likandambwasada
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 5,402
- 6,091
Habari za wikiendi wakuu.
Naandika uzi huu kuwakumbusha vijana wote walioajiriwa na TRA katika zile nafasi mpya 400: na hapa nitaegemea kwa wale ambao hawajawahi kufanya kazi katika utumishi wa umma.
Kwanza nawapa hongera wale wote waliopambana na kupenya kwenye mchujo wa watu zaidi ya 8000 na hatimaye kuwa miongoni mwa watu 400 walioajiriwa.
Pili, ieleweke kuwa wote waoitwa kwenye usaili walikuwa na sifa za kuajiriwa ila kwa kuwa nafasi zilikuwa 400 kivyovyote lazima wengine wakose.
Ninawasihi, kafanyeni kazi mliyoiomba na siyo kuweka mbele maslahi yenu.
Aidha, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la 3 la mwaka 2009 mtumishi wa umma anapoajiriwa lazima afanye kazi katika kipindi cha majaribio yaani 'probation' kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja. Kwa wale wanaoajiriwa katika senior post ni miezi sita.
Probation ni sehemu muhimu ambayo mwajiri huitumia kujiridhisha ubora wa mtu aliyemwajiri na mwajiri anayo mamlaka ya kusitisha ajira hiyo endapo atajiridhisha kuwa mtu aliyemwajiri siyo mtu sahihi wa kuweza kutimiza malengo ya kazi husika.
Pia, wakati wa probation hufanyika kitu kinaitwa 'vetting' kwa lugha nyingine ni upekuzi.
Vetting mara nyingi hufanyika kwa siri kubwa ikiwahusiha maofisa mbalimbali wa serikali na idara za usalama unaowafahamu na hata usiowafahamu.
Sasa kwa wale ambao wameomba kazi kwa malengo tofauti na maslahi ya umma basi wajiandae kisaikolojia kwa jambo lolote baya linaloweza kuwakuta.
Aidha ieleweka kuwa serikali ya awamu ya 5 chini mzee wa tingatinga mh John Pombe Magufuli inasisitiza suala la kulipa kodi na ukusanyi kodi ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hivyo basi waajiriwa wapya hamna budi kwenda kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa uzalendo uliotukuka.
Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukufanya uondolewe haraka kazini na kupoteza kazi wakati wa kufanyiwa Vetting ni kama yafuatayo:
1. KUWEKA TAARIFA ZA UONGO KWENYE CV NA KATIKA TAARIFA ZA AJIRA. Hapa inahusisha pia vyeti feki
2. Utovu wa nidhamu
3. Kutoendana na kazi (incompatibility)
4. Utendaji usioridhisha (incapacity/inefficiency)
5. Matumizi mabaya ya madaraka
6. Historia ya kuwa na makosa ya jinai
7. Uzembe kazini (negligence)
8. Siasa kazini
9. Maadili mabovu yanayochafua taswira ya utumishi wa umma
10. Kujilimbikizia mali
11. Rushwa
12. KUTOA SIRI ZA SERIKALI
N.k.....
Hayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kuhatarisha ajira yako na kuweza kukusababisha kuwa suspended ndani ya muda mfupi kazini.
Mwisho; mkumbuke kuwa Vetting ni zoezi endelevu na halina ukomo.
Pia, kama nilivyotangulia kusema awali kwamba kuna wengi walifaulu ila wamekosa nafasi hivyo ukiondolewa inaingizwa reserve list.
Bw. British SAS naamini unausoma uzi huu, punguza majigambo na kuwakera waliokosa vinginevyo unaweza ukashindwa kazi yenyewe bila hata kumaliza mwaka.
NAWATAKIA KILA LA HERI MKAJENGE NCHI NA KUTANGULIZA UZALENDO BADALA YA KUFIKIRIA KWENDA KUJITAJIRISHA
[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
Sheria muhimu za utumishi za kujifunza uwapo kazini
1. Kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la 3 la mwaka 2009. Hii ni muhimu sana inaeleza mambo muhimu sana karibu yote
2. Sheria ya kazi na uhusiano kazini ya mwaka 2004 na code of good practice 2007
3. Sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003.