Angestaafu May 2017 na kulipwa mafao yake Mil 134.7, sasa agundulika ana vyeti feki

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Habari za asubuhi ndugu zangu.

Rungu la wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki ,limemkumba mhandisi mmoja wa jijini Mwanza ambaye alikuwa astaafu May 2017 na kupewa mafao yake ambayo yanafikia Million 134.7 fedha za kitanzania. Sasa ameambiwa vyeti vyake siyo halali, hivyo anatakiwa kutimiza agizo la Mh Rais, Dk JPM alilolitoa Dodoma siku 3 zilizopita.

Huyu mhandisi (Civil Engineer) amefanya kazi za civil nyingi sana mkoani Mwanza na ziko vizuri tu. Sijajua huo mchakato wake wa vyeti.

Mungu ampe wepesi.
 
Kwa ni kwa akili yako mtu aliyefoji cheti hana akili?Kwa leo unaweza kusema ndio,ila kwa zamani watu walikuwa wakikosa nafasi za sekondari hata kama una akili namna gani.
Kosa ni kughushi.
Unataka kuniambia MTU anaweza Fiji vyeti kwakua tu uwezo anao ila nafasi amekosa?, na kama jibu ni ndiyo awajibike. Lakini Nina mashaka nna huo utetezi wako.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Anaweza akafoji cheti lkn asiwe kafoji utaalamu,utaalamu ni wake ila cheti si chake lkn sababu kinachoangaliwa ni vyeti ndio utendaji na si utaalamu hakuna jinsi.Cha msingi atulie utakuja utawala mwingine atapata haki yake.Kila utawala una kitabu chake.
 
Habari za asubuhi ndugu zangu.

Rungu la wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki ,limemkumba mhandisi mmoja wa jijini Mwanza ambaye alikuwa astaafu May 2017 na kupewa mafao yake ambayo yanafikia Million 134.7 fedha za kitanzania. Sasa ameambiwa vyeti vyake siyo halali, hivyo anatakiwa kutimiza agizo la Mh Rais, Dk JPM alilolitoa Dodoma siku 3 zilizopita.

Huyu mhandisi (Civil Engineer) amefanya kazi za civil nyingi sana mkoani Mwanza na ziko vizuri tu. Sijajua huo mchakato wake wa vyeti.

Mungu ampe wepesi.

Wanamuua hivi hivi wakati Bashite anatanua tu! Double standards!
 
Mi nahamini haya majina ya wafanykazi wenye vyeti feki wapo walionewa wana vyeti halali
 
Back
Top Bottom