Mzee Khamesse na familia yake ni watu ambao wamekuwa "disappointed" na tabia za RC PAUL MAKONDA, Nawanukuu kwa mujibu wa JAMHURI, " alikuja hapa kama mara mbili saa saba usiku na saa tano usiku,hakuingia ndani! Hapokei simu na namba anazowapa ni feki muda wote hazipatikani!

Kwa utamuduni wa kiafrika kwa watu waliokulea na tena kwa MUSUKUMA kama PAUL MAKONDA na pia kwa umaarufu na hesima aliyonayo Mzee Suleiman Khamesse lazima kuna KITU HAPA si Bure!!!!!

HYPOTHESIS YA NNE:

Ukiangalia kwa hao marafiki zake kwa pamoja RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA amejaribu sana kujenga nao urafiki wa karibu mno! Je hii HAIWEZI kuwa ni strategy ya "kum-nail" adui ?! Je CLOUDS media Group hawatajwitajwi katika hii biashara HARAMU ya Madawa ya Kulevya?! Chunguza na fuatilia kifo cha Msanii Albert Mangwea kama MKONO wa CLOUDS MEDIA GROUP hautajwitajwi.

RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA anaweza kuwa ni mtu "HATARI" kuliko anavyochukuliwa ,kubezwa na kudhalilishwa na WATU WENYE UPEO MDOGO kama yule Mnyama niliyemwelezea hapo juu!

Yawezekana RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA akawa sawa na mtu anayetupia kuku wake mahindi pale tu anapotaka kumkamata ili amchinje! ................... Labda RC PAUL MAKONDA "alinusa" kuwa CLOUDS MEDIA GROUP depot yao ya "UNGA" wameihamishia Studio na hivyo akaona aende na kikosi maalum incase ameukuta huo "UNGA" upo awakombe na incase ameukosa awapotezee tu kuwa yeye ni mtu wao na anafuatilia "Kipindi chake".

Hivi ukiwa hujapewa Vyeti uangalie na ukaambiwa uwasikilize wakijenga hoja SAED KUBENEA, BONIPHACE JACOB (MAYOR WA UBUNGO) na RC PAUL MAKONDA nani utasema ana ZIRO! obviousily ni KUBENEA na BONIPHACE JACOB! Je,ZIRO ya Paul Makonda haiwezi kuwa ni ya kutengeneza kwa "SPECIAL MISSION".?!

Unayepiga kelele bila kuruhusu kichwa chako kufanya kazi piga tu kelele LAKINI TAMBUA KUWA yawezekana unapiga kelele bila kujua kuwa wewe ni sawa tu na MBUZIaliyeko kwenye banda la mpika supu!"

Kama hii imeandikwa na Dialo kweli basi huyu mzee kuna kitu kalishwa, si bure hawezi kuandika utumbo huu.
 
Hii mada ilishaletwa humu JF tukaijadili kwa kirefu, kiufupi ni kwamba haina mashiko.

Mwana Usalama gani awe kwenye mission kisha asijue kuwa Cloud kuna CCTV camera, this is nonsense

Kwani ukiambiwa alikuwa anakwepabkamera?
 
Kama aliambiwa mapema asifanye mkutano for a good reason, kwa nini alitaka kwenda kinyume chake? - Mawaziri wangapi waliondolewa madarakani siku za nyuma, ni Waziri gani aliwahi kuitisha media na kujaribu kuonyesha kama vile kaonewa au nini sijui!! Mbona Mawaziri wengine waliwahi kupitia zahma hizo lakini walikaa kimya. Watanzania we don't need 2 discuss a clash of TITANS - tuzungumzie masuala ya maendeleo basi - yaliyo pita yemepita tugange yajayo.

Huo uwezo wa kuzungumzia maendeleo ndio hakuna. Kila kukicha ni majungu tu humu. Panakera
 
DIALO AMEWATUKANA watanzania anaowategemea waangalie Star TV yake ili apate kula yake. Yeye ndiye HAJITAMBUI yuko ICU kifikra. Biashara zake zinawategemea hao hao anao watukana "Hana akili"
Huyu naye elimu yake inatia shake, hata jina lake pia. Ni walewale.
 
Mtasema mengi kuhusu Diallo. Hata hivyo sina hakika Kama ni yeye Kweli. Aliyeandika bila kujali ni nani, amechambua mambo ambayo yanahitaji IQ ya mtu iwe above average kumwelewa. Watu wachache ndo wataelewa. Labda hajafanya vizuri kutaja majina ya watu wengine Kama Mwigulu na wengine lakini uchambuzi wake umetulia
 
Unataka vyeti we kama nani?
Kwani anayestahili kuuliza vyeti ni nani?

Unaelewa kwamba wananchi ni waajiri wa watumishi wa umma? Unaelewa kwamba mishahara ya watumishi wa umma inatokakwenye kodi ya wananchi?

