mapema
JF-Expert Member
- Jul 21, 2014
- 962
- 3,011
Naomba kutoa tahadhari kwa wanaotarajia kwenda VETA wawe makini na aina ya fani watakazo chagua.
Miaka ile tunamaliza elimu ya msingi wakati huo kukiwa na uchache wa madarasa ya kidato cha kwanza huko mikoa ya pembeni na uduni wavipato kwa wazazi wetu chaguo pekee lilikuwa ni Veta.
Nafasi hazikuwa zinapatika kwa urahisi na tulipopata wengine kulingana na mazingira ya miji yetu na ushawishi wa watu tulichagua fani zinazo husiana na ujenzi.
Kipindi hicho kwenye fomu ya maombi unajaza fani 3 ile ya kwanza ndio kipaombele chako ndio watakayo kuweka ikiwa nafasi ipo.
Binafsi nilisoma useremala mwaka wa kwanza tulianza vizuri, waalimu wazuri , mazoezi ya kutosha na hatime tukamaliza
Mwaka wa pili nao tuka aanza vizuri na kumaliza vizuri, inga wa kwa mwaka wa pili kuna vitu vingi viliongezeka, masomo ya ujasiria mali kwa sana , somo la uchoraji , kiingereza na sayansi fulani ambayo sijawahi ielewa hadi leo.
baadae tukarudi mtaani kuanza kazi, walao kipindi hiko kulikua na kazi kuliko sasa ila ufundi ni kazi zinazo dharaulika sana, kazi zisizo na thamani, na hata malipo yake hayana thamani hata uongeze thamani kiasi gani.
Tuyaaacha hayo angalizo langu kwenu wasomi mnaotarajia kwenda veta msichukue fani hizi sijui useremala, ujenzi, uchomeleaji nk, nikazi zinazotumia nguvu sana, zenye hatari sana, zinazotumia akili sana japo tunaonekana vilaza , jasho litakutoka sana, kuumia na kutoka damu sana, kutokuwa nadhifu kimavazi kulingana mtindo wa kazi zenyewe, kudharaulika sana , na mwisho hatua za maendelo ni kama hamna !
Mfano mimi tokea 2008 hadi sasa sina kiwanja!
Mwisho kabisa kupitia mijadala ya hili sakata la wasomi kwenda veta limenifungua akili ni kwa nini sisi mafundi tunadharaulika sana kumbe tuna hesabika vilaza!