Anna Makinda umepewa ticket ya kugombea Urais

Anna Makinda umepewa ticket ya kugombea Urais

Kabengwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
240
Reaction score
47
Kutokana na vuguvugu la IPTL linaloendelea bungeni na mahakamani, fursa ya pekee imejitokeza kwa Madame Speaker, Anna Makinda kujipatia tiketi rahisi ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais akiwa na support kubwa sana ya wananchi.

Shutuma zote alizonazo za kushindwa kuliongoza Bunge kwa ufasaha kwa kipindi cha miaka minne zinaweza kufutwa na kauli yake moja tu kwa siku ya kesho!

Kauli pekee inayoweza kumpandisha na kumfanya aonekane shujaa wa taifa ni kwa yeye kukubali mjadala wa IPTL/ESCROW ufanyike kesho bungeni.

Ni changamoto ngumu sana kwa Madame Speaker ila ni fursa nzuri sana kisiasa kwa upande wake! Historia haitamsahau kamwe kwa maamuzi yake siku ya kesho.

Na maamuzi hayo ya kuwa upande wa wananchi ni ticket nzuri kwake endapo ataamua kuchukua fomu ya Uraisi na kuamua kupambana na waliojipambanua ambao wengi wana kashfa nyingi sana mbele ya macho ya wananchi.

Fursa za namna hii huwa hazijirudii! Kazi ni kwako Madame Speaker... Take it or leave it.
 
Watamfanyia yale ya Sita wakati yupo juu. Sio rahisi! Amesema hatogombea tena ubunge, sijajua anaenda kulima au la! Ila hii ni fursa ya yeye kumaliza muhula huu akiwa ni mama kipenzi cha watanzania. Wakimtosa, poa tu!
 
kutokana na vuguvugu la iptl linaloendelea bungeni na mahakamani, fursa ya pekee imejitokeza kwa madame speaker, anna makinda kujipatia tiketi rahisi ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais akiwa na support kubwa sana ya wananchi

shutuma zote alizonazo za kushindwa kuliongoza bunge kwa ufasaha kwa kipindi cha miaka minne zinaweza kufutwa na kauli yake moja tu kwa siku ya kesho!

Kauli pekee inayoweza kumpandisha na kumfanya aonekane shujaa wa taifa ni kwa yeye kukubali mjadala wa iptl/escrow ufanyike kesho bungeni.

Ni changamoto ngumu sana kwa madame speaker ila ni fursa nzuri sana kisiasa kwa upande wake! Historia haitamsahau kamwe kwa maamuzi yake siku ya kesho. Na maamuzi hayo ya kuwa upande wa wananchi ni ticket nzuri kwake endapo ataamua kuchukua fomu ya uraisi na kuamua kupambana na waliojipambanua ambao wengi wana kashfa nyingi sana mbele ya macho ya wananchi.

Fursa za namna hii huwa hazijirudii! Kazi ni kwako madame speaker... Take it or leave it...

sikuona kama alikuwa na hoja yenye mashiko.kuna hoja kadhaa aliwahi kuzuia wabunge kuziongelea kwa kigezo cha uwepo wake mahakamani.hata sio kweli kwamba bunge haliwezi kuingiliwa na mtu au chombo chochote, kwani ni kazi ya mahakama kutafsiri sheria na hakuna aliye juu ya sheria.hyo ndo mana halisi ya c/balance.bunge lipo kisheria na linafanya kazi kwa mjibu wa sheria, hvyo likikosea ni mahakama yenye mamlaka ya kutoa tafsiri.nadhani alitakiwa kutoa hoja kwamba cag aliagzwa na bunge ktk kvekeleza majukumu yake na sio et4 bunge haliwezi kuingliwa na chombo chochote.
 
Mahakama imejitoa ufahamu kabisa.. kwel dollar ni shiiida
 
Bado nchi hii haijfikia hatua ya kuongozwa na mwanamke.
 
watamfanyia yale ya sita wakati yupo juu. Sio rahisi! Amesema hatogombea tena ubunge, sijajua anaenda kulima au la! Ila hii ni fursa ya yeye kumaliza muhula huu akiwa ni mama kipenzi cha watanzania. Wakimtosa, poa tu!
wakati akijikakamua hakuwa anajua kama kulikuwa na tamko la mahakama na hakuwa anajua kama kuna watu wameenda mahakamani,angejua asingetoa kauli ile.
 
Siasa ni upepo wa uelekeo wa watu kwa kipindi cha uchaguzi! Uchaguzi umekaribia, Anna Makinda amepata fursa ya kupigania the highest office in the country, kwa uamuzi wake wa kesho! As a politician namshauri a take chances...
 
Kwanza alishasema hata gombea tena ubunge, kilichobaki no Urais! Awabwage mafisadi apate credit kwa wananchi for the rest of her life na kama ata aspire kugombea Urais ataweka changamoto mpya kwenye kinyang'anyiro cha urais
 
Tumuombe makinda ana wakati mgumu sana ktk historia ya maisha yake na kwa watanzania kwa ujumla
 
Mjadala uwepo au usiwepo hakuna cha Rais kutoka CCM tena, mara buku kabisa hawa wasaka tunge wakubwa. Hivi kama Mahakama inasema hakuna kujadili ripoti ya CAG au TAKUKURU kwani Rais anazuiwa na nani kuwafukuza wezi na rais kuagiza washtakiwe? Wote huu ni usanii wa CCM kwa vile imewaona Watanzania ni mabwege.
Watu ni walewale kila siku wanaiba mabilioni ya shilingi kisha zinaletwa sarakasi za bungeni halafu yanaisha wakati maelfu ya watu wa nchi hii wamepoteza maisha kwa vyanzo vinavyotokana na wachache kujimilikisha fedha za umma.
Nyerere na Sokoine wangefufuka na tukawapa nchi waongoze kwa wiki mbili tuu kisha wafe tena nadhani wangeiacha nchi tukiheshimiana.
Leo hii eti tunaambiwa Mawaziri wanawatumia majambazi kama Chief Kiumbe kusambaza nyaraka feki ili kulivuruga Bunge na sisi tunaona kawaida kama mazuzu vile. Wallah kama mie Rais huyo Muhongo namchapa makonde kwanza kisha barua ya kumfukuza ataikuta kwa mkewe. غعف نخهح لصشسبف خى xyz £€ @ kabisa!
 
kuweni serious jamani pamoja na makando kando na sarakasi zooooote bado mnafikiria hili lichama liwapatie viongozi, kweli, kweli, kweliiiiiiiiiiiiiii! akha! hili halikubaliki
 
Madame Speaker tangaza nia! Umeweka mark kwenye siasa za Tanzania!
 
Bado nchi hii haijfikia hatua ya kuongozwa na mwanamke.

Watu wanashindwa kuwaangalia wanawake kwa upande wao wa pili,mkitaka kujua udhaifu wa mwanamke fuatilieni kwanini mama Clintoni alishindwa na badala yake chama kikampitisha Obama awe presidential candidate na then rais
 
Aisee huyu mama amejizolea sifa si za kawaida. Wengi tulimfikiria vingine kabisa huyu mama. MH.SITA NAMBA MBILI. Wanawake kweli wanaweza hata bila kuwezeshwa. Mh. Makinda oyeee...!
 
Huyu Mama Hana Uwezo wa Kuwa Rais kwa namna yoyote ile.
 
Kumbe huyu spika na naibu wake wakiamua wanaweza? Dah! Taifa limezizima.
 
Back
Top Bottom