Anguko la Facebook liko karibu

Sella turcica

Senior Member
Oct 13, 2020
104
193
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Ni wazi kuwa wengi wetu tunatumia au tuliwahi kutumia Facebook katika kipindi fulani. Nakumbuka miaka ya 2013 nilikuwa naazima simu kwa watu ili niingie Facebook. Ila baadae niliacha kabisa kutumia huo mtandao.

Lakini mada yangu hasa ni kuhusu WhatsApp na sera ya faragha waliyotoa juzi hapa. Facebook iliinunua WhatsApp mwaka 2014 kwa $19 billion na tangu wakati huo WhatsApp imekuwa ikiingizia Facebook mapato kidogo sana. Kuanzia mwaka 2016 WhatsApp imekuwa ikishare data za watumiaji na kampuni ya Facebook bila wateja kuambiwa. Wapo baadhi waliojitoa ila wengi hawakujua nini kinaendelea.

Juzi kati hapa WhatsApp imekuwa ikituma notification kwa wateja wake kwamba watatakiwa kukubaliana na sera mpya ya faragha kuanzia February 8 au kama hawatakubali basi watashindwa kutumia huduma yao. Watu wengi wamekasirikia hicho kitendo na ikapelekea wemgi kuanza kupakua apps nyingine za kuchat kama telegram na signal. Juzi tarehe 15 wakatoa maelezo ya kuongeza muda kutoka tarehe 8 February hadi 15 May. Hawakusema kuwa watabadilisha chochote, ila wamewapa muda zaidi kwa ajili ya kutafakari.

Sijui Facebook wanajiamini nini hadi kuwa na kiburi cha kuwaambia watu kwamba aidha wakubali data zao kuchukuliwa kwa ajili ya matangazo au waache kutumia WhatsApp. Je, wanadhani kwamba bila WhatsApp maisha hayawezi kwenda?

Facebook imekuwa ikiandamwa na scandals za kutumia vibaya data za wateja wake kwa miaka mingi. Naona kuanguka kwa Facebook kuko njiani.

Zilikuwepo kampuni kubwa tu hapo nyuma lakini walipoharibu na kuchukulia mambo for granted wakapotezwa kwenye soko. Nani alijua kuwa simu za Nokia zingekuja kuwa adimu? Nani alijua BlackBerry ingekuja kupotezwa?

Kitu pekee ambacho kwa sasa Facebook inajivunia ni kwamba WhatsApp ina watumiaji wengi. Almost kila mwenye smartphone atakuwa na WhatsApp. Lakini wakiendelea hivyo mambo yanaweza kuja kubadilika. Kuna apps zinakuja kwa kasi kama telegram na signal. Wasiposoma alama za nyakati suala la Facebook kutawala ulimwengu wa mitandao ya kijamii litakuja kuwa historia.

App-privacy-labels-messaging-apps.jpg
 
Ni kweli watu wengi hawalijui hili mi Ni mmoja wao waliokataa hapa nachosubili kufungiwa tu
 
Na sisi tutaanzisha,
CHATObook
Chato imeingiaje?

Jaribuni kuwa wapinzani wenye busara bwana siyo wachochezi mnashindwa kuleta sera zenu mnakalia kumzonga mtu kila kukicha wakati hamuwezi kumzuia inatusaia nini?
 
Back
Top Bottom