Antivirus mwaka 2008 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Antivirus mwaka 2008

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 16, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Katika ulimwengu wa komputa moja ya kitu ambacho ni muhimu zaidi ni ulinzi na usalama wa komputa hiyo na vifaa vyake vyake , ili komputa iweze kufanya kazi vizuri basi lazima uwe katika hali nzuri .

  Maana yake inatakiwa iwe kwanza inatumia operating system ambayo ni halali ( genuine ) uhalali nikimaanisha wakati inafanyiwa installation iliingizwa katika mtandao na kusajiliwa na kampuni husika ya operating system hiyo , pamoja na hayo software zingine zote zinatakiwa ziwe halali na zimesajiliwa pamoja na kuwekewa updates za wakati huo .

  Moja ya software hizi ni antivirus , mwaka sasa unapita huku tumeona kuja kwa antivirus za aina mbali mbali katika masoko na zingine katika masoko kuonyesha hali mbaya kiutendaji haswa katika kulinda komputa husika na vifaa vyake kama flashdrive hata vingine ambavyo ni vya kuchomeka .

  Kwenye utendaji huu tunaona kampuni kampuni ya Kaspersky na bidhaa zake kama Internet Security na antivirus , mwaka juzi bidhaa hizi zilifanya kazi vizuri sana tatizo lilikuwa haswa kwa watu waliokuwa wanatumia programu ambazo ni batili unapotumia kaspersky inafuta na kuharibu programu kwa namna moja au nyingine .

  Kutokana na tatizo hilo na mengine mengi kaspersky waliamua kuboresha kwanza antivirus na kuwa na version iliyoitwa 2009 hii mpaka sasa hivi haijafanya mapinduzi yoyote yale badala yake ndio ilizidisha machungu kwa watumiaji wake wengine wanaamua kutumia version za nyuma hata katika review mbali mbali inaonyesha kuna tatizo fulani siju mwaka 2009 watatuletea nini kipya .

  Kwa upande wa mcafee nayo bidhaa yake ya 8.5i imekuwa na tatizo katika autorun hata hivyo tatizo hili hawajaweza kulitatua hata walivyotoa version 8.7 ambayo imetoka katikati ya mwezi wa 10 hata version yake ya 2009 nayo imekuwa na tatizo moja la kukataa kutoka katika computer pindi unapotaka kuiondoa .

  Avg walikuwa na version 7 wakaja na 8 , hii 8 inafanya kazi vizuri sana haswa ukiwa umechomeka katika mtandao ili uwe una update mara kwa mara sema tu inakula sana pesa kwa sababu saa zote inapenda kudial hizo updates na usipo update basi inaji diable na ndio inalala hapo hapo .

  Ila nimependa kitu Fulani walichoongeza katika AVG nacho ni site advisor , hii site advisor yake ni nzuri zaidi kuliko ile ya mcafee pamoja na Norton , pamoja na yote hayo bidhaa za AVG huwa zinatoka kiurahisi pale unapoamua kuiondoa na kutumia bidhaa zingine kama hujaridhika nayo .

  Symantec pamoja na bidhaa zake nyingine nyingi zimekuwa na mtindo ule ule wa kuwa kubwa sana unahitaji computer iliyona spidi kubwa ya RAM ,CPU na vitu vingine ili iweze kufanya kazi vizuri zaidi na usisahau kuchomeka katika mtandao ili iweze kufanya updates za mara kwa mara , nimeona watu kama wanafunzi wa chuo wanapata taabu sana na bidhaa za Symantec kutokana na shuguli zao wanazofanya na jinsi wanavyoshirikiana na vitu kama flashdisks na vingine vya kuchomeka chomeka , ila kuna kitu kilichoongezewa kama identity management ambayo inaweza kulinda vitu kama password zako unavyotumia katika manunuzi mbali mbali mitandaoni , na kwa wale ambao wako majumbani kuna kitu Fulani kinaitwa network map .

  Antivirus nyingine uliyofanya kazi nzuri ni Avast mimi sio mtumiaji wa Avast kwahiyo siwezi kusema chochote kuhusu bidhaa zake lakini sehemu nyingi ninapotembelea na kukuta avast basi usalama wa vitu vilivyomo ndani huwa na uhakika zaidi .

  Ndogo kuna antivirus nyingine inayoitwa ThreatFire nayo kiutendaji ni nzuri sana na ni ndogo inafaa sana kwa wale wanaotumia komputa zenye mwendo mdogo lakini sharti uwe umeunganishwa katika mtandao ili iweze kufanya updates za mara kwa mara

  Hata hivyo kuna antivirus za aina nyingi sana kwa sasa na kampuni nyingi za antivirus zina kuwa na antivirus za bure ambapo unaweza kudownload na kujaribu kabla ya kuamua kununua hizo ambazo ziko juu zaidi .

