Kumekuwa na hoja mfu hapa zikipata support ya wana-CCM kuhusu jinsi Mh. Edward Lowassa alivyopokelewa CHADEMA na kuruhusiwa kugoombea Urais. Haya, ngoja tuseme Mbowe alileta hoja ya kumkaribisha Mh. Lowasa kwenye Chama, then, je katika maamuzi yale ya kumpokea si wajumbe ndio walioshiriki katika kudadavua na hatimaye kukubaliana na mantiki ya kumkaribisha Lowasa?
Hivi kweli kama hoja ya kwamba Dr. Slaa aliweka masharti ya kumpokea Mh. Slaa yalipuuzwa na wajumbe na ndiyo maana Dr. Slaa ameamua kupumzika mambo ya CHADEMA, je ni ujumbe gani huu tunaoupata sasa kuhusu Dr. Slaa?? Ni kweli sasa Dr. Slaa ni mtu ambaye akisema hapana au ndiyo na anataka isimame hivyo bila kujadiliwa kwa kuangalia faida na hasara za hoja zake?
Je, kama ni mtu wa namna hiyo, sasa kuna haja gani ya kuwa na katiba ya Chama inayoonyesha namna Chama itakavyoongozwa na kufikia maamuzi kupitia vikao halali vya chama? Ni ukweli usiopingika kwamba ni lazima hoja au ajenda zitoke kati ya wajumbe na zijadiliwe na maamuzi yatafikiwa kwa kuzingatia matakwa ya Katiba na si kwa matakwa ya mjumbe mleta hoja haijalishi awe Dr. Slaa, Mbowe, Prof. Baregu, etc. Sasa kama Dr. Slaa akileta hoja na hoja yake haikupita baada ya kujadiliwa na yeye anaamua kususa, maanake kwamba yeye ni Dictator asiyeamini kwenye vikao halali na mawazo ya watu wengine?
Hakika nimesikitishwa sana na maamuzi ya Dr. Slaa kususia shughuli za CHAMA hasa katika kipindi hiki ambao nafasi pekee ya kupata mtu mwenye influence ametokea CCM na kujiunga CHADEMA. Naomba niseme tu hapa na kulingana na uhalisia wa mambo hapa nchini, Dr. Slaa wa leo hakuwa kwenye nafasi ya kupambana na Magufuli na kushinda. Na kwa msingi huo, Lowassa ni kati ya wachache ambao wanaifahamu CCM in and out na ni mtu sahihi katika kuleta mabadiliko ya kuiondoa CCM madarakani. Hakuna mwingine nje ya Lowasa mwenye nafasi hiyo kwa sasa tuache kujidanganya.
Nasikitishwa sana na hoja ya ufisadi wa Lowasa, swali ni je Katika list of shame je wale wengine mbali na Lowasa wako chama gani kama si CCM? Pamoja na Lowasa kulitolea maelekezo kuhusu ushiriki wake kwenye Richmond kwamba maelezo ya kutositisha mkataba yalitoka juu, lakini bado watu wasiotaka kuwa na fikra mbadala hawako tayari kupokea hilo. Wameendelea kuimba wimbo huo huo wa ufisadi tu hata bila kuangalia je wale wengine tena wengi wako wapi kama si CCM? Hivi mtu kuwa entrepreneurs na kufanikiwa kimaisha ni dhambi? Kama Lowasa ni tajiri kupitia shughuli zake halali sisi tatizo letu ni nini?? In maana matajiri hawaruhusiwi kugombea uongozi? Tuache unafiki watanzania, kwani hata ndani ya CCM kuna matajiri wengi sana lakini wao huo utajiri hauongelewi. Tuache unafiki na kuchafua watu na badala yake tuwe wakweli katika kujadili mambo kwa ujumla bila upendeleo.