Annie Louis

BIN BOR

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
1,013
Reaction score
407
Mama mmoja alikuwa anagombana na mumewe kabla ya kulala.
"Mke wangu vipi, mbona mkali"
"Nimekuta hiki kikaratasi kwenye mfuko wa kaptula yako kimeandikwa Annie Louis. Nataka uniambie ni nani huyu Annie Louis?"
"Aaagh mke wangu kwa wivu tu. Umesahau leo pale leader's club kulikuwa na mbio za mbuzi? Sasa mbuzi niliyetabiri angeshinda ndio jina lake Annie Louis"
"Sasa alishinda?"
"Bahati mbaya hakushinda" mume akamridhisha mkewe, wakalala.

Saa tisa usiku wakati jamaa anakoroma mke akamtikisa kwa nguvu hadi jamaa akadondoka chini. Kwa hasira jamaa akauliza.
"Mke wangu mbona unaniamsha kwa fujo, kuna nini?"
"Chukua simu yako uone. Mbuzi amekutumia meseji, tena kwa kizungu"
 
tehe tehe yaleeee ya shaggy, it wasnt me!! duh
 
kesi ndogo sana hiyo, muambie aliyeandika sms sio Mbuzi ila ni mchungaji
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…