Anna Mghwira apinga kuondolewa uenyekiti ACT Wazalendo

Status
Not open for further replies.

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,007
114,354
MGHWIRA APINGA KUVULIWA U-ACT

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira emepinga kuvuliwa uenyekiti wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo na Baraza la Uongozi juzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana muda mfupi baada ya kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa mara ya kwanza na kupokelewa na watumishi wa 'bomani', Mghwira alisema Baraza la Uongozi halina mamlaka ya kumuondoa kwenye nafasi mwenyekiti wa chama.
Aidha, alisema chama hicho kilifanya maamuzi ya haraka.

Alisema wakati waliomvua madaraka ni Baraza Kuu la Chama, mamlaka ya kumpumzisha mwenyekiti kwenye nafasi yake yamekasimiwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama kwa mujibu wa katiba ya ACT-Wazalendo.

“Niliwasiliana na muasisi wa chama ambaye ni mheshimiwa Zitto Kabwe kwa ujumbe wa simu kwamba nilikuwa kwenye pilika pilika za kuapishwa, hivyo nilimtaka asubiri hadi Juni 15 mwaka huu ambapo ningekutana nao kwenye Mkutano Mkuu wa chama," alisema mama Anna.

"Lakini baraza limeamua kufanya maamuzi ya haraka.”
Alisema hata Rais John Magufuli ni mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini pia anatumikia nafasi yake ya urais.

Mama Anna, ambaye anakuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuteuliwa kuongoza mkoa katika historia ya nchi, alisema uamuzi wa Baraza la Uongozi umempunguzia majukumu, hata hivyo.

Aidha, mama Anna alisema nia yake ni kuwatumikia wananchi na kuchochea maendeleo.

Alisema Rais Magufuli aliona yeye ni mwanasiasa mzuri na ndiyo maana akaamua kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ili awatumikie wananchi.

Mghwira aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Jumamosi iliyopita na kuapishwa Jumanne, kuchukua nafasi ya Said Mecki Sadiki aliyemwandikia Rais barua ya kuomba kupumzika.

Chanzo: Nipashe
 
Vyeo Vitamu Sana!!
Nakumbuka Kuna Kanisa Baada Ya Miaka Miwili Huchagua Wazee Wapya Wa Kanisa
Ikafika Mwaka Waliopo Madarakani Wanatakiwa Kupisha Ila Wakagoma Kuondoka

Waumini Wakahoji Hawa Wazee Wanajitolea Hawalipwi Kwanini Wanalazimisha Kubaki Kwenye Hizi Nafasi?
 
Yaani watu wanajitoa ufahamu hata busara za methali wanapuuza!? "Mshika mawili moja humponyoka" Hata hii ndogo mama haijui!?
 
Huyu mama alikuwa na kaheshima fulani hivi. Haiwezekani mtu ambaye katiba ya ccm inamtaka kuhudhuria vikao vyake ngazi ya mkoa then aendelee kuwa mwenyekiti wa chama kingine tena cha upinzani! Huyu mama wasipomuangalia atakuwa kama Lipumba anavyowafanya CUF!
 
Hotuba ya Mh. Rais ilimtisha, alisema anateua wale anaoweza kuatumbua wakati wowote. Sasa lazima mama Mghwira ang'ang'anie kupanda farasi wawili maana mmoja haaminiki.
Kiongozi anayeongoza kwa hofu ameshashindwa hata kabla hajaanza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom