Habari zinazosambaa mitandaoni ni kwamba, Anthony Diallo, mmiliki wa Star TV na Sahara Media kwa ujumla ameamua kujitishwa zigo la RC wa DSM! Kama habari hizi ni za kweli, basi ni jambo la kushangaza kidogo!
Nimeshangaa kwa sababu agizo la kususiwa RC halikutoka kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari bali lilitoka Jukwaa la Wahariri... TEF pamoja na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania, yaani UTPC.
Hata kama Anthony Diallo aliona agizo hilo halina uhalali, bado nilitarajia angetoa maagizo kwa Mhariri wa Star TV ili yeye ndie atangaze kuendelea na program yao na RC kwa sababu wanaona agizo la TEF & UTPC halina uhalali wowote!!
Kinyume chake, ni Anthony Diallo mwenyewe nae akaamua kutoka mbele.
Kwa ufahamu wangu Diallo sio sehemu ya TEF wala UTPC bali yeye ni mmiliki! Na kama ametoka mbele, kimsingi sio kwamba amefanya hivyo kuwapinga TEF na UTPC bali kuwapinga Wamiliki wa Vyombo vya Habari chini ya MOAT inayoongozwa na Mheshimiwa Reginald Mengi.
Wakati sakata lile lipo bichi, Mzee Mengi chini ya MOAT alilaani vikali kitendo kilichofanywa na RC wa Dar es salaam. Hakukupesa macho na alisema wazi lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya RC wa DSM!
Bila shaka, MOAT iliwaachia Watendaji wake chini ya TEF ndio waangalie ni adhabu gani alistahili RC. Watendaji wake nao wakatoa maamuzi yao.
Hivyo basi, hatua ya Diallo kimsingi sio kwamba anapingana na TEF ambao yeye sio sehemu yao bali anapingana na MOAT. Kwamba, hiyo Star TV ni yake na hakuna wa kumpangia afanye kazi na nani!!
Kama hivyo ndivyo, ni MOAT ndio hasa wanaotakiwa ku-handle rebellious/uasi wa mwanachama mwenzao. Kwavile inawezekana MOAT nanyi hamna mamlaka ya kumpangia Diallo afanye kazi na nani; lakini bado mna mamlaka juu ya mali zenu!
Kama nilivyoshauri hapo awali, mali zenu ni pamoja na magazeti, waandishi wa habari pamoja na wahariri! Na kwavile Diallo hawezi kupangiwa afanye kazi na nani; nanyi MOAT, kwa mtu mmoja mmoja pia mna haki na mamlaka ya kuangalia magazeti yenu yasomwe na kituo kipi na kipi.
Hivyo basi, huu ni wakati wenu wa kutoa agizo kwa magazeti yenu kutosomwa na vituo vya Sahara Media.
Hali kadhalika, Jukwaa la Wahariri ni wakati wenu kutoa maagizo kwa waandishi wenu kutoshiriki vipindi vyovyote vinavyorushwa na Star Media.
Pasipo na kipindi cha kutoka magazetini na ile mijadala inayoita waandishi kutoka media mbalimbali; Sahara Media is nothing!!