Angela Kairuki hapa umechemka

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Hamjambo ndugu wanajamvi. Natumaini ni wazima wa afya tele.
Juzi juzi waziri wa utumishi wa Umma Angela kairuki aliutangazia umma(watumishi wa umma) kupeleka INDEX number ya cheti cha kidato cha NNE kwenye wizara hiyo. Na atakayeshindwa kutuma kabla ya mwezi March atakuwa amejifukuzisha kazi.

MTAZAMO WANGU.
1. Mapema toka awamu ya Tano ya serikali ishike madaraka walitangaza kuhakiki watumishi, zoezi ambalo lilibaini watumishi Hewa zaidi ya 16,000 kote nchini. Zoezi la uhakiki wa vyeti pia liliendeshwa kwa ushirikiano na NECTA ambapo NACTE walitoa namba za simu na barua pepe kwa ajili ya kuesaidia kutoa taarifa za watu wanaotumia vyeti vya watu wengine.
Kabla wizara huska haijatoa majibu ya majina ya watu waliokutwa wanatumia vyeti vya watu wengine,Waziri Angela kairuki kaja na wazo la kutuma Index namba ya form four. Hii inamaanisha kuwa serikali haijabaini watumishi wa umma wanaotumia vyeti vya wengine. Nasema haijabini kwa sababu hawa ambao walikutwa wanatumia vyeti vya wengine Leo hii wanapewa nafasi ya kupeleka index namba ya vyeti vya form four ambavyo siyo vyeti vyao. Nimesikitika sana maana kuna watu wengi sana wanatumia vyeti visivyo vyao lakini Leo hii wanahalalishwa na vyeti hivyo kama vile vya kwao.
2. Kupeleka index namba ya kidato cha NNE haitaweza kubaini watumishi Hewa wa serikali kwa misingi ya kuwa wengi wa wanaotumia vyeti visivyo vyao utakuta wamekomea kidato cha NNE. Kwa maana hiyo hawa watumishi hewa(wanaotumia vyeti visivyp vyao) watahalalishwa kuwa ndiyo wamiliki wa vyeti hivyo.

USHAURI
Namuomba Angela Kairuki(Waziri) atoe majina ya watumishi waliobainishwa kama watumishi Hewa wakiwemo wale wanaotumia vyeti visivyo vyao na wale wenye vyeti fake. Mkifanya hivi itawapa nafasi wananchi/ RAIA waliosaidia wizara kubaini watumishi hewa na wanaotumia vyeti visivyo vyao kuweza kujua kama taarifa za wamiliki wa vyeti visivyo vyao wamebainishwa au hawajabainishwa.

MWISHO
Naitumaini waziri wa wizara husika ataliona hili na kulifanyia kazi mapema kabla zoezi la kupeleka/kutuma index number halijamalizika.

Nawasilisha
Wenu
Rais2020
Rais wa Mioyo ya watu
 
Back
Top Bottom