Anna Mghwira: "Maamuzi ya Bunge si mnada wa hadhara kwenda na anayetoa bei kubwa".

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Bajeti yaTanzania 2016 / 2017 inasomwa wakati takribani theluthi moja ya wabunge wako nje ya bunge.

Hali hii hatari sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Bunge linashindwa kabisa kuhimili tofauti za mawazo.

Maamuzi ya Bunge si mnada wa hadhara kwenda na anayetoa bei kubwa; ni zaidi ya wingi ama uchache wetu. Ni juu ya mustakabali wa nchi na utumishi wa umma.

Uongozi wa Bunge na Wabunge wote, tafakarini sana utu, uadilifu na uzalendo wenu kwa taifa letu.

Tofauti za mawazo bungeni zinatakiwa kuongeza ubora wa utendaji si kudhoofisha. Mnairefusha mno safari yetu ya nuru njema.

Mama Anna Mghwira: Mwenyekiti ACT-Wazalendo.
 
Wale wasaka posho huwa hawawazi zaidi ya hela. Wanashindwa kujua bora kumpiga spika kuliko kumkimbia. Wajifunze kwa mabunge mengine.

Maranyingi watu wakijua unazira kwa kila jambo watakuonea kila siku. Na utaona kiroja kingine kinakuja napo watatoka.

Huu ni utoto tu.
 
ndugu yangu unachosema tofauti na ukweli, kama hakuna uhuru wa bunge unategemea wafanyeje?Ina maana hakuna mawazo mbadala ya wabunge wa ccm tu ndy yanayohitajika wakae kuidhinisha kama wewe unavyopenda haikusaidii kufikiri wapinzani wana mawazo ya upuuzi siku zote kaeni muwe mihuri. Ni waTZ wa ajabu wanao shadadia kuminywa kwa uhuru wa bunge, itatuchukua miaka mingi mno kuwa na taifa lenye uchumi wa kati.
 
Nasema kukimbia Bungeni, tena kukimbia kamwanamke ka 1976 tu ni upuuzi ambao hauwezi tokea katika mataifa ya wezetu.

Nasema ni kukosa cha kufanya. Na haita saidia.

Sasa anayewasaidia CCM ni nani kama si wao.

Sisi tuliwachagua ili wapambane na tulijua wanakwenda kwenye mapambano si kupokea posho tu.

Wapambane, waache upuuzi wao wa kuikimbia CCM na watuamilie kilakitu.
ndugu yangu unachosema tofauti na ukweli, kama hakuna uhuru wa bunge unategemea wafanyeje?Ina maana hakuna mawazo mbadala ya wabunge wa ccm tu ndy yanayohitajika wakae kuidhinisha kama wewe unavyopenda haikusaidii kufikiri wapinzani wana mawazo ya upuuzi siku zote kaeni muwe mihuri. Ni waTZ wa ajabu wanao shadadia kuminywa kwa uhuru wa bunge, itatuchukua miaka mingi mno kuwa na taifa lenye uchumi wa kati.
 
Bajeti yaTanzania 2016 / 2017 inasomwa wakati takribani theluthi moja ya wabunge wako nje ya bunge.

Hali hii hatari sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Bunge linashindwa kabisa kuhimili tofauti za mawazo.

Maamuzi ya Bunge si mnada wa hadhara kwenda na anayetoa bei kubwa; ni zaidi ya wingi ama uchache wetu. Ni juu ya mustakabali wa nchi na utumishi wa umma.

Uongozi wa Bunge na Wabunge wote, tafakarini sana utu, uadilifu na uzalendo wenu kwa taifa letu.

Tofauti za mawazo bungeni zinatakiwa kuongeza ubora wa utendaji si kudhoofisha. Mnairefusha mno safari yetu ya nuru njema.

Mama Anna Mghwira: Mwenyekiti ACT-Wazalendo.
Safi sana huyu mama ni Tunu ya Taifa!
 
Back
Top Bottom