Anguko kuu la CHADEMA

Anguko kuu la CHADEMA

RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
679
Reaction score
1,220
Habari ya asubuhi wanabodi?

Ni tumaini langu kwamba tuko salama na tunaendelea kupambana katika kulijenga taifa letu.

Ndugu wanabodi katika kuendelea na mapambano ya kulijenga taifa letu nawaomba sana msijisahau kujilinda na ugonjwa wa COVID-19. Tuendelee kuchukua tahadhali na kuwa waangalifu wa hali ya juu.

Wanabodi wa JF, kama kichwa cha uzi huu kisemavyo hapo juu ni kwamba CHADEMA ni chama cha ajabu sana kwani kimeshindwa kusimamia misingi ya demokrasia na haki asilia(Natural justice). Kwa mantiki hii CHADEMA mwaka huu imejichimbia kaburi bila kujijua.

Wanabodi, CHADEMA ni chama ambacho kinahubiri demokrasia na wakati mwingine huwa wanenda mbali zaidi na kumtuhumu mheshimiwa Rais wa JMT kwamba ni dikteta, hapendi ushauri n.k ila kwa kipindi hiki CHADEMA imedhihirisha ni jinsi gani walivyo wanafiki, wazandiki na madikteta kutokana na matendo ya mwenyekiti wao.

Wanabodi, CHADEMA kuwafukuza wabunge wake bila kuwapa haki ya kuwasikiliza wanatuonesha picha gani sisi wananchi wa kawaida?

Wanabodi, CHADEMA kutoa amri kwa wabunge wake wasiingie bungeni na kukataa kueleza lengo la hiyo amri na sababu za msingi za kufikia huo uamuzi wa kutokuingia bungeni na kutowashilikisha wabunge wake katika hilo jambo, je inaleta picha gani kwa wananchi wa kawaida na wanachama wake?

CHADEMA, kuwakata wabunge mishahara yao kwa ajili ya kuanzisha akaunti maalumu ambayo itawasaidia wabunge hao katika kampeni pale ambapo watakuwa wamekwama na kutumia hiy o hela kinyume na makubaliano ya wanufaika(wabunge wa CHADEMA) inaleta picha gani kwa jamii?

WanaCHADEMA ile demokrasia, utawala wa sheria na haki asilia ambayo mmekuwa mkihubiri bungeni, kwenye mitandao ya kijamii iko wapi katika chama chenu? Kwanini mnapenda kuwanyooshea wezenu vidole kwamba wao ni wachafu wakati nyie ndiyo wachafu wakuu, wazandiki na wanafiki wakubwa?

Kwa mantiki hiyo, mkipewa dhamana ya kuongoza nchi yetu mnataweza kweli? Kama mambo mmeshindwa kutekeleza katiba yenu pamoja na katiba ya JMT mtawezaje kuongoza nchi?

Mwaka 2005 nilitokea kuipenda sana CHADEMA kwani ilikuwa na watu wenye uwezo mkubwa sana katika mambo ya kisiasa. Waliposimama kutoa hotuba/hoja hakika ni watu ambao walionesha uwezo, ukomavu na weledi katika siasa. Ila kutokana na udikteta wa DJ umesababisha anguko kubwa sana la CHADEMA. Wale watu wote wameanza kuikimbia CHADEMA kwani inaongozwa na mtu ambaye siyo sahihi. Siku zote ni ngumu sana mtu mwenye akili ndogo kumuongoza mtu mwenye akili kubwa na ndiyo maana Dr. slaa, Zito Kabwe na wenzake waliondoka mapema CHADEMA kwani waliona mbali sana kama mnabii.

Mwisho, CHADEMA acheni unafiki wenu. Unafiki ni jambo baya sana katika Dunia hii. Kama mnafikiri wananchi hawaoni mnachofanya nawapa pole sana. Kwa sasa wananchi tupo makini sana. Sijui kwa mwaka huu matakuja na sera gani za kuwashawishi wanachi.

Ahsanteni na karibuni kwa michango.
 
Lakini mwenye nchi yuko Rubondo anafanya nini? Ameikimbia korona. Hivi aliyekaa mafichoni huku anawaambia wenzake wachape kazi,wasitishwe. Na na ambaye ameonesha hofu ya dhahiri yupi ni mnafiki. Nadhani kuna haja ya kujua maana ya manafiki. Wewe mtoa mada ndo mnafiki maana unajifanya huujui ukweli wakati unajua. Chadema inasimamia kile inachokiamini. Ila wewe ni bendera fata upepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe ndo Mungu wakweli hapa Tz kilichobaki nikumuomba Mungu wetu Mbowe aendelee kutuponya sisi vilaza walumumba wenye PhD fake na tuliobashite.
 
Ndani ya hichi chama kuna ukandamizaji mkubwa... Msidanganyike na maneno ya mataga wa huku nje.
 
Ahsante Lumumba buku saba.Lakini mwenye nchi yuko Rubondo anafanya nini?Ameikimbia korona.Hivi aliyekaa mafichoni huku anawaambia wenzake wachape kazi,wasitishwe.Na na ambaye ameonesha hofu ya dhahiri yupi ni mnafiki.Nadhani kuna haja ya kujua maana ya manafiki.Wewe mtoa mada ndo mnafiki maana unajifanya huujui ukweli wakati unajua.Chadema inasimamia kile inachokiamini.Ila wewe ni bendera fata upepo

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani mtu akitoa mawazo yake yasipowafurahisha basi kalipwa buku saba...Hadi Lijualikali alilipwa buku saba!!! Hakuna anayekubali kukandamizwa na kulazimishwa kufanya vitu ambavyo sio ilhali uhalisia anauona. Msipobadilika mbona mtaita kila mTz buku saba.
 
Mkuu mimi siyo mwanchama wa CCM nimesahau kuliweka wazi hilo jambo.
 
Ofisi ya Bunge inapomlipa mshahara mbunge inalipa kwenye akaunti yake binafsi au akaunti ya chama?

Jibu liko wazi pesa inawekwa kwenye akaunti ya mbunge.

Anapotoa pesa kwenye akaunti yake binafsi akapeleka kwenye chama kwa sababu yeyote ile hawezi kusema amelazimishwa kuna hiyari hapo wasitudanganye.
 
Lakini mwenye nchi yuko Rubondo anafanya nini? Ameikimbia korona. Hivi aliyekaa mafichoni huku anawaambia wenzake wachape kazi,wasitishwe. Na na ambaye ameonesha hofu ya dhahiri yupi ni mnafiki. Nadhani kuna haja ya kujua maana ya manafiki. Wewe mtoa mada ndo mnafiki maana unajifanya huujui ukweli wakati unajua. Chadema inasimamia kile inachokiamini. Ila wewe ni bendera fata upepo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kakimbia basi kiti ki wazi cha urais. Sasa nakushauri kakalie kiti hicho ujitangaze wewe kuwa ndo raisi tuone. Ukishindwa basi mwenye kiti chake yupo anachapa kazi.
 
Yaani mtu akitoa mawazo yake yasipowafurahisha basi kalipwa buku saba...Hadi Lijualikali alilipwa buku saba!!! Hakuna anayekubali kukandamizwa na kulazimishwa kufanya vitu ambavyo sio ilhali uhalisia anauona. Msipobadilika mbona mtaita kila mTz buku saba.
Wanasikitisha sana hawa watu. Tatizo la hawa sycophants wa CDM ni kwamba uwezo wao mdogo sana. Sifa kubwa ya mtu mwenye uwezo mdogo ni kutokukubali hoja au ya/ la mtu mwingine, chuki bila sababu n.k
 
Back
Top Bottom