Angekuwa mkristo mngechoma makanisa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angekuwa mkristo mngechoma makanisa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Father of All, Oct 28, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Auawa kwa kuiba mabati ya ujenzi wa msikiti
  Na Sonyo Mwenkale

  Wananchi wa Kijiji cha Kwankonje Kata ya Kwankonje wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, wamemuua mwanakijiji mwenzao, Msingwa Bakari (28) kwa tuhuma za kuiba mabati saba yanayodaiwa ni ya ujenzi wa msikiti.
  “...umati wa watu walizunguka ofisi na kuanza kuchoma moto ofisi alimohifadhiwa mtuhumiwa,” alisema Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Ali Bakari.
  Mtu huyo anayedaiwa kuwa alikuwa mwizi sugu katika eneo hilo, aliuawa kwa kupigwa mawe, magongo na fimbo, baada ya wanakijiji hao kuchoma moto ofisi ya serikali ya kijiji alimokuwa amehifadhiwa muda mfupi baada ya kukamatwa.
  Taarifa zilizopatikana kutoka kijijini hapo na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, zilieleza kwamba tukio hilo lilitokea saa 2:30 usiku wa Oktoba 26, baada ya mtu huyo kudaiwa kuiba mabati hayo yaliyokuwa nyumbani kwa Sheikh mmoja katika eneo hilo.
  Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Ali Bakari ambaye ni mdogo wa marehemu, alisema kwamba juhudi za kumuokoa ili asiuawe na wananchi hao zilishindikana kwa madai kwamba wanakijiji walikuwa wengi walivamia ofisi hiyo na kuichoma moto kwa kutumia mafuta ya petroli.
  “Jitihada zetu za kuwatuliza zilishindwa baada ya wananchi kuchoma moto ofisi kwa kutumia petroli, Msingwa alipoona vile jengo linaungua aliruka na kutoka nje, tukaendelea na jitihada za kumlinda, lakini kuna Sheikh mmoja alianza kumshambulia baada ya wananchi kuona vile ni kama imehalalishwa wakamshambulia kwa mawe, vigogo pamoja na fimbo hadi mauti yalipomfika,” alisema.
  Alisema polisi walipofika walikuta ameshauawa na kuondoka na mwili wa marehemu kuupeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni.
  Kufuatia tukio hilo Mkuu wa wilaya hiyo Rweyemamu, amewaonya wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi kuua watu kwa visingizio vya hasira kali, akisema mwenye mamlaka hayo ni mahakama pekee.
  “Wajua mtu leo ni mwizi lakini anaweza akaacha baadaye akawa mtu mwema katika jamii na inawezekana akawa hata kiongozi na msaada mkubwa kwa jamii. Lakini hatua waliyochukua si sahihi kabisa nataka ikome isitokee tena maeneo mengine Handeni,” alisema.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mauwaji haya si ishara nzuri
   
 3. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  waje zomba na ally kombo (plus the likes) watuambie!
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kama kaiba mabati huyo angechomwa tu maana hapa bongo wezi wanachomwaga kila mahali so sidhani kama inahusiana na dini unaweza ukute hata huyo mwizi mwenyewe ni muislam
   
 5. c

  chief72 JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 567
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hebu soma tena taarifa yako inaonekana hata wewe hujaelewa unachokiandika
  amechomwa kwa sababu mwizi au kwa sababu kaiba tu msikitini? pili kachomwa na raia au na waislamu
   
 6. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  ukweli unabakia palepale hawa jamaa wanachuki sana na wakristo..wangepata sababu ndogo tu ya kutumaliza wangefurahi sana...good news ni kwamba hawawezi ba hawataweza kamwe....
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
 8. v

  valid statement JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hilo lijizi lingekuwa
  linaamini juu ya
  ukristo.Wala usihoji.
  Wangemuua na wangesema
  kanisa limemtuma kuiba
  hayo mabati ili kudhoofisha maendeleo ya kiislam. Wangechoma kanisa
  lililokaribu na eneo husika. iWangeiweka hilo tukio
  kwenye ajenda yao ya
  maandamano haram ya
  ijumaa.i
   
 9. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Just that? Kwa nini Sheikh aliyeanzisha kumpiga huyo mtuhumiwa asikamatwe kwa kosa la mauaji?
   
 10. peri

  peri JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wanaendeleza porojo za kuwapaka matope waislam na uislam.

  Chuki imewajaa mpaka wanashindwa kuelewa wanachoandika.

  Kweli inapodhihiri, uongo hujitenga.

  Mwenyezimungu hamfichi mtu mnafiki, atamuumbu ili watu wote wamjue.
   
 11. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 12. S

  Simba Yuda Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iweni na huruma kwani mwenye uwezo wa kuhukumu kwa haki ni MUNGU pekee
   
Loading...