Anguko la Diamond Platnumz

Mbona kila mtu anamponda mtoa mada hayo ni maoni yake. Mpinge kwa hoja sio kutoa maneno kwa kukurupuka.
 
Join Date : 27th January 2015

Location : Dar es salaam
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received1
Likes Given
0
Ndilo hili lililokufanya ujiunge jf!?
 
Dah! yaani umejiunga jana tu, leo umeanza kutia unafiki na umbea! Mmmmmmmmmm! ndugu yangu. kwetu kule Iringa Mwagito ni Kijana wa kiume, sasa kwa huu umbea, naogopa hata kusalimiana na wewe kikwetu! Lazima utakuwa una mume!
yaani kumfananisha Diamond na Ya moto band ni sawa na kufananisha Zidane na Lunyamila
 
uko hivi badala ya kufanya mambo yako unakaa kufuatilia mambo ya wengine huku ukifurahi kushuka kimafanikio kwao na vice versa.

Kwa hiyo nikifatilia mfano incident ya Lipumba, Tezi dume et al ni mambo ya kike?, vitu vingine mkishindwa kutolea maana bora mkae kimya
 
Bro ungeendelea tu kusaka ajira, najua una hasira hadi sasa unamchukia Diomond lakini siyo yeye aliyesababisha matatizo ya nchi hii, chukia viongozi na ujinga wako wa kutumika wakati wa kampeni.. graduates watanzania miaka hii jinga sana!
 
Hii chuki yako imetokana na ugumu wa maisha pole mkuu

Kaza aliyekupita kakupita tuu.
 
uyu alie post hakna akil kichwan mwake ata moja naweza sema aache ujinga, na nyimbo za tanzania zinazikilizwa kwa wingi mpaka Sasa Hadi Miaka Ijayo Kwa Sababu Ya Diamond Ilo Halina Ubishi Kila Mtu Anajua.mwambye Aende Kwenye Blog Ya Udaku.
 
Badala ya kumchukia na kujaribu kuyashusha mafanikio ya Mtanzania mwenzenu kwanini msijaribu kukaa na kuangalia wengine watafika vipi huko alikofika Diamond..? Maana ninavyosoma posts & comments hapa JF inaonyesha kama kuna kampeni ya kujaribu kumshusha Diamond bila ya sababu za msingi.. Japo sio mpenzi sana wa nyimbo za vijana lakini Diamond amenivutia na juhudi zake za kufika hapo alipofika..
 

hawa ndio wanakuja kutesa watu uzeeni kwa ombaomba sababu ya kuwa na umbea
 

dua ya kuku haimpati mwewe, diamond yuko makini sana na si mtu wa kuridhika na mafanikio
 

Diamond atalinganishwa na Ali Kiba na sio vinginevyo. Utasubiri sana kuona anguko la huyu kijana Diamond. Kwanza kama walivyosema waliotangulia wewe umejiunga jf. jana kwa ajili ya kupost uzi huu wa wivu na utambue unatumika vibaya.
 
Diamond atalinganishwa na Ali Kiba na sio vinginevyo. Utasubiri sana kuona anguko la huyu kijana Diamond. Kwanza kama walivyosema waliotangulia wewe umejiunga jf. jana kwa ajili ya kupost uzi huu wa wivu na utambue unatumika vibaya.

Umeni-quote mie haya..???
 

Kuendelea kwa wasanii wengine haimaanishi diamond anashuka, kiufupi tunataka wengi waendelee
 
Ila hata kama anguko lipo, lakini ameshamake pesa za kutosha; kuwekeza kwa miradi mingine. Naamini mtu hawezi ishi katika umaarufu kwa miaka mingi sana...ipo siku lazima ashuke..... Kuwahi kufanikiwa maishani huweza kupelekea kuwahi kuchuja au kwisha.....unabaki wa kawaida tu...its normal.
 

Aisee..... kweli umaarufu umeshuka dah! hadi nimecheka peke yangu🙂
 
Yaani kajiunga jf na post ya kwanza diamond

Badala ya kumuombea mwenzake mazuri ili achangie kwenye uchumi wa nchi yeye hapati usingizi kwa kumuwazia mabaya.

Ama kweli kuna watu na viatu.
 
Diamond alipotoa wimbo wa 'Mbagala' ndipo nyota yake ilipozidi kung'aa sana,na alipoacha kufanya kazi na studio ya Sharobaro ndipo wengi tulifikiri ingekuwa mwisho wake,na ndipo akaja na nyimbo mbili za 'mawazo' na nyingine imenitoka jina. Ndipo watu wakasema huu ni wakati wa Diamond. Lakini alipotoa wimbo wa 'nataka kulewa' zilitokea story za pembeni na takribani wasanii wawili wakadai wameibiwa wimbo huo.
Ndipo akaja akatoa wimbo wa 'kesho',hakuna aliyeongea kuhusu wimbo huu ambao uliendelea kun'garisha nyota yake afrika mashariki. Baadae akaja kutoa wimbo wa 'Number one' wimbo ulimpelekea kutambulika bara zima la Afrika,hususani baada ya kufanya remix ya wimbo huu. Sitaki kuzungumzia kwa upande wa nyimbo zake nyingine kama mdogo mdogo au bumbum ile aliyofanya na msanii Iyanya.
Kwa ufupi ni vigumu kuzungumzia mwisho wa Diamond kwa sasa. Ila ni msanii ambaye lazima nikiri kuwa anajua kucheza na akili za mashabiki wa muziki na ni msanii mwenye juhudi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…