Ang'atwa na nyoka akizini na mke wa mtu

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,535
Kijana mmoja shija kasamwa mwenye umri wa miaka 28,leo mchana amejikuta akipata masahibu ambayo iwapo atapona kamwe hatayasahau kabisa ktk maisha yake.

Kijana huyo mkazi wa mkoa wa Shinyanga ktk kijiji cha Chela ameng'atwa na nyoka mwenye sumu kali akiwa msituni akivunja amri ya sita na mke wa mtu.

Inasemekana ndio ilikuwa tabia yake kufanya uchafu huo na mwanamke huyo asiye mwaminifu ktk ndoa yake.

Sasa leo kama kawaida yao walijirusha msituni,wakiwa huko kabla hawajaanza kufanya mapenzi walisikia sauti za watu wakija upande waliokuwepo ndipo wakaamua kuingia kichakani kwa hofu ya kuonekana,ndani ya kile kichaka kikubwa kilichokuwa kimefungasha miti mingi kiasi kwamba haikuwa rahisi kuonekana kwao,ndipo wakaamua kufanya uchafu wao eneo hilo ndipo wakiwa bado wanaendelea na starehe ilihali yule kijana akiwa kashusha suruali yake na makalio yake kubaki wazi alishtuka ghafla kang'atwa na nyoka huyo anayesadikiwa kuwa ni aina ya cobra,kelele za maumivu zikakusanya wanakijiji na mke wa mtu akakimbia kwa hofu.
 
Dah hiyo ni noma mkuu nafikiri adhabu hiyo haitoshi kwa mzinzi hasa lakini sijafahamu huyo nyoka amemng'ata sehemu gani au kwenye makalio ambayo yalikua wazi tufafanulie mkuu.
 
Huko Chela ni kijiji anachotoka mh E.Maige. Kuna nyoka wakali sana wanapatikana huko, kiujumla Mkoa wa Shinyanga una majoka hasa pole yake kijana mzinzi .
 
Imeandikwa katka biblia mwanamume mzinzi hana akili kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom