Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 76,355
- 108,485
"Vimada kutwa wako zanzi, Mie ndani nakuna nazi" Angela wivu umemzidia
Hahah kumbe nawe wamo eenh...
"Vimada kutwa wako zanzi, Mie ndani nakuna nazi" Angela wivu umemzidia
Wacha wenzako nao wajilie wewe msubiri nyumbani saa nane za usiku
Hahah kumbe nawe wamo eenh...
mmmmmh!! Embu nisalimie kwanza......wenzako tulitungia mashairi nyimbo za Mbaraka MwinsheheUmenikumbusha kwenye mitihani ya Kiswahili kutunga ushairi ilikua balaa basi ntafikiriaa mistari ya diamondi nikiona haielekei nahamia ya stamina nikiona namna gani nachukua mistari ya bibi kidude
Nilikua nanunaje!!??maana kutunga mashairi kipaji afadhali hata utenzi
Angela nimekuja kukujibu Mentor Mume wangu!
Waungwana mwenzenu nipeni pole, Mwenzeu sipendwi kama upele
Wenzngu wamepata waume wapole, Mie nabakia napiga kelele
Mwanaume niajua ni mwenda pole, kumbe ndo mla nyama mwenda pole
Tarajio langu la ndo limepotea kizani
Mwanaume mvuvi halisi, Wala huvui vingisi
Si kazi Huotea mifulusi, Majabi huya jalisi
Haogopi kaskazi wala kusi, Kutwa kuntia mie nuksi
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Niliamua niolewe na anenifaa, Mume mwenye kusfiwa
Niolewe mie ndoani nipate kuzaa, Kama vile nilivozaliwa
Mengi niliahidiwa mume kunituzaa, Zote ahadi hewa
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Nikavishwa johoza kifahari, Nikajua ndoa ni ya kheri
Mama yangu aliona fahari, Bintie kumlete uzeeni kheri
Nikajua nitaiepuka mibuzi shari, Nimtendee mume kila lakheri
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Mume wewe si mume tena, Bali gume gume aliokataza Mtume
Mume wanifoke mbele ya wana, Huna hata mswalie mtume
Kila siku wewe kunitukana, Hjui maana ya mume
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Wenzangu wapigwa na khanga, Mie najikaza nibaki kulea wana
Dharau zako kali kama upanga, Najitahidi hapa kwako kujibana
Nikiondoka nita tanga tanga, Pia nitawatesa wangu wana.
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Hali ngumu kulalama, ilihali washinda bar na kina salma
Watoto kutwa walalama, Mie nawambia wazi upo kwa Salma
Sijui kwanini hukumuoa Salma, Labda tu hamkukutana mapema
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Machahce nimeyasema uwazi ila mengi yako siyaweki wazi
Wadada kuolewa wala si kazi, Mda mwengine ni uduwanzi
Vimada wako ktwa wako zanzi, Mie ndani nakuna nazi
Trajio langu la ndoa limepota kizani
Angela mekusikia, kilio menifikia
Japo kijaniingia, huruma watafutia
Majirani meniitia, wambea wapita njia
Angela Mke Wangu, yote ulitaka wewe!
Hawaujui ukweli, wa yetu ndani nyumbani
Nje wajifanya asali, ndani kwetu ni vitani
Maneno tu mie silali, lalamikacho sikioni
Angela Mke Wangu, yote ulitaka wewe!
Muulize na Aneti, dada wetu wa nyumbani
Hadi kushushia neti, ulimwita kitandani
Kisa upo kwenye net, bize kutwa jukwaani
Angela Mke Wangu, yote ulitaka wewe!
Ndoa hii meichoka, nyumba ndogo sitoacha
Unaniona mi kaka, nkikugusa w'sema Acha
Kuvuja kwake pakacha, mchukuzi hatoacha
Angela Mke Wangu, yote ulitaka wewe!
Ukweli nakuambia, hata uite ukoo
Ndiyo nitaitikia, kesho nipo kwa Ufoo
Usipo badilikia, Eddy ndo aniweka kwako
Angela Mke Wangu, yote ulitaka wewe!
Maneno ya majirani, endelea kusikiza
Waeleze mtaani, mbeleni watakuliza
Beti zo watazighani, wanifata kuki-giza
Angela Mke Wangu, yote ulitaka wewe!