• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Angalizo juu ya msemo huu

bahati93

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Messages
214
Points
250
bahati93

bahati93

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2015
214 250
Hello habari

Huu msemo nimekuwa nikikutana nao mara nyingi pale naposikiliza vipindi vya asubuhi kwenye radio.

Kama leo wakati nasikiliza radio nikashtukizwa kwa kuusikia tena, nadhani hawa watangazaji wanaigana wanavyousema huu msemo bila kuutafakari vizuri kabda hawajaanza kipindi vyao. Huu msemo hauna tofauti na yale maneno ambayo watu wanaongea pale wanapokutana ili tu kutimiza utamaduni wa salamu, kama (unaendeleaje - mtu anakuuliza/unamuuliza pasipo kuwa na nia ya kutatua shida ambayo atakwambia, daah ni siku nyingi hatujaonana - kwa nani hafahamu kwamba hatujaonana siku nyingi)

Okay sasa turudi kwenye msemo ambao naona inabidi kuwa makini kutoutumia hasa hasa asubuhi, msemo wenyewe unaenda hivi WANGAPI LEO WALITAMANI KUAMKA LAKINI HAWAJAWEZA WAMETANGULIA MBELE YA HAKI (maudhui yake yapo hivi una variation mbalimbali).

Sasa jambo ninaloliona ni kama msemo wa kujitamba kwa walio hai juu ya ambao wametangulia msemo unapoteza maana kwa sababu na siku ambapo msemaji atatangulia mbele ya haki waliobaki hai duniani watasema hivyo hivyo juu ya marehemu pasipo kutaja jina, kwani huu msemo unajumulisha marehemu wote.

Tuache huu msemo jamani maana KIFO anatucheka sana tunavyowasemea walitangulia kama vile sisi hatutapata mauti.
 

Forum statistics

Threads 1,405,903
Members 532,149
Posts 34,499,425
Top