Ushawahi kusikia mtu anamuuliza Said Bakhressa vyeti?
 
Duh akili ni nywele jamani, mwenzetu hana kabisa, apunguziwe ata za kwapani apewe tu, zitamsadia......
Watu wengine mnachekesha sana . . [emoji23] [emoji23] [emoji23] Lakini ni ujumbe murua kabisa . . [emoji106]
 
Diallo is a successful business man he knows what's talking about, badala ya kumsikiliza na kutafakari alicho eleza wewe unatumia lugha za vijiweni kumbeza mtu ambaye ana umri kuliko hata wa Baba yako, sina hakika kama uliwahi kusoma hata kitabu kimoja alicho quote humu, jitahidi kutafuta walao kimoja kisome sina shaka kuna kitu utajifunza. Oh, one more thing - remember this man knows: Our Country, Ruling Party, one and all past and current Administration members. As I said, Dk.Diallo knows the above mentioned item/group like back of his hand - don't you forget that. Jifunzeni ku-analyse mambo kiundani zaidi kuliko ku-resort kwenye mihemuko, vile vile Watanzania tujifunze kuchukulia comments za ma WISE MEN seriously - ushauri tu.
Wale waleeeee . . !
 
"Kuanzia Sakata la kutaja Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya mpaka kinachodaiwa "Uvamizi wa kituo cha Clouds Media Gruoup"! RC Paul Makonda amekuwa gumzo kuu hapa Nchini kwa sasa ,kuanzia kwenye vyombo vya habari,mitaani na kwingineko!

Nikiwa hapa Kijijini kwangu Mwanduhitinje nimekuwa nikilifuatilia suala hili kwa taratibu sana bila mihemuko ili nijifunze kitu kipya na kwa kweli nimejifunza sana!

Kabla sijasema mafunzo niliyopata kutokana na "Sakata" hili niwaeleze kuwa nimesikiliza Clips zote za "Askofu" Gwajima kuhusu RC Paul Makonda,Nimesoma magezeti yote yaliyo na yanayoandika habari kuhusu RC Paul Makonda,Nimefuatilia post zote za Mange Kimambi kuhusu RC Paul Makonda,nimefuatilia comments za Watu mbalimbali kuanzia RC Paul Makonda akichipukia UVCCM akitokea TAHLISO kama Rais wake na hata alipom-blast Lowassa kuwa hana sifa za kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, na sasa naeleza mafunzo niliyopata na hasa baada ya kusoma Gazeti la JAMUHURI kwa kile walichokiita Uchunguzi uliofanywa na WAANDISHI WETU!

FUNZO LA KWANZA: Tanzania ni miongoni mwa Nchi Duniani zenye uhaba wa Waandishi wa habari na Wasomi (Ninaposema wasomi simaanishi wale wenye "A" zote na Makofia mengi lakini wameishia kufuga kuku na Nguruwe kule CHANGANYIKENI).

FUNZO LA PILI: Watanzania wengi ni watu wasio na agenda yoyote ya maana ya ku-accomplish katika maisha yao bali ni watu waliokata tamaa na wanaotumia MATUKIO kama "pain killers" ya kuwapunguzia maumivu kutokana na KUSHINDWA kwao.Ndio maana Watanzania wengi hushabikia sana habari zinazomdhalilisha mtu au kumshusha chini mtu aliyeko juu kama RC Paul Makonda.

FUNZO LA TATU: Watanzania hatuna wanasiasa wenye maono,wanasiasa wetu wengi ni waganga njaa tu ambao wamefanya siasa kama kichaka tu kujifichia na kutafuta riziki kwa ajili ya maisha yao na siyo maendeleo ya wapiga kura na Taifa kwa ujumla!

FUNZO LA NNE: Tanzania hakuna UPINZANI,na itachukua miongo mingi sana Nchi hii kuweza kuongozwa na Chama cha Upinzani.Hawana Ajenda na ni watu wa MIHEMUKO! Ajenda zao ni kama hizi WEMA SEPETU KUPOKELEWA CHADEMA,TUNDU LISSU KUWA RAIS WA TLS, RC PAUL MAKONDA KAVAMIA KITUO CHA CLOUDS MEDIA GROUP.

FUNZO LA TANO: Wapinzani wa Tanzania HAWAJITAMBUI na WALA HAWAJUI WANAMTUMIKIA NANI! Hawana Rafiki wa kudumu wala Adui wa Kudumu! LOWASSA FISADI,LEO LOWASSA JEMBE! NAPE VUVUZELA leo NAPE JEMBE kwa kuwa "amekurupuka" kutoa tamko la kulaani Kabla ya Taarifa ya uchunguzi wa kamati yake aliyounda kumfikia mezani!

