Angola kurusha satelaiti muda mfupi ujao

Mzawa_G

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
669
Reaction score
1,479
Nchi ya Angola ambayo inapatikana huko upande wa magharibi kusini mwa afrika , basi wapo mbioni kurusha satellite yao nyengine ambayo itajulikana kama Ango-sat 2 ambayo itakwenda kuchukua nafasi ya Ango-sat 1 ambayo ilishindwa kufanya kazi mara baada ya kufika katika orbit ya dunia yetu

Urushwaji wa satillite kwa nchi ya Angola utakwenda kuongeza nguvu katika moja ya shirika lao la wananchi ambalo linajihusisha na shughuli mbalimbali za anga za mbali linalofahamika kama ( Angolan government national space Program ) na vikundi mbalimbali vya watu wachache vinavyojihusisha na mambo ya anga za mbali

Ango-sat 2 itaweza kurusha masafa yote ya band za C , Ku na Ka ( transponder ) kumbuka mfumo huu wa Ka unatumika zaidi katika kurusha na kupokea mawimbi makubwa zaidi yale yanayobeba mfumo ya internet na mengineyo hata urushwaji wa picha za video kwenda kwenye kituo cha kupokelea

Serikali ya Angola imewapa tena shirika la anga la Urusi ili kuweza kuwarushia satellite hii ambayo imetengenezwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Airbus

Satellite itabebwa na rocket ya Proton-M/DM-3 ambapo itarushwa huko Baikonur Kazakhstan muda wowote kuanzia sasa na pia ndani ya rocket hiyo kutakuwa na vifaa mbalimbali vya russia ambapo vimepangwa kwenda kufanyiwa uchunguzi huko anga za mbali.

By. Gerald
FB_IMG_1665518398858.jpg
 
Nimeweka kambi hapa ,ila taifa hili kwa uchumi wako siyo haba jmn nasiki Ni ya tatu kwa Africa kwa utajiri baada ya Afrika Kusini na Nigeria

JamiiForums-1466141388_720x718.jpg
 
Huko wanasomaje..sisi hata maji ya kunywa bado hayajawafikia watu..umeme tu Ni shida.

Ila kuongoza Tz Ni kazi Sana raia wake Ni msukule kazi yao Ni kupelekwa pelekwa na kushabikia simba na yanga.

Viongozi wao Ni wachawi wanatami kula nyama za wananchi wao kupitia Kodi, rushwa, wizi,

Tunasafari ndefu sana
 
Aaah! Ili taifa inawezekana Mungu anatupa adhabu kam ya wa Israeli kabla ya kufika Kanaani ...
 
Nchi ya Angola ambayo inapatikana huko upande wa magharibi kusini mwa afrika , basi wapo mbioni kurusha satellite yao nyengine ambayo itajulikana kama Ango-sat 2 ambayo itakwenda kuchukua nafasi ya Ango-sat 1 ambayo ilishindwa kufanya kazi mara baada ya kufika katika orbit ya dunia yetu

Urushwaji wa satillite kwa nchi ya Angola utakwenda kuongeza nguvu katika moja ya shirika lao la wananchi ambalo linajihusisha na shughuli mbalimbali za anga za mbali linalofahamika kama ( Angolan government national space Program ) na vikundi mbalimbali vya watu wachache vinavyojihusisha na mambo ya anga za mbali

Ango-sat 2 itaweza kurusha masafa yote ya band za C , Ku na Ka ( transponder ) kumbuka mfumo huu wa Ka unatumika zaidi katika kurusha na kupokea mawimbi makubwa zaidi yale yanayobeba mfumo ya internet na mengineyo hata urushwaji wa picha za video kwenda kwenye kituo cha kupokelea

Serikali ya Angola imewapa tena shirika la anga la Urusi ili kuweza kuwarushia satellite hii ambayo imetengenezwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Airbus

Satellite itabebwa na rocket ya Proton-M/DM-3 ambapo itarushwa huko Baikonur Kazakhstan muda wowote kuanzia sasa na pia ndani ya rocket hiyo kutakuwa na vifaa mbalimbali vya russia ambapo vimepangwa kwenda kufanyiwa uchunguzi huko anga za mbali.

By. GeraldView attachment 2384156
Sisi tuendelee kurusha MANENO tu walah😡😡😡
 
Hapa Tanzania , hata Toilet paper ya kuchamba matakore hamna .
 
Back
Top Bottom