Angalizo kwa CCM na serikali yake

Angalizo kwa CCM na serikali yake

kinai

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
159
Reaction score
35
Kwa jinsi mchakato wa katiba unavyoendeshwa ni dhahiri kuna dhamira ya wazi ya kutengeneza katiba itakayopendelea serikali ya ccm kwa kuweka mambo mengi ya kuifuraisha serikali ya ccm. CCM wamesahau kwamba kwa katiba mbovu iliyopo waliweza kushinda kwa 60% kutoka 80% ya uchaguzi mkuu wa 2005. Nina uhakika ccm watatumia hila zao kutengeneza katiba ya kujipendelea wao. Lakini wanapaswa kutambua upepo wa mabadiliko unaovuma kwa kasi kipindi hiki na zaidi hii katiba wanayotaka kuitengeneza inaweza kuwa kiboko cha kuwachapia wao wenyewe kwani vyama vya upinzani vina uwezo wa kuchukua mapungufu yatakayojitokeza na kuyafanya agenda yao katika chaguzi zijazo. Hapo ccm itatapatapa sana na kuzidi kupoteza imani kwa wananchi. Mwisho, watawala wa leo ni wapinzani wa kesho, ugumu au ubaya watakaouweka katika katiba mpya hata wao siku moja wataulalamikia na watu watawaambia: " si nyinyi wenyewe mlitengeneza katiba hiyo". Tuache uvyama tutengeneze katiba ya kuinufaisha nchi na watu wake kwa miaka 50 ijayo. Wananchi tuache ushabiki na kutumika tukijua hakuna mwanachama wa kudumu katika vyama vya siasa. Leo chadema kesho unaweza kuwa ccm na ccm ukawa chadema au cuf. Tanzania ni yetu sote
 
Mnalalamika kama wanawake wa nyumba ndogo!!
Join Date : 16th February 2011
Posts : 1,319
Rep Power : 0
Likes Received192
Likes Given11​



Mkuu unajua maana ya Rep Power kuwa 0? Wee ni mbulula usiyeweza kutoka. Post kibao (1,319) zote ni utupu hakuna post hata moja yenye mantiki.
 
Back
Top Bottom