  Na kwa sasa kampuni nyingi za antivirus pamoja na antispyware ziko katika harakati za kulindi vifaa vinavyochomekwa katika komputa kama flashdisk na vingine vya kuchomeka kuhakikisha usalama zaidi ni ukweli uliowazi kwamba virus wengi sikuhizi wanaambukizwa kwa njia hii .

  Pia kuna ukweli kwamba flashdisk nyingi zilizo masokoni hazina software zozote zile za ulinzi zinazoweza kuzuia virus au kitu cha ajabu kuingia au kuandikwa katika flashdisk hiyo , ingawa kuna programu kama iflash ambayo unaweza kuitumia kulock usb port zote mtu asiweze kuchomeka flash na kuiba data au kuhamisha chochote katika komputa yako

  Jamii nyingi duniani pia zinaunganisha vifaa kama simu na vingine vya mawasiliano katika komputa zao kwahiyo kampuni za antivirus na antispyware nazo ziko katika utaratibu wa kuhakikisha simu hizo haziadhiriwi au kama zikiadhiriwa basi zinaweza kusawishwa na kuondolewa mauchafu yote yale .

  Uzuri wa antivirus na antivirus unatakiwa uweke pale komputa yako inapokuwa haina tatizo lolote sio umeshituka iko slow unataka kuweka antivirus au umeona hivi unakimbilia antivirus hatuendi hivyo , unapotumia antivirus hakikisha sio bandia au batili kama mtu amekuwekea angalia kama ni licenced na isajili kwa majina yako wewe mwenyewe kama ni cooperate katika hizi kampuni basi unatakiwa udhibitishiwe kwamba ni halali na inaweza kutunza usalama wa mali zako .

  Kabla ya kununua antivirus yoyote unaweza kuangalia yafuatayo ukiacha bei na upatikanaji wake .

  1 - Iwe inauwezo wa kuscan email ya aina yoyote pamoja na attachments zilizo katika email hiyo kabla hujaamua kudownload , hata unapotuma attachment antivirus hiyo inatakiwa ukiambie kama ni safe au la .
  2 – Ni virus hiyo programu iwe na firewall yenye uwezo wa kuangalia mawasiliano kati ya komputa yako na zingine inazowasiliana nazo kwa muda huo kama kuna chochote kibaya basi ikupe ujumbe na kukushauri nini cha kufanya .

  3 - Siku hizi sehemu nyingi sana kuna access za wireless , sasa unaponunua antivirus hakikisha inaweza kugundua kama kuna uvamizi wowote unaotaka kufanywa kwa njia ya wireless .

  4 – Je antivirus hiyo inaweza kuscan computa yako muda wowote unaotaka au unaweza kuiwekea muda maalumu wa kuscan computa yako ? kama inaweza hivyo ni antivirus nzuri inakufaa

  5 – Antivirus zote zinahitaji kufanyiwa updates za moja kwa moja ( automatic ) pale unapounganishwa katika mtandao hata ambayo wewe utanunua unatakiwa uwe unaweza kuiupdate inapochomekwa kwenye mtandao .

  6 – Pia inatakiwa uwe na uwezo wa kublock mtu mwingine asiweze kuacess computa yako toka sehemu nyingine ingawa mara nyingi hii ni kazi ya firewall

  7 – Kisha antivirus hiyo inatakiwa isiwe inakula sana memory yako na kuifanya komputa yako kuwa slow ushindwe kufanya kazi zingine , ingawa unashauriwa uiache komputa yenyewe wakati wa kufanya full scan .

  Na huo ndio mwisho wa makala hii fupi maoni mengine niliyoandika ni ya kwangu sio ya kampuni yoyote au kikundi chochote cha watu , unapoamua kutumia antivirus hizo chochote kikitokea mimi sio wa kulaumiwa

  Usiku mwema

  Yona F Maro
   
 2. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #2
  Nov 16, 2008
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  shukrani kaka! kwa maelezo yako ambayo yameni fungua macho.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Shy kama ulivyosema ninakubaliana na wewe kuwa antivirus nyingi zina ukomo wa uwezo kwa virus maana watengeneza virus pia wamekuwa wajanja kuwazunguka watengenezaji wa antivirus.
  Hivyo ni vizuri kuweka antivirus unayoipenda na kuiamini lakini isikupe hakika ya % zote mia kuwa hutapat shida ya virus.
   
Loading...