Baada ya kusoma hayo MAFUNZO niliyopata kuhusu "SAKATA" la RC PAUL MAKONDA embu njoo sasa nikupitishe kwenye hizi "hypothesis" zangu kabla hamja-conclude jambo lolote.

Observation moja muhimu kwanza ni hii hapa: Watanzania wengi, Wanasiasa,Wasomi na Wananchi wa kawaida wanafananishwa na mnyama mmoja mwenye umbo kubwa sana sawa na Uwanja wa mpira wa miguu lakini ni mnyama mwenye kichwa kidogo mithili ya bakuli ndogo ya kulia supu! Uwezo wa mnyama huyu kufikiri ni mdogo sana na kuhisi chochote ni mpaka umguse kichwani.( Their brains are very small to entertain two big events at once ! they must drop one event to entertain the other !) ! Ndio maana Nchi hii ni ya MATUKIO hili likija litafunika hili na hakuna impact yoyote na hata hili la RC Paul Makonda litapita muda si mrefu kama unabisha subiri Bunge lianze April! RC Paul Makonda wewe vumilia tu bado KITAMBO KIDOGO WATASAHAU TU!

HYPOTHESIS YA KWANZA:

Nimesoma kwa utulivu sana Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI kuhusu Paul Makonda,Mtu aliyesemwa na akina "Askofu" Gwajima kuwa Paul Christian Makonda anatumia vyeti vyake Ndugu Paul Pierre Christian amekanusha vizuri sana na pia hana dada aitwaye Christina aliyetajwa na akina "Askofu" Gwajima. Hakuna dhambi yoyote jina lako kufanana na la mwingine, Juma Ali wako wangapi Zanzibar? Mohamedi Ali wako wangapi Duniani?!

Sheria inaruhusu kubadili jina na RC Paul Christian Makonda na kama ni kweli alikula kiapo mahakamani kubadili jina basi alijua jina alilokuwa akitaka kutumia la PAUL CHRISTIAN MAKONDA si lake la awali! Kwa nini basi aliende mahakamani?

HYPOTHESIS YA PILI:

Je PAUL CHRISTIAN MAKONDA hawezi kuwa ni mtu makini mwenye "SPECIAL MISSION" kutoka "KITENGO" fulani anayo-accomplish ?!

"Qualities "anazoonyesha RC PAUL MAKONDA zinazoweza ku-support hii hypothesis ni hii ya kupoteza "initial identity yake",pili angalia comments za Mzee Khamesse na familia yake ni watu ambao wamekuwa "disappointed" na tabia za RC PAUL MAKONDA, Nawanukuu kwa mujibu wa JAMHURI, " alikuja hapa kama mara mbili saa saba usiku na saa tano usiku,hakuingia ndani! Hapokei simu na namba anazowapa ni feki muda wote hazipatikani!

Kwa utamuduni wa kiafrika kwa watu waliokulea na tena kwa MUSUKUMA kama PAUL MAKONDA na pia kwa umaarufu na hesima aliyonayo Mzee Suleiman Khamesse lazima kuna KITU HAPA si Bure!!!!!

HYPOTHESIS YA TATU:

Katika vita hii ya Madawa ya kulevya tunajua RC PAUL MAKONDA amefanya jambo ambalo hata Marehemu Amina Chifupa alitaka kujaribu lakini hakulifikia. Kilichompata Amina Chifupa sote tunajua. Hivyo hawa WAUZA UNGA NA WATEGEMEZI WAO HAWAWEZI KUMFURAHIA RC PAUL MAKONDA LAZIMA WAJARIBU KUMWANGAMIZA TU! Na hapa Mheshimiwa Rais DR. JMP kama unaujua ukweli kuhusu kijana huyu basi please MLINDE KWA GHARAMA YOYOTE!
Ndio maana unapoona NAPE NNAUYE anatukuzwa kuwa ni jembe japo ukweli ni kuwa "AMEKURUPUKA" sana na kutozingatia ile dhana ya "collective responsibilty". WENGI WANAPIGANA VITA YA WAUZA UNGA DHIDI YA RC PAUL MAKONDA BILA WAO KUJUA au KWA KUJUA na Nape Nnauye AKIWEMO!

HYPOTHESIS YA NNE:

Kuhusu RC PAUL MAKONDA kuvamia kituo cha CLOUDS pamoja na kupewa Magari na Watuhumiwa wa biashara ya Madawa ya kulevya yaani kampuni za TANGA PETROLEUM LIMITED NA NAS HAULAGE LIMITED. Hapa nikiri wazi kuwa najenga hoja yangu kufuatia maarifa niyopata kutokana na kusoma vitabu vifuatavyo: Kitabu cha The Book of Five Rings cha Mjapani Miyamoto Musashi, Kitabu cha 48 Rules of Power na Kitabu cha Lucifer Principles cha Howard Bloom.

