Angalizo kwa CHADEMA

Angalizo kwa CHADEMA

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
409
Salamu wanaJF,

Kupitia kauli ya kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya uimarishaji kimafunzo kwa Red Guard, napenda kutoa angalizo hili:

Katika kambi ambazo zinaanzishwa ,kuwepo na tahadhari kubwa kwani wenzetu wa CCM wanaweza wakatumia mchezo wao wa kurusha mabomu, kuteka watu ,kupiga watu aidha kwa kuvizia au kwa njia yoyote ile, tuwe makini na hawa watu.

Nasema hivyo kwa kuwa CCM wamekuwa wakitoa kauli za kupinga kitendo hicho hali itakayopelekea watu wanaohusika kukamatwa ovyo ovyo na kufanyiwa mambo ya ajabu, kwani hawa jamaa (CCM) wanaweza wakawa wamejiandaa kwa lolote.

Lakini kwa kuwa MUNGU yuko upande wa CHADEMA jaribio lolote la kinyama halitafanikiwa, tunaanza na kumaliza na MUNGU.MUNGU ibariki CHADEMA,MUNGU ibariki Red Guard, mipango yote na hila zote za kishetani zisifanikiwe kamwe.
 
Tuwapeleka nje ya nchi kwa awamu hapa Tanzania magamba yatatumaliza kwa mabomu yao.
 
Back
Top Bottom