Animations za Kitanzania

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Hebu tujuzane animations za Kibongo. Japo tasnia hii bado haijakua lakini kuna chache zimetengenezwa. Hebu tujuzane Animations za kitanzania. Mimi nazifahamu hizi chache.

1. Zamani ilikuwepo moja inaonyeshwa ITV, dogo fulani wa kike akiitwa sara. Nafikiri kuna watu wa nje walikuwa wanafadhili. Mafikiri hakuna animation ya kitanzania bora kama ile.

2. Kuna moja naionaga Youtube ni stori ya madenge na Dimoso. Japo quality siyo kivilr ila inafurahisha sana.

3. Kuna hawa jamaa wa ASAS wana tangazo lao la maganja na makundubai, wako vizuri japo quality bado chenga.

4. Kuna jamaa nasikia wametengeneza animated film. Wanaaita Mbulaland. Sijaiona ila wanadai wanaionyesha kwenye maonyesho ya film ya Zanzibar.

Animations gani zingine unazifahamu zimetengenezwa na watz?
 
MbuLand na Mozizi zote zilikuwepo ZIFF....not bad at all!

Hilo tangazo la ASAS binafsi silipendi hata kidogo...sina uhakika kama ni ile lafudhi ya kulazimisha ama nini 😏
 
MbuLand na Mozizi zote zilikuwepo ZIFF....not bad at all!

Hilo tangazo la ASAS binafsi silipendi hata kidogo...sina uhakika kama ni ile lafudhi ya kulazimisha ama nini 😏
Hahaaa, mimi linalifurahishaga. Hao Mozizi nayo ya bongo? Bahati mbaya hawajaweka matrailer youtube.
 
Back
Top Bottom