Ukiangalia kwa hao marafiki zake kwa pamoja RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA amejaribu sana kujenga nao urafiki wa karibu mno! Je hii HAIWEZI kuwa ni strategy ya "kum-nail" adui ?! Je CLOUDS media Group hawatajwitajwi katika hii biashara HARAMU ya Madawa ya Kulevya?! Chunguza na fuatilia kifo cha Msanii Albert Mangwea kama MKONO wa CLOUDS MEDIA GROUP hautajwitajwi.

RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA anaweza kuwa ni mtu "HATARI" kuliko anavyochukuliwa ,kubezwa na kudhalilishwa na WATU WENYE UPEO MDOGO kama yule Mnyama niliyemwelezea hapo juu!

Yawezekana RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA akawa sawa na mtu anayetupia kuku wake mahindi pale tu anapotaka kumkamata ili amchinje! ZITTO KABWE anasema ameambiwa kuwa kile kikosi alichotumia RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA "kuvamia" CLOUDS kilikuwa maalum ambacho idhini yake hutolewa na Rais au Boss TISS. Je,tunajuaje kama RC PAUL CHRISTIAN MAKONDA alitumia style ile ya YUDA ISKARIOTE aliyotumia kumtambulisha YESU Christo kwa wale maadui waliofika bustanini kumkamata? Labda RC PAUL MAKONDA "alinusa" kuwa CLOUDS MEDIA GROUP depot yao ya "UNGA" wameihamishia Studio na hivyo akaona aende na kikosi maalum incase ameukuta huo "UNGA" upo awakombe na incase ameukosa awapotezee tu kuwa yeye ni mtu wao na anafuatilia "Kipindi chake".

Kwanini isiwezekane hivyo kama ni huyu PAUL CHRISTIAN MAKONDA ambaye alituhumiwa kumfunga Ridhiwani Kikwete kamba za viatu na bado akaja kumuorodhesha katika orodha ya watu 97 anaowatuhumu kufanya Biashara ya dawa za kulevya!

Amemtaja Ridhiwani Kikwete na Yusufu Manji kuhusika na biashara ya Madawa ya kulevya kitu ambacho MWIGULNCHEMBA hawezi kufanya hata kama angekuwa na ushahidi mkononi!
Tungekuwa na Waandishi makini wangechunguza RC Paul Makonda anapokuwa nje ya Nchi anaongea na akina nani MISSIONS zake ni zipi lakini kwa hawa wetu ambao wakiamka wanakimbia kuangalia leo Mange Kimambi ame -post nini au Jumapili hii "Askofu" Gwajima atamchanaje Paul Makonda!

Hivi ukiwa hujapewa Vyeti uangalie na ukaambiwa uwasikilize wakijenga hoja SAED KUBENEA, BONIPHACE JACOB (MAYOR WA UBUNGO) na RC PAUL MAKONDA nani utasema ana ZIRO! obviousily ni KUBENEA na BONIPHACE JACOB! Je,ZIRO ya Paul Makonda haiwezi kuwa ni ya kutengeneza kwa "SPECIAL MISSION".?!

Albert Einstein alipata kusema kuwa akili iliyotumika kutengeneza tatizo haiwezi kutumika kutatua tatizo hilo.NDUGU WATANZANIA TUTAMBUE KUWA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA NI NGUMU KULIKO TUNAVYOFIKIRIA na kama unabisha kamuulize JAKAYA MRISHO KIKWETE au WILLIAM LUKUVI.

Unayepiga kelele bila kuruhusu kichwa chako kufanya kazi piga tu kelele LAKINI TAMBUA KUWA yawezekana unapiga kelele bila kujua kuwa wewe ni sawa tu na MBUZIaliyeko kwenye banda la mpika supu!"

Kulikuwa na vichaa kadhaa katika wodi ya vichaa. Daktari wao akaamua kuwa evaluate kwa njia tofauti. Akachora mlango katika moja ya kuta akakaa kuwaangalia. Wote kasoro mmoja alikimbilia mlango na kuhangaika kuufungua. Daktari akamfata aliyebakia akiamini sasa yuko sawa. Akamwuliza mbona wewe huhangaiki kufungua mlango? Akitegemea jibu liwe ule si mlango ni mchoro. Yule jamaa alicheka sana akasema, nawashangaa wanavyohangaika, ufunguo ninao mfukoni. Daktari aka conclude kwamba huyu ni kichaa zaidi ya wenzake.

Sasa diallo ndiyo anawaona wenzake wana matatizo. Nilisikia anadai eti yeye ni Harvard Graduate, je kuna ukweli wowote? Au kuna ki kozi alisoma pale?
 
Waweza fikiri upon saw a sana. Lakini kiukweli hakuna kitu kigeni umeandika hapo......blah blah tuuuuuu.......na hitimisho boooovu.....
 
Back
Top Bottom