MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,520
- 1,368
Masoka Management Training Institute has been elevated to Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) since July this year.
http://dailynews.habarileo.co.tz/home/?id=1966
Naomba niulize sii serikali ilitoa waraka last year kukataza conversion of diploma colleges into Universities? Did this apply to Private colleges as well?
Kwa nini wasijenge Vyuo vipya? Hivi vyuo vinaanzishwa kila mahala- vingine vina wanafunzi 50 au 100 tu- vinatusaidiaje kama Taifa?
Tunaua technical and other diploma college kwa kuvibadili kuwa universities. Ni kweli bado tunahitaji vyuo vikuu lakini hizi skill sets nyingine nazo bado zinahitajika.
Kwa mwendo huu tunaweza kuwa na shortage ya watu wenye skills hizi na ku dilute the whole meaning of a degree. Nchi kama Nigeria na Uganda kuna university graduates wanaendesha taxi. Nasi tunataka kuelekea huko?
Do we have enough wahadhiri with proper qualifications to teach various courses in these Universities!?
1.
2. Hivi kile Chuo Kikuu cha Bukoba kinaendeleaje? Sijawahi kukisikia tena!
Mzalendo halisi Heshima mbele.
Una utani na sie wahaya? Hujui sisi tunasoma Harvad Univeristy, Oxford au University of NY
Nimejaribu kutafuta web yao siioni, kama kuna mtu anajua then naomba ili nipitie nione the quality of teaching staff na resources walizonazo.
Inasikitisha sana. Sasa hv kila anayejisikia anakiita chuo chake University na anapewa kibali hasa kwa miamvuli ya vyuo vikuu vishiriki. Naweza kusema, serikali sasa ipunguze siasa kwenye maswala ya msingi, wasilete siasa za Buzwagi kwenye masuala ya elimu, la sivyo tutaonekana tumekosa muelekeo hasa pale tutakapojiunga na shirikisho (tunaloshinikizwa na viongozi) la Afrika ya Mashariki. Wenzetu Kenya waliona si vyema kubadili colleges kuwa universities wakaleta wawekezaji kama wale walioanzisha Daystar University n.k. The same wawekezaji huwa wanatoa chance kadhaa kwa wazawa wenye vipaji kiasi cha wao kujiunga na hivyo vyuo ambavyo vingi ni vya kimataifa. Sasa hv Kenya hata mtoto wa masikini ana digrii. Sio kama hapa bongo watoto wa masikini wenye digrii ni wale wenye exceptional vipaji, as chuo tegemezi kwa masikini (UDSM) nacho kimegeuka private (practically) though theoretically na kiuongozi ni cha serikali.
Kuna mwana JF mmoja nimeona anatetea swala la hizo colleges kutokuwa na professors au doctors. But sidhani kama anaelewa kuwa Universities huwa zinakuwa assessed on annual basis na kuwa ranked internationally. Chuo kikuu cha DSM mwaka 2005 kilikuwa cha 64 ingawa kina professors wa kumwaga. Sasa sijui hivyo anavyovitetea vina professors wangapi na vitakuwa ranked wapi.
Pia atambue wawekezaji au hata mashirika na miradi ya serikali, wanaajiri based on sehemu mtu aliposoma yaani kama mtu anavyooa based on malezi ya mke mtarajiwa.
Siku hizi elimu imeoza, mfano, UDSM ina lecture rooms ambazo zina uwezo wa kubeba wanafunzi 500, but maprofesa ambao wameshachafuliwa akili na siasa, wana-admit wanafunzi 800 ili tu serikali ipate namna ya kujisifia kuongeza kiwango cha elimu. Huu ni upumbavu uliokomaa. Utakuta wanafunzi wamesimama milangoni, wengine wamekaa chini, ni aibu. Sasa sijui hz ni bora digrii au digrii bora zinazozalishwa hapo. Utakuta uongozi wa chuo unakazana kurekebisha mazingira kwa gharama kubwa wakati hakuna madarasa.
Siku hz, ukienda hivyo vyuo vingine kama Mzumbe, ni aibu, kuna digrii za ajabu. Watu wanapewa A za kumwaga ili tu washindane na vyuo vingine. Wakati ukikaa nao kwenye utendaji ni bora form six au form four. Ni wachache tu ambao wana akili binafsi. Bt these watu hawafundishwi kuelewa but kufaulu na kupata A nyingi ili wakienda kwenye soko waonekane wanafaulu sana. But ukichunguza, utakuta wanafunzi wanajua maswali before hata ya mitihani. Tunakwenda wapi..??
Mimi nafikiri serikali sasa iwekeze nguvu, na kualika wawekezaji kwenye sekta ya elimu rather than kualika wawekezaji wengi kwenye madini yasiyo na manufaa kwa wananchi wa chini. Waangalie mifano ya Kenya kisha wafikirie namna ya kuinua elimu na sio kuchafua elimu.
kishazi,
1. Hakuna mtu anakataa haja ya kuwa vyuo vikuu zaidi. Hoja -kwa nini wasijenge vipya? Why conversion of diploma colleges? Wajenge tu vipya kama Dodoma! Moi started 3 or 4 public health universities- this is the way Tz we must go! Hivi vyuo vidogo vodogo ya 50 to 100 students kwa population ya 40 mil. has so little impact!
2. Sijui kama emphasis ni Elimu ya juu Tz- kwani wapo graduates kibao tu mtaani hakuna job. Massive Investment in elimu ya ufundi 2 au 3 kila wilaya mimi nimgetoa kipaumbele! In 10 to 20 years Tz itakuwa kama nigeria- graduates driva taxi! Well sii mbaya wengine wanaweza tafuta kazi nje though!
Chukua tano:
Nchi nilizoishi walimu wa msingi wana-digrii. Wapiga chapa wana-digrii.
Nafasi ya watu wenye digrii kupata kazi Tanzania ni nyingi tu.
Wenye digrii wanakosa kazi nchini nigeria kwa sababu wanategemea sekta ya mafuta na kuleta kila kitu. Wangetumia mtaji wa mafuta kuanzisha kazi zenye kuleta ajira, tatizo lisingekuwepo.
Halafu kwanini kila mfano ni lazima Tanzania ilinganishwe na Nigeria au Ghana?
Toeni mifano ya Malaysia, South Korea au Singapore.
Suala la Elimu ni kitu nyeti katika nchi. Mie sioni taabu kuwa na vyuo vikuu vingi, hilo sio tatizo. Tatizo ni aina ya elimu itolewayo. Kama inakidhi mahitaji na inaendana na wakati, je inampa competence na skills zinazohotajika katika karne ya 21? if all answers are yes then sioni tatizo. Ila kama jibu ni No then there is no need kuwa na utitiri wa vyuo amabavyo mhitimu ukimpa kazi anakutolea macho!!