Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Bin Maryam,
Tanzania imekuwa na Assistant Medical Officers (AMO) na ndo mhimili ya huduma za afya- kwani madaktari baada ya kupata degree wamekimbilia SA na Botswana!
Singapore- naogopa kuilinganisha na Tz- tunaachana mbali mno! Ghana, Kenya, Uganda- ni fair kujilinganisha nao- kwa kuwa tunafanana fanana vile! Hata Tz na SA nasita kulinganisha!
Alan Greenspan ameelezea Phenomena ya Dutch Bonanza inayosema kuwa nchi zenye kutegemea rasilimali hazifanyi juhudi kufungua sekta nyingine. Wanakuwa na GDP kubwa na un-employment kubwa. Na moja ya nchi hizo ni Nigeria. Wanatumia mafuta kulisha watu, kujenga miji n.k
Nchi kama Singapore ambao hawana rasimali asilia wanatumia watu kujenga nchi na matokeo yake watu wanapata ajira.
Tanzania kwa sasa inapata mapato kutokana na madini na utalii. Tukitegemea madini na utalii kutupatia mahitaji yetu ya kila siku basi ajira kwa wanaomaliza shule zitakuwa za taabu kama ilivyo Nigeria au Ghana.
Lakini kama tutakuwa kama Singapore kwa maana ya kutumia workforce yetu kuleta maendeleo basi ajira zitapatikana na tusiwe na wasiwasi.