MwanaPekee
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 382
- 386
Hivi karibuni BM akiongea na wananchi wachache wa Mkoa wa Lindi, ambao taarifa zilizopo ni kuwa ulitumika ushawishi wa fedha kuwakusanya; alisikika akikitaka Chama cha Mapinduzi kumsafisha kwa kile alichodai kuchafuliwa ili aweze kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu. BM alitishia kwamba iwapo hatasafishwa basi atafanya maamuzi mengine, ambayo wachambuzi wa siasa wanatafsiri kauli yake hiyo kuwa inaashiria kuwa atahama CCM na kwenda katika moja ya vyama vya upinzani.
BM aliwahoji watu hao akisema, “Uchaguzi ni mwezi wa ngapi?” akajibiwa, “Wa kumi”. Akauliza tena, “Huu ni mwezi wa ngapi?” akajibiwa “Wa sita”. Akamalizia kwa kusema, “Chochote kinaweza kutokea hapa katikati”.
Ninachokiona hapa ni kuwa BM anajua wazi kuwa viongozi wa CCM hawatanasa katika mtego wake wa kutaka kusafishwa, kwani makosa aliyoyafanya ni dhahiri kabisa. Kwa sababu hiyo alitumia wasaa huo kuutangazia umma kuwa anahamia upinzani. Chama gani? Hakutaja. Ijapokuwa mtu ukiongeza za kwako tu utajua ni chama kipi, kwani mtaji wa chama ni Wanachama. CDM hawawezi kuingia tena kwenye mchezo wa “Kubadili gia angani” kama walivyofanya 2015 na sasa wana watia nia wengi tu. Kwa kuwa vyama vinavyofuatia kwa kuwa na washabiki wengi baada ya CDM ni CUF (Lipumba ametangaza nia), then ACT-Wazalendo (Hawana mgombea hadi sasa) basi anaweza hamia kwenye kimojawapo.
NINI KITATOKEA? Kuna wanaosema BM atahama na wafuasi wake kwenda huko aendako na kutoa political mileage kwa chama hicho. But ukweli ni kuwa BM hana wafuasi wengi kama ambavyo wengine wanadhani, bali ni mdomo wake tu na kujifanya kuwa ni mtu muhimu sana ndani ya chama na serikali ambapo kimsingi zama zake zilishapita kitambo. Isitoshe, hakuna watu watakaotaka ku-risk nafasi zao kisiasa wakijua wazi kuwa BM hana hata sera moja inayomuuza na hivyo kuwafanya Watanzania wamwamini na kumchagua kama Rais. Kimsingi hata kama bado hawajaingia ulingoni, BM ashapigwa “KO” na Magu kwani maendeleo aliyoyafanya Rais huyu ni unprecedented.
Mvuto aliokuwa nao Edo 2015 hauwezi kufananishwa hata chembe na BM kwa sasa ambaye kwa wakati huo Watanzania walimkataa katakata. Hata hivyo mbali na mvuto huo wa Edo, alishangaa kuona kuwa amehama almost peke yake licha ya kuwa na matumaini makubwa kuwa kuna wimbi kubwa la wana CCM lingemfuata.
BM ndo atakufa mchana kweupe kabisa na huwenda asifuatwe hata na mtu mmoja, labda acheze filamu kwa kuwanunua watu kama ambavyo ameshaanza kuwalaghai Watanzania kuwa eti “mioyo ya vijana inachemka” kote nchini. Kuna wakati unajiuliza, ni vijana wa wapi hao ambao wanamtaka BM, maana kila unayeongea naye hataki hata kusikia jina la mtu huyo. Baada ya uchaguzi Mkuu atarudi CCM na huo ndo utakuwa mwisho wa BM kisiasa, as kaburi lake la siasa litafukiwa rasmi.